TANZIA Aliyekuwa Mbunge wa Mufindi na Waziri wa Elimu Awamu ya Tatu, Joseph Mungai afariki dunia

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
438
munagi 0.JPG

Joseph Mungai enzi za uhai wake

Habari za kushtusha toka chanzo cha kuaminika Hospitali ya Muhimbili kinathibitisha aliyewahi kuwa waziri wa Elimu ndugu Joseph Mungai na Mbunge wa Mufindi amefariki dunia.!

Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.

Joseph James Mungai alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1943

Habari za hivi Punde zilizotufikia na Kuthibitishwa na Mwanae Zinasema Joseph Mungai Amefariki dunia leo Jioni Majira ya saa kumi. Habari hizi zimethibitishwa na Mwanae Kitova
 
Wazee wapumzike wakumbuke kuwa maisha yana mwisho....

Wawe wanatenda mema wanaenda zao.......

Maana huyu ndiye aliua elimu yetu kwa kuchezea chemistry+ physics

Niwakumbushe tena wazee wengine waliobaki siri ya kuishi muda mrefu ni hekima na busara......

Ndio maana Mwinyi anadunda na ni Mwenye tabasamu pamoja na kuwa na miaka karibia 100......

But ...R.I.P.......
 
Habari za hivi Pundi zilizotufikia na Kudhibitishwa na Mwanae Zinasema Joseph Mungai Amefariki dunia leo Jioni Majira ya saa kumi.. Habari hizi zimedhibitishwa na Mwanae Kitova
 
Kama ni kweli Joseph Mungai kafariki basi wameongozana na rafiki yake Samuel Sitta!!
 
View attachment 431075
Josephu Mungai enzi za uhai wake

Habari za kushtusha toka chanzo cha kuaminika Hospitali ya Muhimbili kinathibitisha aliyewahi kuwa waziri wa Elimu ndugu Joseph Mungai na Mbunge wa Mufindi amefariki dunia.!
Tunashukuru kwa mema yote aliyotufanyia watanzania ,kwa mabaya aliyotufanyia tunamsamehe maana hatunaye tena hata tukiyashupalia hasikii wala hatuoni.poleni wafiwa.Mungu amuweke panapomstahili
 
Back
Top Bottom