Tanzia: Aliyekuwa M/Kiti wa CHADEMA Lushoto afariki Dunia

Benson Mramba

Verified Member
Oct 29, 2013
586
1,000
Aliyekuwa M/Kiti na Muasisi wa CHADEMA Wilayani Lushoto Ndugu Zuberi Dhahabu amefariki dunia jana majira ya saa saba mchana. Ndugu Dhahabu aliugua muda kwa mrefu tangu mwaka 2010 baada ya kupata ajali ya pikipiki akiwa katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kwa mujibu wa vipimo vya hospitali Ndugu Dhahabu alipata matatizo katika pingili zake za uti wa Mgongo hali iliyomfanya adhoofu kila siku tangu wakati huo. Alipatiwa matibabu katika hospital ya KCMC, Tumaini na baadae Muhimbili.

Ndugu Dhahabu anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake katika Kijiji cha Dochi Wilaya Lushoto

Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu Mpendwa wetu. Amin
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,520
2,000
Innaillah wainalillah raju'n. CDM ilitoa shilingi ngapi kati ya milioni 390 inazopata kila mwezi ili kusaidia matibabu ya huyu mpambanaji aliyeumia akiwa anasaidia kampeni?
 
mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
RIP kamanda...ndiyo maana Mbowe anasema hiki chama kuna watu wamewekeza mauti,kufirisiwa,jasho na damu alafu kuna baadhi ya watu wachache wanataka kukisambaratisha chama. RIP kamanda
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,520
2,000
RIP kamanda...ndiyo maana Mbowe anasema hiki chama kuna watu wamewekeza mauti,kufirisiwa,jasho na damu alafu kuna baadhi ya watu wachache wanataka kukisambaratisha chama. RIP kamanda
Wapo wanaofia chama na wapo wanafaidi chama. Ule mkopo wa milioni 140 ungeweza kabisa kutumika kumtibu kamanda huyu nje ya nchi akapona. Lakini leo hii akina Josephine ndio wanafaidi damu za watu hawa.
 
Deogratius Kisandu

Verified Member
Dec 2, 2012
1,335
2,000
Innaillah wainalillah raju'n. CDM ilitoa shilingi ngapi kati ya milioni 390 inazopata kila mwezi ili kusaidia matibabu ya huyu mpambanaji aliyeumia akiwa anasaidia kampeni?

john mrema mwaka 2012 alitoa elfu 20 kwa niaba ya chama kipindi cha uchaguzz tamota.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,108
2,000
Namfahamu vizuri sana na kwa maisha binafsi ILA alihamia chama Fulani baadae.....hakua na mchamgo WA kivileeee japo alikua anakula kotekote
 
Deogratius Kisandu

Verified Member
Dec 2, 2012
1,335
2,000
Aliyekuwa M/Kiti na Muasisi wa CHADEMA Wilayani Lushoto Ndugu Zuberi Dhahabu amefariki dunia jana majira ya saa saba mchana. Ndugu Dhahabu aliugua muda kwa mrefu tangu mwaka 2010 baada ya kupata ajali ya pikipiki akiwa katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kwa mujibu wa vipimo vya hospitali Ndugu Dhahabu alipata matatizo katika pingili zake za uti wa Mgongo hali iliyomfanya adhoofu kila siku tangu wakati huo. Alipatiwa matibabu katika hospital ya KCMC, Tumaini na baadae Muhimbili.

Ndugu Dhahabu anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake katika Kijiji cha Dochi Wilaya Lushoto

Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu Mpendwa wetu. Amin

walipomvua uongoz benson mramba hela za michango ya matibabu zikaanza kuliwa.
 
Deogratius Kisandu

Verified Member
Dec 2, 2012
1,335
2,000
Wapo wanaofia chama na wapo wanafaidi chama. Ule mkopo wa milioni 140 ungeweza kabisa kutumika kumtibu kamanda huyu nje ya nchi akapona. Lakini leo hii akina Josephine ndio wanafaidi damu za watu hawa.

kaka mkimpata kisandu atawasimulia kwa machungu kuhusu huyu mzee jinsi alivyotelezwa.
 
Gogle

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
1,483
2,000
Kwanza huyo marehemu alikuwa pro- Zitto au Anti- Zitto?, chadema chumbani au chadema sebuleni?, hebu nyoosha taarifa yako
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,537
2,000
Mkuu, mie sina CHAMA hadi leo hii na sidhani kama ntakuja kuwa na Chama. Next time, usiniandike kwenye List ya Chadema kwani mie huko simo. Mie ni Mpigania haki za Binadamu na siku CDM ikiingia madarakani, ntaanza kuwapinga na wao kama Serikali mara wakianza kuboronga.

Nafikiri utakuwa umenielewa wewe na timu yako yote.

BTW: Natoa Pole zangu kwa Wafiwa bila kujali vyama wanavyotoka na Mungu amtangulie Marehemu na kumlaza pema, Amen.
Hili ni suala la muhimu sana mje hapa mtolee maelezo, sio kukalia propaganda wakati kiongozi wenu amefariki kwa kukosa matibabu stahiki tena bila msaada wowote wakati alipata ajali akiwa katika harakati za chama. Njooni hapa Tumaini Makene, Molemo, mohamed Mtoi, @Dr W Slaa, Josephine, Mungi, Mzee Mwanakijiji, Zitto, Sikonge, alfred Pigangoma, crashwire, GODbles Lema
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,520
2,000
Mkuu, mie sina CHAMA hadi leo hii na sidhani kama ntakuja kuwa na Chama. Next time, usiniandike kwenye List ya Chadema kwani mie huko simo. Mie ni Mpigania haki za Binadamu na siku CDM ikiingia madarakani, ntaanza kuwapinga na wao kama Serikali mara wakianza kuboronga.

Nafikiri utakuwa umenielewa wewe na timu yako yote.

BTW: Natoa Pole zangu kwa Wafiwa bila kujali vyama wanavyotoka na Mungu amtangulie Marehemu na kumlaza pema, Amen.

Nimekuelewa sana mkuu, naomba uniwie radhi kwa yalitokea. Unisamehe mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom