Tanzia: Aliye wahi kuwa RPC wa Mkoa wa Ruvuma na Musoma, Kapita Mwaruka amefariki

D2050

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
1,904
1,067
Inalillahi wainna ilayhi rajiuun,
Aliye wahi kuwa RPC mkoa wa RUVUMA na MUSOMA KAPITA MWARUKA amefariki jana tar17-5 asubuhi mjini Songea.

Mzee Mwaruka yamemkuta mauti hayo baada ya kushuka basi la kampuni ya Super feo akitokea Dar kurudi songea. Taarifa zilizopo mara baada ya kufika ktk stendi ndogo ya Mahenge, alishuka na kisha kuelekea anakoishi lakini hakufika mbali ghafla aliishiwa nguvu na kisha kudondoka.

Bodaboda wa stendi hiyo walienda mara moja kwa mkewe na kumpa taarifa na kumchukua mkewe kumleta sehemu alipo mumewe ndipo alipofanya jitihada za kumkimbiza katika hospitari ya mkoa Ruvuma. Walipo fika OPD mzee aliaga dunia.

Mwili wa mzee Mwaruka unategemewa kuzikwa leo katika makabuli ya Chimgege huko matogoro. Msiba upo seadfarm nyumbani kwa marehemu.

HAKIKA SISI NI WAMWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA
 
Poleni sana wafiwa.

Hizi kazi tunazofanya Mungu atusaidie kutenda haki ili siku tukiondoka tukapumzike.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom