TANZIA: Ajali yaua Padre na Waumini wake huko Masumbwe, Kahama jioni hii

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,509
2,000
Gari aina ya Toyota Hilux imegongana uso kwa uso na lori aina Fuso eneo la Kanegele nje kidogo ya mji wa Masumbwe kuelekea Kahama.

Gari hiyo ni mali ya Kanisa Katoliki Jimbo Kahama, ndani ya gari hiyo alikuwemo Padri Kijana aliyejulikana kwa majina ya Andrew Lupondya ambaye ndie aliyekuwa dereva, kulikuwemo pia na waumini(idadi bado haijajulikana) ambapo inaelezwa kuwa wote wamepoteza maisha.

Kanisa limepoteza padri kijana aliyelitumikia kwa mwaka mmoja tu tangu apewe upadrisho wake!

Mungu awalaze marehemu wote mahali pema peponi.

"BINADAMU TU MAVUMBI, NA MAVUMBINI TUTARUDI! AMINA!

UPDATE

Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Kanegere, Kata ya Bukandwe, Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea jana saa 9.30 alasiri.Habari zilizopatikana usiku huu, zinadai kuwa miongoni mwa watu waliofariki ni Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kahama, Padre ANDREW LUPONDYA ambaye aliwabeba abiria wanaosemekana ni waumini wa kanisa hilo ambao baadhi yao pia wamefariki dunia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Salum Ndimu amekiri kupokea maiti wanne na majeruhi wanane


IMG-20161224-WA0001.jpg

IMG-20161224-WA0003.jpg
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,481
2,000
Habari mbaya sana! Pamoja na yule kamanda kuonekana amelala chini ya gari kwa ukaguzi bado ajali!
Mimi naona madereva hawafikiri wala kufuata sheria za udereva bali wanawaza matrafiki wenye EFD na tochi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom