Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 132
Tanzanite yaendelea kuhujumiwa,wawekezaji wauza madini ghafi nje
Na Mwandishi Wetu
AGIZO la serikali la kupiga marufuku usafirishaji nje ya nchi wa tanzanite ghafi lililotolewa miaka minne iliyopita, limeshindwa kutekelezwa baada ya wadau kuendelea kuuza madini hayo ghafi nje ya nchi.
Uchunguzi umeonyesha kwamba wadau wote wa madini hayo akiwamo mwekezaji wa madini tanzanite, Kampuni ya Tanzanite One ya Arusha bado wanasafirisha madini hayo ghafi kwenda nje kuyauza.
Hali hiyo inatokana na serikali kushindwa kusimamia agizo lake ililolitoa mwaka 2003.
Waziri wa Nishati na madini wa wakati huo, Daniel Yona katika hotuba yake ya bajeti alisema kwamba serikali imependekeza madini ya tanzanite yaanze kukatwa hapa hapa nchini kabla ya kusafirishwa kwenda nje.
Yona alisema serikali imetangaza kusudio la kupiga marufuku usafirishaji nje wa tanzanite ghafi na kwamba kufuatia tamko hilo, wizara ilituma ujumbe kutembelea nchi ambazo huchukua madini ya Tanzanite kama malighafi ikiwamo India, Thailand na Italia.
Alisema katika ziara hiyo waligundua kwamba kusanifu tanzanite nchini italeta faida kubwa na kwamba Tanzania inabidi itekeleze uanzishaji wa maeneo huru ya biashara (EPZ) kwa kukaribisha mifuko ya pensheni nchini kuwekeza katika ujenzi wa majengo ya kupangisha katika maeneo hayo na kuongeza mafunzo ya ukataji vito ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wauzaji wa Madini Tanzania (TAMIDA), Sammy Mollel aliliambia Mwananchi kuwa hatua ya Kampuni ya Tanzanite One kusafirisha madini ghafi kuyapeleka Afrika Kusini kuyauza limechangia kwa kiasi kikubwa kuua soko la madini hayo nchini.
Alisema kuhamishiwa kwa soko la madini hayo Afrika Kusini kumewafanya wanunuzi wazawa kushindwa kupata nafasi ya kununua madini hayo na kuiachia Kampuni tanzu ya Tanzanite one Trading, kununua madini yote na kuyapeleka Afrika Kusini kuuzwa kwa mawakala wao.
"Biashara ya tanzanite hapa nchini imekufa, tumekubali kuhamisha soko na ajira Afrika Kusini, " alisema Mollel.
Pia alisema kupungua kwa upatikanaji wa madini katika eneo hilo kumechangiwa na uamuzi wa serikali kufunga migodi 30 ya wachimbaji wadogo kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea kati yao na mwekezaji Kampuni ya Tanzanite. Zaidi ya wachimbaji wadogo 1,500 wamepoteza kazi.
Mollel alisema wachimbaji hao hivi sasa hawana kazi na kwamba uamuzi huo unaweza kuongeza idadi ya wahalifu mitaani.
Alisema ingawa sera ya madini inasema wazi kuwa mchimbaji mdogo atasaidiwa kupatiwa soko, ufundi na elimu ili aweze kuzalisha zaidi , lakini wachimbaji wa Mererani serikali imewaacha kama yatima.
Alitoa mfano wa serikali ya Thailand ambayo imeendeleza sekta ya madini kwa kuwawezesha wananchi wake kuchimba badala ya kukumbatia wawekezaji kutoka nje.
Hata hivyo, Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Tanzanite One, David Marealle aliliambia Mwananchi kuwa tatizo linalowakabili wachimbaji wadogo Mererani ni kukosa mitaji kwa ajili ya kuwekeza katika uchimbaji.
Alisema madai kwamba madini katika eneo hilo yamekwisha na kwamba kampuni yao ndiyo ambayo imehodhi eneo lenye madini zaidi hayana msingi.
Marealle alisema wachimbaji wadogo kama wangeweza kuungana na kupata mtaji mkubwa wanaweza kupata uwezo wa kununua vifaa vya kisasa vya kuchimba na hivyo kuendelea kupata madini mengi.
"Wachimbaji wadogo, waungane wapate mtaji wa kununua vifaa vya kisasa , madini yapo, lakini kama wataendelea kubaki mmoja mmoja hawawezi kupata madini mengi," alisema.
Kuhusu kampuni yao kuhodhi soko la tanzanite na kupeleka madini hayo ghafi Afrika Kusini kuyauza, Merealle alisema kitendo cha Tanzaniate One kununua madini mengi kimesaidia serikali kupata makusanyo makubwa ya kodi inayotokana na madini.
Alisema kampuni yao inailipa serikali hela nyingi tofauti na zamani ambapo watu walikuwa wakitorosha madini hayo kinyemela na kuyauza nchi jirani bila ya serikali kupata chochote.
Afisa Uhusiano huyo alisema kampuni hiyo hivi sasa imehamishia mjini Arusha makao makuu yake kutoka Afrika Kusini na kwamba ipo mbioni pia kulirejesha soko la madini hayo hapa nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapugi alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kuwa bado makampuni ya madini ya tanzanite yanaendelea kusafirisha madini hayo ghafi kwenda nje ya nchi.
Hata hivyo, alisema angetoa maelezo zaidi kuhusiana na suala hilo baadaye.
Kupungua kwa shughuli za madini Mererani kumesababisha kupungua kwa mzunguko wa hela na hivyo kuwalazimisha baadhi ya wachimbaji wadogo na wafanyabiashara kuanza kuondoka katika eneo hilo.
Mji wa Mererani ambao miaka mitatu iliyopita ulikuwa umefurika watu muda wote wengine wakiwa baa na maeneo mengine ya starehe huku wengine wakiwa katika mashimo wakichimba madini ya Tanzanite hivi sasa, umeaanza kupungua watu.