njundelekajo
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 310
- 227
SIASA ZA AFRIKA NA MAISHA YA WANAHABARI
NA Noel Nguzo.
Wakati huu wa joto la marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar limeripotiwa tukio kutekwa kwa mwanahabari Salma Saidi mwandishi WA Gazeti LA Mwana nchi visiwani humo na mwakilishi wa radio DW ya nchini ujerumani.
Kwa vyovyote vile ni vigumu sana kutohusisha "kutekwa " kwake na siasa hasa katika Uchaguzi "tata" uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani visiwani humo C.U.F
Kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya kulinda waandishi wa habari ulimwenguni(the cometee to protect journalists-C.P.J) ya mwaka 2013 Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo si salama kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao.
Kamati hii iliyoanzishwa mwaka 1992 imesema karibu ya asilimia 20% ya wanahabari duniani wameuawa ama na maafisa WA serikali au na majeshi yake.
Ukiacha tukio la mwandishi huyo WA DW.Yapo matukio yanayoshabihina na na nafasi ya Tanzania iliyopewa na kamati hii kuhusu usalama WA waandishi WA habari.
Desemba 2009 mwandishi Fredrik Katulanda alivamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana kumsababishia kilema cha mguu
Sept 2010 wakati WA kampen za Uchaguzi jimbo LA sumve mwandishi huyohuyo (Frederick Katulamba) alivamiwa na kupigwa na watu takribani 15
Sept 2011 Mwandishi Richard Massatu alikutwa amekufa maeneo ya igoma Mwanza huku macho yake yakifungwa kwa gundi ya super glue.Huyu alikua na mhariri WA Gazeti la kasi Mpya
Vipo pia vifo vyenye utata kama vya aliyekua mwandishi WA I.T.V John Lubango pamoja na aliyekua mwandishi WA radio Kwizera ya nchini Burundi marehem Issa Ngumba
Sept/2/2012 Nyololo mkoani Iringa mwandishi wa chanell 10 Daudi Mwangosi aliuwawa kinyama kwa kinachodaiwa ni mlipuko wa bomu la machozi
Lipo tukio pia la Bwana Absalom Kibanda aliyepoteza jicho lake pamoja na matukio mengine mengi yaliyoripotiwa ambayo ni mengi kimsingi.
Kwa Afrika tukio kubwa LA hivi karibuni ni lile la Nov 2/2013 kaskazini mwa Mali katika mji WA
kidali .Waandishi wawili WA Radio R.F.I(radio France international) Claude Verlon na Chislaine Dupont waliripotiwa kuuwawa wakati WA Uchaguzi wa wabunge nchini humo.
Ripoti zinasema jumla ya waandishi Mia saba kumi na nne wameripotiwa kuuwawa duniani kwa kipindi cha miaka kumi ya hivi karibuni.
NINI CHANZO CHA MATUKIO HAYA?
Jibu unaweza kulipa kwa kufikiri kwa nini hasa Salma Said "ametekwa " kipindi hiki?,Kwa nini iwe sasa wakati huu WA Uchaguzi?
Ukiendelea kuchunguza utagundua matukio mengi yana uhusiano na siasa na hasa michakato ya Uchaguzi.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwanahalisi la mtandaoni(Mwanahalisi online) inadaiwa kua taarifa za awali bi salma alikua amepata taarifa kua anasakwa na jeshi LA polisi kwa hivyo aliamua kutoroka.
Hakuna haja kwa nchi za kiafrika kupoteza pesa na gharama kubwa kufanya "maigizo" ya kukuza demokrasia kama baadhi ya mambo yanayoambatana demokrasia yanaminywa.
Mara zote Siasa za Afrika zimeonekana kuumiza zaidi zaidi baadhi ya makundi ya watu kutokana na nafasi zao za ushiriki katika Siasa hizo.
Baadhi ya watawala wanaamini kuua upinzani ni kudhibiti haki ya raia kupata habari sahihi.Hawa wamesahau hata Mungu alipingwa na viumbe vyake.
Ikishindikana kabisa ni bora ikajulikana tu utawala WA kiimla ndio pekee unaofaaa afrika kuliko kuchagua machache mnayoyapenda ndani ya demokrasia
By Nguzo N.R