Tanzania’s shilling hits record low

Sijui hana washauri huyu mtu.....

Wanipe kazi ya kutoa ushauri wa kuokoa sarafu yetu hal;afu tutunge sera nzuri za Uchumi.Tatizo wanaamini katika Umri wa mtu na hawaangalii uwezo au ukubwa wa ideas za mtu........!
 
Ingawa mie siyo mchumi nadhani kuna kasoro katika uchapishaji wa hizi noti mpya. Noti ni za kiwango duni afadhali hata za zamani. Afrika Kusini noti ya juu ni ZAR 100 sawa na USD 14, Kenya KES 1000 sawa na USD 10 na Uganda UGX 50000 sawa na USD 18. TZS 10000 sawa na USD 5! Bora tupate noti za 20000 na 50000, tumechoka kubeba mzigo wa madafu!
 
Mwl. J.k Nyerere alisema ''Pesa Siyo Msingi Wa Maendeleo'' kitu ambacho hata mwandishi wa kitabu Paper Money Collapse Mr. Detlev Schlichter anakosoa mfumo pesa , sikiliza anavyotupa vitu vyake ktk video hii akigusia pia suala la anguko la thamani , mifumo ya kifedha, monetary theory n.k:



Video kwa hisani ya LibertarianAlliance
 
Last edited by a moderator:
Tungaekuwa hatukuingia mikataba ya madini kimangungo mangungo basi Bank kuu ndo ingekuwa stoo ya madini yetu na kama yangeuzwa nje kutokea hapo, basi sh. yetu isingefika hapo.
 
Wengine wanafurahi sana aisee....maana mfano mtu akituma hela bongo sasa hivi ambayo £1 bongo anapata 2650 kama sikosei, sasa hiyo pound moja mtu unanunua karanga tu basi, hela yetu kwa ujumla imeshuka sana tena sana....sasa hivi watu ndio wanatumia advantage kufanya transaction kutoka international ili wapate hela yetu....

How many people who are in UK or USA send money to Tz? The disandvantage outweighs the advantage.
 
Hii ndio kufa kufaana,wakati walalahoi wanalia na kushuka kwa Tzs wao wanatamani hata ifike 1USD to 2500TZS,ile wale jamaa zao(Wawekezaji) waje kwa wingi,maana kiuchumi wakati mwingine ni vzuri kuwekeza nchi kama hizi wenye uchumi wa kuungaunga au wa kisanii kama wetu.
 
****** na serkali yake woote kichwa cha mwendawazim. Wakati wa mwalim ingawa mambo hayakua mazuri sana lakini pesa bado ilikua na thamani
 
nina mpango wa kuziconvert hela zangu zote za madafu into us$ regardless how little it is...ni hasara kuwa tshs kama una mpango wa kufanya international transactions in the future..
kama ni arbitrageur ni rahisi kupredict...

Lakini kwa kufanya hivyo unakuwa unazidi kuongeza tatizo kwa sabau unazidi kuongeza demand ya dollar, kwa hiyo unateneneza matatizo mwenyewe "self fulfilling prophecy".
 
Back
Top Bottom