Tanzania's National Electoral Commission is toothless

Jan 16, 2007
721
176
Kutokana na matukio mengi na matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi huu 2010, nashauri tume hii ivunjwe na wizara husika wafikishwe mahakamani kwa uzembe au makusudi kwa maagizo ya CCM.

Hii itakua fundisho kwa watakaofuatia.

Kwa uzembe au makusudi wamesababisha masumbufu na kwa baadhi ya wapiga kura kutotimiza haki yao hiyo muimu aidha kwa kuhairisha uchaguzi kwa baadhi ya majibo utalighalimu serekali mamilioni ya pesa kupanga uchaguzi huo upya.

Ukichunguza mtililiko wa matukio kuanzia uchapaji wa karatasi za kupigia kura,idadi ya karatasi n.k.Hainiingii kichwani kwa tume ambayo iko kwa ajiri hiyo wasijue idadi kamili ya wapiga kura katika jimbo husika? Au kuchanganya karatasi zipi ziende wapi? Au nembo za wagombea ni wazi kulikua na samples za karatasi hizo kabla ya kuchapishwa.

Hatua kali zinapashwa kuchukuli kwa vingozi wa tume n,waziri muhusika na wote waliohusika na mchapishaji kama kosa ni lake afidie gharama zitakazotokana na kurudiwa uchaguzi.

Vinginevyo itatufanya kuamini au kuthibitisha imani yetu kwa mchezo mchafu wa CCM.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Hakuna haja ya mahakama tuwapotezeeeeeeeeeeeee
Kama enzi za Stalin Urusi
 
Tume hii kwanza ijiuzulu kabla haijafikishwa mahakamani, maana naona ni wahuni zaidi ya wale vibaka wa gizani.

Hatuna tume bali tuna genge la wahuni

i repeat
hatuna tume bali genge la wahuni

bila tume huru, msuli unakuwa mkubwa sana, hata hizi kura tunazoelezwa nazo pia zinauwalakini kama mtu anapewa kura tatu mtu mmoja na inakuwa imepangwa tayari.

Kumbe malalamiko ya upinzani wa kuwepo extra vote ni ya kweli.
 
Mmewatangazia watu chadema imeshinda shy na tena tbc wanatangaza ccm imepita kwa kura moja.. Msituchezee kabisa.
 
Ivi kweli kuna mtu mwenye akili timamu asiyejua kuwa NEC wanafanya hila kubadilisha matokeo?
Ivi kweli unaweza kusema huu ulikuwa uchaguzi huru na kweli Tanzania?
NEC wametia aibu Tanzania
CCM wametia aibu
Na watanzania mtatia aibu kama kweli mtakubali haya matokeo!
hatuwezi kusubiri siku 5 za kuhesabu kura mil 19!
Ukimya wa CHADEMA nao unanipa mashaka! Come out, speak out! Mbona mnakubali unyanyasaji na inefficiencies za ajabu? Hamjui kuwa nyie ndo sauti ya wananchi? Mnawezaje kuwa People's Power huku mnawasaliti wananchi na ukimya wenu?

Wito kwa WaTz...Tusikubali matokeo yoyote yenye utata! Uchaguzi ni haki yetu kwenye katiba. Na imedhihirika kuwa NEC wanataka kusaliti hii haki! TUSIKUBALI.
 
Chadema chama makini sana. Sina wasiwasi na 'vichwa' vinavyokiongoza chama hiki makini.

Tulia.

Sote tuna ham na mabadiliko. Tulia.

Chadema is "Tanzanian Dream"
 
Inakera sana kuona vurugu zinazotokea na watu kuumizana na pengine kuuana kwa ajili ya nec kukosa msimamo na kusimamia haki. Jamani kwa mwendo huu tuko wapi? Enzi za ukoloni watu walitumia kura kuwaondoa wakoloni na waliheshimu kura za watu.je sisi wengine ni watu waaina gani?

Inasikitisha kuona katika karne hii..... Bado tunantumia nguvu mbona ni karne ambayo iko kinyume kabisa na mambo ya aina hii ni aibu kubwa kwa taifa kwani taarifa zinapatikana kiurahisi mno kuliko huko nyuma.

Jamani bado tanzania kunakazi kwa nini tulikubali vyama vingi?mie sioni sababu yakujiita nchi ya demokrasia huku hatuna ari ya demokrasia jamani kama nec haitakuwa huru tuache chaguzi za vyama vingi tutatoana ngeu kila siku na kusambalatisha taifa
 
huyu makame kama damu ikimwagika lazima ailipie, yeye na ccm yake watalipa tuu believe you me!
 
Hata kwenye tovuti yao wanachindwa kuweka hata majina ya wagombea wa mwaka huu! Matokeo ndio uote ndoto. Naona mstari moja tu "TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAANZA KUTANGAZA MATOKEO YA AWALI YA URAIS" basi!! What a shame!!
 
Mtu mwenye busara siku zote huwa hakurupuki kwenye maamuzi. Unajua hivi sasa CCM na serikali yake inataka pa-kusingizia.
 
Mzee kila mtu anayaona yanayotokea, na kukurupuka kuongea unaweza ukapoteza mengi. Hapa chama kinaoperate chini chini na kinafanikiwa. Hakuna mambo yatakayoaribika. Chama kina mfumo mzuri wa kushughulikia maswala yake hasa ya uchaguzi, chama kilijipanga na kilijua haya yote yatatokea. Sasa mkubwa usiwe na hofu mambo yataenda shwari, tuliposhinda patatangazwa tumeshinda. Naomba tuwe wavumilivu, CHADEMA si chama tu bali ni taasisi(institution).
 
hatukurupuki hovyo, sisi chadema tunajua njama ambazo nec inafanya km kada wa ccm pale itv rainfred masako anavyozuia matokeo yasitangazwe eti sio rasmi.
 
Usitutie moyo tu hii habari ni kweli? i hope iwe kweli coz kinachoendelea sasa nec
 
ivi kweli kuna mtu mwenye akili timamu asiyejua kuwa nec wanafanya hila kubadilisha matokeo?
Ivi kweli unaweza kusema huu ulikuwa uchaguzi huru na kweli tanzania?
Nec wametia aibu tanzania
ccm wametia aibu
na watanzania mtatia aibu kama kweli mtakubali haya matokeo!
Hatuwezi kusubiri siku 5 za kuhesabu kura mil 19!
Ukimya wa chadema nao unanipa mashaka! Come out, speak out! Mbona mnakubali unyanyasaji na inefficiencies za ajabu? Hamjui kuwa nyie ndo sauti ya wananchi? Mnawezaje kuwa people's power huku mnawasaliti wananchi na ukimya wenu?

Wito kwa watz...tusikubali matokeo yoyote yenye utata! Uchaguzi ni haki yetu kwenye katiba. Na imedhihirika kuwa nec wanataka kusaliti hii haki! Tusikubali.

no research no right to speak, kama kawaida chadema huwa hawakurupuki. Ni lazima wawe na concrete evidence. It will be great irresponsibility kwa chadema kukurupuka na unfounded statements ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani. Kama chama makini ni lazima pia chadema itafakari athari za kauli zake kwa taifa, wananchi na amani na utulivu badala ya kufikiria tuu kwenda ikulu.
 
Vyovyote iwavyo ccm haitakiwi kwa asilimia kubwa sana..
 
hatukurupuki hovyo, sisi chadema tunajua njama ambazo nec inafanya km kada wa ccm pale itv rainfred masako anavyozuia matokeo yasitangazwe eti sio rasmi.

Halafu anaboa wa Tanzania sana huyu jamaa. Mimi napenda haki hata pale chama changu kinapobwagwa kwa haki napenda kuwa fair. Anapoona matokeo yanayomfurahisha yeye, naanza kuyapigia debe na kuonyesha yalivyo mazuri kuliko mangine, poor him. Msameheni bure...hajui alitendalo. Hajui Tanzania kwanza, vyama baadaye. Vurugu zikiibuka bibi yangu aliyepigia CCM anaweza kuuawa nazo kwani vurugu haina macho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom