Tanzania's media UOZO mtupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania's media UOZO mtupu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Jan 25, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kwenye strong democracy yoyote ile Media ni kama 4th estate lakini kwetu inaonekana kama vile media kazi zao ni kuserve special interests be it ziko owned na Chama tawala, serikali,opposition, vikundi vya dini au watu binafsi

  sielewi inawezekana vipi ufisadi unaofanywa PPF media ikawa kimya namna hii...najiuliza Freemedia au IPPMEDIA au akina MWANAHALISI au UHURU na DAILY NEWS mbona wako kimya namna hii?

  Je is it fair kusema kuwa media in Tanzania hawana interest na waTanzania bali wao ni special interest groups bas au ndio tuseme they just dont care?

  The same applies na ufisadi BRELA, TRA, UJENZI na sehemu zinginezo

  To be honest saa zingine mie naona kichefu chefu asubuhi nikiona headlines za magazeti yetu. Hakuna investigative journalism, waandishi wa habari ndio hao hao wa kuunganisha unganisha, ukisoma business news ndio matapishi matupu. the only paper ambao naona kidogo wanafadhali na wako detailed ni THE CITIZEN sasa sijui sababu wanajaribu kuwa kama DAILY NATION la Kenya au vipi


  Naona solution ni social media kama twitter,facebook groups and so on. Otherwise relying on the Kubeneas will not get us anywhere
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  You can say that again!! people dont know what and how media should be. Media cook stories and write what people wish, this is the order of the day!! to them mwanahalisi is unique news paper..what a joke!
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  waandishi wenyewe ngumbaru 'kanjanja' ndo maana Mkapa aliwaponda wote wako hapo ktk hyo fani kuganga njaa wanaandika news bila reliable sources sometime kilichoko ktk headline sicho kinachosemwa ndani, yaani wanaangalia mauzo tu. Hata habari za soka la majuu wanakosea na ni za kusoma from net sometime nahisi ka hawajui lugha sijui wanalipua au hamna weledi? Patamu ni pale kuna statics fulani wote walikuwepo ktk press conference ila data zitatofautiana! Yani huwa nakasirika acha tu kwenye magazeti mimi huvutiwa zaidi na kingo, bi mkora, chezo na kipanya huko kwingine aagh mradi nipoteze muda. Hayo ya udaku ndo hata staki kuyaangalia coz they are full of nonsense.
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,229
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Ndugu...penye siasa haya hayakwepeki...si Tanzania tu...ukishalitambua hilo haitakupa taabu! Usipende tu yanayosanifu mawazo yako...hata machungu meza tu,badae utajua ukweli uko wapi!
   
 5. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  The problem isn't Media, the problem is what is news to Tanzanians! Media write not for themselves, they do for the audience and they have researched what the Tanzanians want. They give them what they want... That's all about free market economy!
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  In fact magazeti karibia yote nchini ni ya udaku only that mengine udaku wake ni wa kijamii na mengine wa kisiasa. Ebu soma Alasiri, Dar Leo, n.k. Utashangaa. Vichwa vya habari ni vya kuuza gazeti. Ukiingia ndani habari mistari minne na mwandishi ameandika kwa hisia zake tu. Ndiyo maana mzee nkapa aliwatukana hadharani kwamba ni waandishi habari uchwara!

  Ni magazeti machache sana angalau yanajaribu kuandika habari za uchunguzi japo nayo yanakosa weledi fulani. Hata mimi ninafurahishwa na katuni zaidi kuliko habari.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mfano kama habari hii hapa chini, huu sijui ni uandishi wa wapi!!!!!!! Halafu eti ndiyo gazeti la serikali
  Yaani ni ushabiki mwanzo hadi mwisho, pnapotolewa criticism ni kwa mjumuisho jumuisho tu. Hakuna kusubstantiate wala kutoa mifano halisi.

  Mbunge azuia michango ya maendeleo

  Source: Habari leo

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Singida; Tarehe: 25th January 2011

  MBUNGE wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, amepiga marufuku michango yote ya shughuli za maendeleo jimboni mwake kwa madai kuwa shughuli hizo ni jukumu la Serikali iliyopo madarakani.

  Akizungumza bila hata kuzingatia umuhimu wa wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo yao, mjini hapa juzi Mbunge huyo alisema pia anakusudia kupeleka bungeni hoja binafsi kuzuia michango hiyo nchi nzima na kuondoa vizuizi barabarani kwa kuwa mambo hayo hayapo kisheria.

  Mbunge huyo ambaye katika jimbo lake, michango ya wananchi ilifanikisha ujenzi wa shule za kata, bila kuona faida wanayopata wanafunzi katika shule hizo, alisema kwa vile michango hiyo haipo kisheria, basi hakuna uhalali wowote wa kuendelea kulipa.

  Kwa mujibu wa madai ya Mbunge huyo, ambayo hayaelekei kutambua hata juhudi za wahisani ambao wamekuwa wakichangia sehemu ya miradi ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kuchangia sehemu iliyobakia, alidai kufanya hivyo ni kuendelea kuwaneemesha watendaji serikalini na katika halmashauri.

  "Huu ni unyang'anyi na unyanyasaji mtupu wa wananchi ambao hausaidii chochote zaidi ya kuwaneemesha watendaji," alisema mbunge huyo bila kutambua kuwa miradi mingi katika makazi ya wananchi, imefanikiwa na kuwanufaisha wananchi baada ya kuhamasika kujitolea na Serikali na wahisani wakasaidia kilichobakia.

  Amesema hata mwanafunzi anapochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Serikali, hutakiwi aende na michango kama ya taaluma, mlinzi, mahafali, dawati, ndoo, jembe na hata fagio mbali na karo ya shule.

  Akitoa mfano, alisema katika mwaka wa fedha 2009/2010, zilitolewa Sh bilioni 2.151 kwa ajili ya shughuli za elimu Mkoa wa Singida, lakini mkoa ulirudisha Hazina kiasi cha Sh milioni 465 baada ya kushindwa kuzitumia.

  Pia amesema vizuizi vyote vya barabarani kwa ajili ya kukusanyia ushuru wa mazao unaokwenda halmashauri katika jimbo hilo vimeondolewa.

  Alisema amefanya hivyo kwa kuwa mmoja wa mawaziri wa zamani, Hassan Ngwilizi alishavipiga marufuku nchi nzima mwaka 2002 na hivyo kuwepo kwake ni haramu na kunasababisha kero nyingi kwa wananchi.

   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hawa ndiyo waandishi wanaolala kwenye vilabu vya mataputapu na asubuhi anadamkia kwenye vyumba vya habari. Hata kwa kulazimishwa siwezi kusoma upupu huo. Naweza kuvumilia kutazama kinyesi lakini siyo kupitisha macho kwenye habari hii.
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Je is it fair kusema kuwa Media in Tanzana wanaongoza kwa kudidimiza democracy?

  Nazungumzia media isiyouliza issues za checks and balance serikalini au transparency this is dangerous

  No wonder siku hizi hata JF watu washaacha kuleta quoteza na news clips kwani washajua hawana jipya media yetu
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,553
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu SLIDINGROOF, hauitendei haki kwa kuuita Tanzania Media, uozo mtupu!. This is not fair, umegeneralise too much na kuzitumbukiza media zote na waandishi wote kwenye tenga moja la samaki, na kuconclude wameoza wote.

  Viko vyombo vya habari na waandishi individual, vimefanya/wamefanya kazi nzuri huko nyuma na wanaendelea kufanya kazi nzuri hata sasa, hivyo sio haki kuwabeza wote katika ujumla wao.

  Japo nakubali tasnia ya habari kuvamiwa, lakini still there are the few ones ambao they are still the good ones.

  1. Hivi unaelewa what it takes to be ana investigative journalist?.
  2. Hivi unafahamu media situation ya hapa kwetu na maslahi ya waandishi?.
  3. hivi unafahamu watu kama kina Ben Mkapa, Dr.Sengodo Mvungi, Dr.Harison Mwakiembe, Priof. Palamagamba Kabudi, wote walikuwa waandishi na wakaikimbia fani?, unajua kilicho wakimbiza?.
  4. Hivi unajua kilichopelekea Jenerali Ulimwengu na himaya yake ya magazeti kwa nini alianguka na kulazimika ku hand over kwa mafisadi na yeye kujibanza pembeni na ka Raia Mwema kake ka weekly?.
  5. Do you know what does it take to create Ted Turner, Rupert Mordoch, Sulvio Belusconi and the Maxell kind of people?.
  6. Hivi unajua Media mongul wetu Mengi, anachota huku kujazia kule ili kuiendesha media empire yake?
  Kuna mengi tusiyoyajua kuhusu media yetu, tusiishie kulalamika tuu na kulalama, hebu tuangalie mazingira ya kazi za media zetu.
  Kusema kweli, waandishi wetu, wanafanya kazi kwenye very pathetic situation, ndio maana mimi binafsi, naunga mkono kwa nguvu zangu zote, those 'little brown envelopes', not for 'petty cash journalism', but only for facilitation!.
  Hebu kubali kwanza, no matter how bad our media/journalists are, there are some good ones ili niweze kuendelea kuchangia...!
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pasco umeelezea vizuri na kupelekea any sensible person ku-sympathize with the situation. Ila hapo kwenye quote naona kidogo sijaelewa!!!!!! hahah ahahah ahahah ahah!
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  will be back in few kukujibu kwa kirefu zaidi.
   
 13. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Slidingroof,

  Kwa kweli nimekukubali unaposema kuwa media za TZ ni kuzungumkuti uko sahihi kabisa kwani wanaJF wanajitahidi kumwanga ma-newz mengi sana tena yenye ushahidi wa kutosha ambao hata mtu au kikundi cha watu kudai kuwa wamezushiwa na kwamba gazeti litashitakiwa kwa ku-cook data. Mfano mtu kama kubenea always yuko mstari wa mbele kuboresha habari kwa kina lakini madudu ya PPF mbona kakaa kimya kama vile kapewa mrungula. Hizo nondo za ppf zingempa ujiko ambao hauna mfano kwani chati ya paper yake ingepanda sana. Alafu wanachama wengi wanaochangia ppf hawasome JF mfano huko mikoani hakuna mitandao na magazeti huwa yanafika bila kikwazo. Je kwa hili wana media mgeuza sana ma-newz papers yenu hizi wikileaks-tz zilichambuliwa kwa umakini wake.
   
Loading...