Tanzania's Land Act of 1999 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania's Land Act of 1999

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 6, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  A portion of the act states this

  Swali linakuja, je Rais akitumia madaraka yake vibaya na kuigawa ardhi hii bila kujali maslahi ya Taifa, lakini kuna kinga kama hii, je kama Taifa tufanyeje?

  Je jinsi tulivyotoa ardhi kwa Grumeti, Loliondo, SEKAB na sasa South Korea na Saudi Arabia, je nao watanufaika kwa kufidiwa pindi watakapopaswa kuhamishwa au kunyang'anywa ardhi?

  Je mtu kama James Sinclair na Tanganyika Range ambao ndio wanahodhi kwa ujumla ardhi yote ya Tanzania iliyo na madini, ni nani aliwapa mamlaka makubwa namna hiyo na ikiwa itabidi kuwafukuza au kuwanyang'anya ardhi kutokana na kutambulika kuwa Uongozi wa nchi uliokuwa na dhamana ulikodisha na kumpa Sinclair ardhi hii si kwa manufaa ya Taifa letu, ni nani atamfidia Sinclair ambaye atakuwa tayari kutumia hii sheria yetu ya 1999 kudai fidia?
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mi nadhani its about time, watu waanze kurudi particulary mtu kama Rev ukirudi au hata usirudi upewe nakala moja na gazeti la kibongo ambalo lina big circulation hili watanzania waelimishwe.

  Haya mambo kwa kweli yana chosha and its about time JF focused on waking up the nation. Hawa wapinzani wako more interested na malumbano yao rather than haki ya mtanzania no difference between them walio CCM or outside.

  None of them wana concentrate na jamii bali politicians. Hata sijui kwanini hawaelewi wanasiasa hawapigi kura ya kuangusha uongozi bali wananchi. Kama wale wamasai wauko loliondo, na sehemu zingine zote watu wanaofukuzwa kinyama nyama.

  Lets be realistic wengi si wapiga kura humu and our daily breads are earned in different continents.Fimbo ya mbali aiui nyoka na huo ndio ukweli wenyewe. Bali JF sasa inahitaji kuwa fahamisha na kuwaelimisha watanzania. Namna moja ni mastaa wa Jf watafutiwe nafasi za nakala ili kuwaamsha watanzania wengi. Kama JF ilivyo niamsha mimi. Persistence pays one day wataamka, lakini si kwa namna hii inayoendelea humu ndani, its about time the battle is taken where it matters the most. Na hii ni kuwaelimisha watanzania
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Rais akitoa ardhi bila maslahi ya wananchi..anapigiwa kura za kumwondoa (uchaguzi)

  Atakayechaguliwa kwakuwa ardhi iko chi yake ana uwezo wa kumnyang'anya mtu yeyote wakati wowote kwa niaba ya wananchi wake.
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  ukinyanganya unapigwa madai ya fidia ya kufa mtu , kama ulivyo kuwa mkataba wa iptl, hapo serikali yenyewe iunaufyata mkia, au unampa jamaa mapato yake ya miaka mia ijayo.
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama hiyo ndiyo tafsiri yake kisheria then...wapinzani wangekomaa nalo hilo kuliko kuzunguka kwenye issue moja (ufisadi) miaka minne...

  Hiyo ni very serious weakeness kwenye sheria ya nchi hasa kwa kitu muhimu kama ardhi...
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Je Mwinyi alipotoa Loliondo, aliondolewa kwa kura au ni muda wake ulifikia kikomo?

  Je Mkapa alipojipa Kiwira na kutoa Baraka kwa kina Barrick, aliondolewa kwa kura au muda ulifikia kikomo?

  Je Nyerere alipotaifisha mali binafsi 1967 (sijui sheria ilikuwa inasemaje wakati ule) au lile hamisha hamisha la vijiji vya ujamaa, je aliondolekwa kwa kunyimwa kura au aliamua kujiondoa mwenyewe?

  Ni lini katika Afrika au Tanzania in particular kuwa kiongozi anaondolewa madarakani kwa kura kutokana na tathmini ya kweli kuwa kashindwa madaraka au katumia dhamana vibaya?
   
 7. K

  Kleptomaniacs Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kesi zote zinazohusu masuala ya utwaaji,uhawilishaji wa ardhi etc husikilizwa na mahakama kuu kitengo cha Ardhi, endapo una uhakika kuwa Rais amefanya maamuzi bila kuzingatia maslahi ya taifa kwa mujibu wa sheria ya utatuzi wa migogoro ya ardhi na sheria za ardhi ambazo ndiyo hasa chanzo cha sheria hiyo una fursa ya kufungua mashtaka kuhoji uhalali wa mamlaka ya Rais, Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi inahusika na kesi zote zinazohusiana na sheria ya uwekezaji, mamlaka ya Rais ya utwaaji.​

  Kuhusiana na suala la madini, inafaa kujua tafsiri ya ardhi inahusisha vitu gani ili tusichanganye mambo, Ardhi kwa mujibu wa Sheria ya ardhi, imefafanuliwa kuwa ni ile inayojumuisha vitu vyote vilivyo juu na chini ya uso wa nchi vikiwemo majengo, uoto wa asili na maendelezo yote yaliyofanywa isipokuwa madini na bidhaa za mafuta na gesi, kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha sheria ya ardhi namba 4 ya 1999. Hii ina maana kuwa madini, mafuta na gesi si sehemu ya ardhi kwa mujibu wa sheria ya ardhi na usimamizi wa raslimali hizo upo chini ya mamlaka husika ambayo ni wizara ya nishati na madini. Usimamizi wa rasilimali hizi uko chini ya sheria ya Madini Namba 5 ya 1998. Lakini kwa vile madini yapo ardhini, kuna uhusiano mkubwa kati ya ardhi na madini na uvunaji wa rasilimali hiyo unaweza kusababisha mgongano baina ya watumiaji. Hivyo sheria ya Madini inatoa maelekezo juu ya taratibu za uchimbaji madini katika maeneo yaliyoko ndani ya mamlaka iliyosajiliwa kisheria au kimila. Kwa undani zaidi tazama vifungu vya 94-96 vya sheria ya madini ya 1998. ​
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naomba kurudi hapa kwenye hili suala la ardhi kwa kupitia habari mbili ilizotokea tangu niandike thread hii ambazo zinahusiana na masuala ya ardhi na soko la ardhi na maendeleoa ya nyumba.

  1. Benki Kuu kutumia fedha nyingi kujenga nyumba z aGavana na Manaibu wake
  2. Kubadilishwa kwa Vyeti vya Umiliki na gharama zake.

  Je ni jukumu la nani na ni mamlaka gani inayodhibiti mfumuko wa bei za ardhi na shughuli nzima za ujenzi wa nyumba ikiwa ni pamoja na malighafi za ujenzi?

  Ni nani aliyethaminisha kwa mfano eneo la ardhi zilipojengwa nyumba za Benki Kuu na kudai kuwa maeneo hayo yana thamani ya kiwango cha juu kiasi hicho?

  Je uholela huu wa bei za ujenzi na ardhi unaathiri vipi mfumo wa uchumi wa Taifa letu na zaid thamani ya sarafu yetu?

  Kama Rais ndio mwenye dhamana ya kuilinda ardhi, kwa nini kwa kutumia madaraka yake na Wizara husika ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya miji, hata Wizara ya Ujenzi na Miundo mbinu hawajaweza kuweka kipaumbele cha kulea sheria bora za ardhi na umiliki wake na kuweka viwango vya thamani vinavyoeleweka?

  Je kwenye ardhi na maeneo ambayo biashara ya viwanja na bei zake ni za kupindukia, Serikali inakusanya mapato inavyotakikana au kuna upenyo unaoruhusu watu kujineemesha kwa kuuza ardhi, nyumba na umiliki mzima wa ardhi bila kulipia kodi za mauzo hata kodi za ardhi kulingana na viwango vya uthamani wa ardhi vilivyoko Wizarani (Sales tax, property tax)?
   
Loading...