Tanzania's gold exports rise 23% in year to July - Central Bank

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,229
662
Reuters said:
- Tanzania’s gold exports rose 23% in the year to July, its central bank said on Thursday. Africa’s fourth-biggest gold producer after South Africa, Ghana and Mali hopes to see a rebound in its mining sector after a tax crackdown and overhaul of its mining code in 2017 spooked foreign investors.

“The value of gold exported (in the year ending July 31) ... …. grew at an annual rate of 23.3% to $1.783 billion because of an increase in export volume,” the (central) Bank of Tanzania in its latest monthly economic report. The report did not provide figures for export volumes.

The country’s gold exports in the previous year amounted to $1.45 billion. Gold accounts for more than 40 percent of the East African nation’s non-traditional exports. Tanzania exported gold worth $1.549 billion in the 2018 calendar year, up slightly from $1.541 billion a year earlier, central bank data shows. Tanzanian President John Magufuli, who took office in late 2015, is pushing for more revenue from the mining sector, which is a relatively small contributor to national output.

In 2017, the government passed laws which the industry complained would be costly and onerous. Among other things, the laws hike taxes on mineral exports, mandate a higher government stake in some mining operations and force the construction of local smelters, a move some companies said was uneconomic. Magufuli also ordered the central bank in January to start buying the country’s gold to curb smuggling and build reserves to stabilise the local currency.

Hizi habari ni njema kwa taifa letu.
 
Naunga mkono hoja, kumbe ni kweli tulikuwa tunaibiwa sana, kama tumezuia makanikia, tumesitisha uzalishaji North Mara, na gold export zimeongezeka, then tulikuwa tunapigwa kweli kweli, sasa tukiruhusu makinikia na kufungua North Mara, si Gold export zitapaa?.

This is very good news.
P
 
Hiyo report haioneshi volume imekua kwa kiasi gani. Inawezekana increase iliyopo ni kwa sababu bei ya dhahabu imepanda duniani na pili inawezekana increase in volume isitokane na kuibiwa Bali kuongezeka kwa uzalishaji.

Mgodi si mahala ambapo production huwa constant siku zote. Sometimes production huongezeka.

Inawezekana pia zamani tulikuwa tunaibiwa. Kupata jibu sahihi la nini hasa kimetokea ilitakiwa BOT watusaidie kujua volume imeongezeka kiasi gani; bei ya dhahabu imepanda au kushuka kwa kiasi gani; production trends za migodi zikoje; na je uzalishaji wa migodi yote ukoje kulinganisha na huko nyuma?
 
Ila sasa mbona Maisha magumu na ajira hakuna?

Maisha magumu na hizo data nina uhakika ni za kupika kama Kagame.
Period.
 
Uncle wangu unajua kuna ndugu zako 110 wamepoteza kazi huko North Mara?, watoto wao watakula nini?, vipi ndugu waliokuwa wanawategemea
Siungi mkono mtu yoyote kupoteza ajira, ila pia kuna wakati inafikia hakuna jinsi yoyote kwa entity ku survive bali ni lazima ipunguze wafanyakazi.

Mpaka sasa ban on export gold concentrate inaendelea, mgodi ume change umiliki toka kwa Acacia kwenda kwa Barrick, tena kwa taarifa tuu sio North Mara pekee watapunguza wafanyakazi bali migodi mingine itafuata, na taasisi kibao zinafuta due to shrinking economy.

Mimi tuu mwenyewe na kakampuni kangu ka PPR, nilikuwa na wafanyakazi 20, tukipanga jengo zima la NHC pale mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango ya mshahara wa DC!. Baada ya kuingia Magufuli, mambo yamebadilika, nimelazimika kupunguza wafanyakazi 15, tumebaki 5!. Mkwepu tumehama tumehamia Posta House kwenye kajichumba tuu!.

Ila pia Mungu nae ana mipango yake, hivyo hao watakao punguzwa kazi, watalipwa golden handshakes ndefu nene, wenye akili watapata mitaji na kuendesha maisha mazuri zaidi, na wengine watazitumbua na kusubiri kudra za Mwenyezi Mungu.
P
 
Mpaka sasa ban on export gold concentrate inaendelea, mgodi ume change umiliki toka kwa Acacia kwenda kwa Barrick, tena kwa taarifa tuu sio North Mara pekee watapunguza wafanyakazi bali migodi mingine itafuata, na taasisi kibao zinafuta due to shrinking economy.
Kwahiyo ume declare kwamba uchumi unashuka, at the same time unasema uchumi unapanda msimamo wako upo wapi?
 
Ila pia Mungu nae ana mipango yake, hivyo hao watakao punguzwa kazi, watalipwa golden handshakes ndefu nene, wenye akili watapata mitaji na kuendesha maisha mazuri zaidi, na wengine watazitumbua na kusubiri kudra za Mwenyezi Mungu.
Nakubaliana na wewe 100% Mungu anamipango yake sawa, jamii zinazozunguka migodi hiyo je uchumi wake utabaki the same?, hao watu wakilipwa hiyo unayoita golden shakehand unauhakika maisha yao watakuwa wanaishi karibu na migodi ili mzunguko wa hela usipungue maeneo hayo?, hili swala ni pana sana na majawabu yake yanahitaji hekima kubwa mno
 
Kaka mungu Hana jembe wewe Lima ukivuna ndio anabariki kazi ya mikomo yako, hakuna Baraka kwenye kufutwa kazi
 
Nakubaliana na wewe 100% Mungu anamipango yake sawa, jamii zinazozunguka migodi hiyo je uchumi wake utabaki the same?, hao watu wakilipwa hiyo unayoita golden shakehand unauhakika maisha yao watakuwa wanaishi karibu na migodi ili mzunguko wa hela usipungue maeneo hayo?, hili swala ni pana sana na majawabu yake yanahitaji hekima kubwa mno
Mwalimu wa Tuisheni, umeisha wahi kutembelea maeneo yenye migodi mikubwa?. Tuanzie na Mwadui, nenda Kahama, nenda Geita, nenda North Mara, Bulyankhulu etc, angalia maisha ya mgodini na maisha ya nje ya mgodi ni mbingu na nchi!. Migodini wanaishi kama peponi huku nje ya migodi ni kama Jehanum kwenye umasikini uliotopea!.

Thanks to CSR projects ambapo maeneo yote ya migodi yanalazimika kwanza kutenga bajeti na kusaidia miradi ya kuduma za jamii walioizunguka migodi kwa kuwajengea mashule, mahospitali na kuboresha mioundombinu na huduma za jamii za afya na elimu.

Pia sasa wanalazimika kutoa asilimia fulani ya mapato yake kwa halmashauri husika ili kuongeza mapato ya halmashauri kugharimia miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.

Hata wafanyakazi wakipunguzwa, miradi hii itaendelea. Athari za Kiuchumi kwa jamii hizo ni loss of income iliyokuwa contributed na uwepo wa watu hao katika eneo husika.
P
 
Kwahiyo ume declare kwamba uchumi unashuka, at the same time unasema uchumi unapanda msimamo wako upo wapi?
Mkuu Mwalimu wa Tuisheni, kuna aina mbili za uchumi. Macro Economics, ni uchumi mkubwa na Micro Economics, uchumi mdogo wa mtu mmoja mmoja.

Tanzania tunapaa Kiuchumi kwa uchumi mkubwa, uchumi wa viwanda, uchumi wa gesi na ukusanyaji wa mapato ndio maana tunanunua ndege kwa cash na kujenga miradi mikubwa kwa fedha za ndani, wakati uchumi mdogo wa mtu mmoja mmoja vyuma vinazidi kukaza.

Aliyesema uchumi unapanda sio mimi ni BOT, pato la taifa linaongezeka kila uchao, uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 7.2%. Rais Magufuli kazuia kusafirisha mchanga wa dhahabu, pato la dhahabu limeongezeka!. Hii maana yake huko nyuma tulikuwa tunaibiwa sana!.

Magufuli kapunguza wafanyakazi hewa, akawaondoa kazini wafanyakazi hewa, hajaajiri wafanyakazi wapya huu ni mwaka wa nne, huku serikali ikifanya kazi kwa ufanisi, hii maana yake civil service was over staffed, watu walikuwa wengi sana na wanakaa tuu hawafanyi kazi, sasa watu ni wachache wanapiga kazi kubwa na inaonekana!.

Tulikuwa na biashara nyingi, kufuatia Magufuli kubana mianya ya rushwa na ukwepaji kodi, biashara nyingi zimekufa, lakini TRA wanazidi kukusanya kodi kwa matrioni, hii maana yake kodi ilikuwa inakwepwa sana!.

Uchumi wa mtu mmoja mmoja unaporomoka, vyuma vimekaza huku uchumi wa taifa ukiimarika kwasababu wanaofaidika na kukua huko kwa uchumi ni sekta zenye watu wachache, sekta za ujenzi, fedha, mawasiliano, madini, na biashara zenye asilimia 23% ya Watanzania wote, asilimia 67% inategemea kilimo, hawa maisha yao wengi wao kila siku ni afadhali ya jana. Ndani ya makundi yote mawili sekta binafsi tupo na baadhi yetu tuna suffers!.

P
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom