Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Iga, Oct 22, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Oct 22, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi leo duniani kuna takriban nchi 231 duniani. Kiuchumi, Tanzania, Malawi, Gaza Strip, Sierra Leone, Somalia na East Timor ndio nchi sita hoibintaaban za mwisho ulimwenguni.

  Hadi kufikia sasa katika nchi yetu ilipofikia ni sawa Gaza Strip ya Wapalestina ilipo? Sisi , Gaza na Malawi wote tuna GDP per capita ya dola 600 za Kimarekani. Waliopo chini yetu ni nchi zilizoathirika sana na vita na misukosuko ya kijamii nazo ni Somalia, Sierra Leone na East Timor. Sierra Leone na East Timor baada ya mwaka huu, hata hivyo, lazima ziwe juu yetu kwa hiyo nchi itakayokuwa ya mwisho kabisa itakuwa ni Somalia ikifuatiwa na Tanzania. Tujiulize ni wapi tulipokosea, tunapokosea na tutakapoendelea kukosea? Ya kwamba pamoja na kugundulika utajiri mkubwa wa dhahabu na madini mengine hali ya Watanzania ndio imezidi kuwa mbaya kuliko ya watu wote duniani isipokuwa Somalia.


  Unataka ushahidi nenda hapa:

  World Facts and Figures - GDP per capita by country
   
 2. M

  Mbunge Senior Member

  #2
  Oct 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  INATISHA. Lakini li nchi lenyewe jingakubwa utafanyaje hadi liamke hili lidude kweli? Mimi nikizungumza na wenzangu naona kama vile hawanielewi.

  Angalia baadhi ya vijinshi eti kama Gaza ni kama 1 ya 10 ya mkoa wa Pwani sasa tusipogeuza mikoa yetu maeneo ya kiuchumi na kijamii inayojitegemea na kuingiza ushindani wa kiuchumi kati ya mkoa na mkoa hivi k weli tutafika?

  Sidhani. Jamani decentralization ije-mikoa iwe kama nchi ili itajirike na kuwaondoa wananchi wake kutoka kwenye lindi la umasikini wa kutia aibu duniani. Kisha delegation of authority toka kwa mzee ili Wakuu wa mikoa wawe magavana na wafanye vitu vyao kwa kudhibitiwa na serikali kuu.

  Aidha mawaziri wabaki wachache lakini wanaofanya kazi zinazoonekana na kuhitajika na sio k uibebesha jamii mzigo wa mawizara yote hayo lakini yanaharibu zaidi kazi badala ya kufanya mambo yawe nafuu na bora zaidi kwa walipa kodi na wananchi wote kwa ujumla!
   
 3. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  GDP kisiwe kipimo pekee cha kusema nchi gani ni tajiri zaidi duniani na nchi gani ni masikini wa kutupa.

  Watu wa development studies wana kitu wanaita INDICATORS OF DEVELOPMENT,ambayo ina vitu vingi ma hiyo GDP ikiwa ni kasehemu tu ambavyo kwa pamoja ndivyo vinapima uwezo wa kimaendeleo wa nchi tofauti.

  Kuna vitu kama huduma za kijamii kwa mfano shule,hospitali,zahanati,maji safi na salama,kuna walimu wangapi katika nchi,uwiano wa madaktari na wagonjwa,vitanda hospitalini nk
  Kuna vitu kama miundombinu,barabara,reli,,anga,simu,mzunguko wa pesa,upatikanaji wa ajira,nk nk

  Mambo yako mengi.Kwahiyo unaposema GDP pekee ndiyo kipimo cha maendeleo,si kweli.Inabidi uziangalie hizo indicators zote halafu ndiyo utupangie list ya matajiri na masikini.

  Halafu hiyo GDP yenyewe inatafutwaje?iko even?Nchi kama Luxembourg ina watu wasiozidi 500,000(laki tano),hiyo population ni kama mara sita ndiyo ifikie population ya watu wa jiji la Dar Es Salaam kwa mfano.Sawasawa na Rwanda na Burundi ambazo nazo zina idadi ndogo ya watu.
  Manake kanchi kenye watu wadogo kama Luxembourg,ni sawa na mkoa fulani wa Tanzania au mji fulani wa Marekani au nchi nyingine kubwa.ukikafanyia hiyo GDP ni sawa labda kwa mfano ufanye GDP kwa sehemu nyingine kwa uwiano huohuo.Kwamfano ukifanya GDP ya mkoa wa Dar Es Salaam,utapata nzuri sana zaidi ya hiyo 600.

  Kwahiyo point hapa ni hiyo uneven distribution of incomes in different parts of different populations in a big country like Tanzania.

  Ndiyo utaona bajeti ya ulinzi ya Marekani ni zaidi ya bajeti ya nchi tano za ulaya lakini kwenye GDP inashika nafasi ya 2/3/5

  Kwahiyo usidanganyike na hizo figure mkuu
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwavuli wa ubinafsishaji hautuacha kamwe! Ubinafsishaji na Uwekezaji. Tunabinafsisha hata ambavyo havina sababu ya kubinafsishwa. Tunawaalika hata watu kuwekeza kisichofaa. Mfano ni huyu aliyenunua kitalu cha uwindaji loliondo. Amewekeza nini pale? Hakuna chocote pale. Vijana wa kimasai wameambulia nini pale, zaidi ya aibu tupu. Hakuna sehemu yenye ufuska kama Loliondo kwenye hiki kitalu cha mtoto wa mfalme. Wanawake wanaletwa na ndege hadi Loliondo, wanatua pale, wanapokelewa na dereva wa waarabu ambaye naye nimwarabu,,, wanapelekwa kambini kwa hawa waarabu ,,, ni raha tu huko. Waswahili hawafaidiki na chochote hapa. na huko nyuma walikuwa wanatua na kuruka moja kwa moja bila hata kupitia mamlaka husika. Afadhali siku hizi wanapata kibali pale KIA.

  Shame!
   
 5. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  This is what Tanzanians are good at. Apologetics. Giving alot of words to justify unjustifiables! The fact is nchi yetu iko mkiani mwa mataifa ulimwenguni katika safu ya maendeleo. Upo? Hilo swala la GDP linasomeka darasani na naamini hata mleta hoja analijua hilo. Sasa inabidi tuchangie hoja kama ilivyoletwa. au UNDP na Worldbank wanatusingizia? Sisi sio masikini as they presume?

  Hivi statistics zingeonyesha kwamba tuko mbele kimaendeleo tungehoji vigezo walivyovitumia? Definetely..ukiguswa panapo lazima useme umeonewa. Tanzania tumechoka...inabidi tutafute mstakabali wa kujikomboa. Utashangaa kesho kutwa..Burundi, Rwanda, Congo ambao tumewahifadhia wakimbizi lukuki...wanatuwashia indicator ya maendeleo..na wasomi mtabaki oooohhh...hivi vigezo vya GDP vinapotosha...

  Tanzania nchi yetu kwa WANAOIJUA VYEMA, we are damn poor! Nenda vijijini ujionee. Tatizo watu mnafikiri Dar inaishia shoppers plaza na sleepway! Ohh..Yes my president said kwamba watanzania wa kanda ya kaskazini hatuli mapanki! Baada ya kuadress tatizo!

  Watanzania tumechoka sana! Duh!
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  nimeona ktk list kuna nchi inaitwa....... "World".............dah......iko wapi hii nchi....unajua tena wengine jiografia ilitupitia kando
   
 7. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,nimekupata.
  Hoja yangu siyo kuukana umasikini wa watanzania.Hoja ni kwamba kisitumike kigezo kimoja kidogo katika kuzipanga nchi kimaendeleo.Tanzania ni masikini,tena ni masikini wa kutupa lakini kwa hizi takwimu za GDP utaona kuwa nchi kama Liberia kwavile ina GDP kubwa kuliko Tanzania basi ina maendeleo kushinda Tanzania kwa mfano.Hili ndilo ninalopinga.
  Nadhani tuko pamoja sasa.
   
 8. M

  Mkora JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  CONVINCING EVIDENCE PLEASE HATUTAKI SIASA HAPA

  Mimi mwenyewe nimefika Luxembour kweli wapo wachache na nchi ndogo lakini wakazi wake woote ni matajiri sasa kuna kosa gani.

  kumbuka kadika hiyo GDP calculation wamejumuisha pesa za EPA ambazo zingeweza kupunguza makali ya umaskini nchini pamoja na kipato cha mamilioni ya watu Tanzania wanapata $1 kwa siku.

  Solution ni ku fix this problem no cheap un acceptable comment
   
 9. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Soma na uelewe mtu anachoandika,usikurupuke.
  Kufika kwako Luxembourg hakuongezi uhalali wa upangaji wa nchi tajiri na nchi masikini duniani kwa kigezo cha GDP pekee.
   
 10. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Swali kubwa ni kwa nini tuwe sisi na sio wengine .....wakati tuna mazingira mazuri zaidi ya kuweza kuendelea

  Kama ni population size Nigeria karibu 140 Millioni, Egypt 80millioni, South Africa zaidi ya 40 millioni ....etc

  Inawezekana kwenye mambo mengi tunayofanya kama nchi hakuna "efficiency", chukulia mfano wa bandari ya Dar es Salaam tu, kelele zimepigwa muda mrefu kuhusu ubovu wa utendaji kazi hapo bandarini matokeo yake ni kuwa wateja wanaamua kuhamishia shehena zao Msumbiji, Kenya, SA na Namibia. Athari zake ni kuwa mapato ya taifa yanapungua overall.

  Tukija kwenye kilimo, asilimia kubwa ya kilimo chetu ni 'subsistence' na tunalima mazao yale yale miaka nenda miaka rudi hatuangalii mazao gani mbadala yanaweza kulipa zaidi.
   
 11. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo ndiyo suala la kujadili katika thread hii.Tujadili kwanini sisi pamoja na maliasili zote tulizonazo,amani nk lakini bado tu masikini katika ujumla wake na siyo kutumia GDP pekee.Tujadili sababu za umasikini wetu,kwanini hatuendelei na siyo kupotosha eti kwavile Liberia ina GDP kubwa kuliko Tanzania basi Liberia ina maendeleo zaidi ya Tanzania au Tanzania ni masikini kushinda Uganda kwasababu Uganda ina GDP nzuri wakati ukifuatilia maisha ya mtanzania wa kawaida na myuganda wa kawaida(ambao ndiyo wengi katika nchi hizo) ni yaleyale isipokuwa wapo wachache(wengi wao ni wanasiasa mafisadi) wenye maisha mazuri.
  Sasa kama utayachambua maendeleo kwa kufuata vielelezo vyote vya maendeleo utaona nchi moja ina maendeleo katika vigezo kadhaa na inashindwa na nchi nyingine katika vigezo kadhaa.Kwahiyo unapotumia GDP pekee kusema nchi moja ni masikini kuliko nyingine unapotosha kwakuwa unakuwa unaviacha hivi vigezo vingine.
  Asante mkuu!
   
 12. M

  Mkora JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu kitu gani cha kuelewa wakati huitaji hata form four kwa hili solution tukubali our responsibility, jamaa amekupa data ambazo zimetoka Benki ya dunia sasa wewe unaeleta siasa ndio unabidi uelewe
  Luxembourg kuwa kuwa 500,000 sio tija mbona nchi nyingi zina watu wengi kuliko Tanzania na zipo juu yetu ndugu yangu hapo ni formula tuu
  sio kujifananisha na Bulldoza au embe dodo (kiongozi wenu Malecela)
  Au nawewe unaona Tanzania ni Dar es salaam Tuu that is too cheap thinking
   
 13. M

  Mkora JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu naomba utupe data tanzania inaweza kuwa juu kwa vigezo gani straight to the point?
   
 14. I

  Iga Senior Member

  #14
  Oct 22, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NINADHANI Watanzania wameshiba porojo, visingizio na sababu hii au ile ya kutoweza kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa.

  Simply, kwa sababu hii ni nchi ya wababaishaji. Kila mtu anajifanya anajua. Na kwa sababu kila mtu anajua ni sawa na wote hatujui.

  Nilipoanzisha mada hii nilidhania tutaichukulia kwa uzito wake. Hapa cha muhimu ni kujiuliza kwanini miaka karibu 50 baada ya uhuru nchi yetu iliyokuwa mkiani wakati wa uhuru hadi leo bado iko palepale mkoani.

  Wanaobisha wanakumbuka India, Malaysia, South Korea, Japan yenyewe, Singapore, Mauritius, Botswana na kadhalika zilikuwa wapi. Na sasa ziko wapi.

  Hii ina maana moja tu. Kwamba kuna kitu wanachokijua na walichokifanya ambacho sisi hatukijui na hatujakifanya. Ukichunguza viongozi wetu wengi wametoka kwenye umasikini mkubwa, iwe Nyerere mwenyewe, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na usiseme hao wa Zanzibar!!! Hawa kazi yao kwanza ilikuwa kujineemesha wenyewe, kisha familia zao na kisha ndugu, jamaa na marafiki zao. Sasa hatujui maana Kikwete sio masikini kiasi hicho kama na yeye atakwenda njia hiyo hiyo au atataka kwanza awatajirishe Watanzania kisha ndio ajifikirie yeye mwenyewe [kama atajitenga na wafadhili wake na maswahiba zake wakubwa walioichafua nchi kiasi ilichochafuka leo pamoja na kukwanya na Baba wa taifa kabla hajafariki!]. Hilo ni shauri lake. Akiachia na yeye zawadi ya Mo Ibrahim hata kwa Muumba hatakuwa na sababu ya kujietetea! Akumbuke Kurani takatifu inasema mke, mali na watoto [na marafiki-ongezo langu] ni MTIHANI mkubwa! Akipita huu tu kafaulu!

  Turejee kwenye pointi, ili tuendelee ni lazima tufanye mambo haya:
  . Kwanza tutambue kuwa kelele zetu za kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu hazijatusaidia kitu,
  . ujenzi wa viwanda umetushinda,
  . fedha na mitaji hatuna,
  . njia rahisi ya kupata fedha na mtaji ni biashara na sisi tunailegezea, wakati wenzetu Dubai wanapaa,
  . sekta nyingine ya kujilimbikizia ni huduma lakini serikali yenyewe legevu inaachia uchafu kila mahala na hakuna anayelalamika wala kujali. Tumeshazoea. Kampuni za usombaji taka ni chafu kuliko taka zenyewe!
  Usiseme kuhusu bustani na maua-utadhani Ikulu imepiga marufuku tusiwe na bustani na maua majumbani kwetu, maofisini na hasa sisi waswahili-angalau wageni na mabenki yao wanajitahidi,
  . tuna wizara kebekebe lakini zinakanyagana vidoleni na inaelekea mawaziri wakubwa kwa wadogo ukiwauliza wanalipwa mshahara kwa ajili gani watakuwa hawana majibu. Kinachotakiwa management by objectives, decentralization, delegation of authority na lean government. Hebu mmoja afanye analysis ya goverment expenditure compared to GDP utakuta seirkali yetu ina ratio kubwa kuliko hata serikali zenye uwezo! Kichaa tupu!
  . mama lao ni kwamba hakuna wizara yenye vision yake yenyewe, mission yake na strategic objectives au malengo ni wapi wanakotaka kuipeleka nchi na watu wake kufikia muda fulani. Vipo? Ninaomba iwe huu ni uzushi wangu. Nambieni basi wizara zina vision, mission na strategic objective jamanai? Katika karne hii , miaka hii ikiwa tunakwenda sawasawa na kina Mzee Malecela, Kawawa,Waryuba, Msuya na kadhalika tumekwisha!

  . Kubwa na baya zaidi ni kule watu wa CCM kujiona wao ndio wana akili kuliko Watanzania wote [siku hizi ninasikia tuko milioni 40 latest UN figure-2007] tukiwekwa pamoja. Hakuna njia ya mkato ya kuikwamisha nchi kimaendeleo kama ubaguzi wa kivyama. Yaani chama kimoja kubagua vyama vingine na watu wake na kuwapa hata wababaishaji na wajinga nafasi ya uongozi ingawa wanajua fika hao ni wajinga na kazi hiyo hawataiwezea. Mfano mzuri ni Zanzibar na hali iliyofikia sasa.

  Zanzibar yenye watu milioni 1 tu ina kila sababu ya kuwa na GDP per capita ya dola za Kimarekani tena 5,000 hadi 10,000. Lakini wameishia kuwa na gomvi za kuku na bata huku wakigharamia ng'ombe na ngamia eti kwa kuwa huyu ni CUF hafai, sasa wanakufa na vikoi vyao kiunoni na hakuna chochote kilichoviringishwa kwenye kunjo lake!

  KUJENGA UCHUMI pamoja na hayo yote pia kwahitaji kwanza kutoa elimu ya:
  -UCHUMI
  -MENEJIMENTI
  -BIASHARA
  -UHASIBU
  -RASILIMALI WATU

  kwa lugha ya Kiswahili. Pungufu ya hapo mwaka 2010 nchi duniani zitaongezeka na kufikia 250 na nina hakika Tanzania itakuwa ya 249! Poleni wanangu na wajukuu wangu! Mbona mnalo!
   
 15. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninukuu wapi niliposema Tanzania ni Dar Es Salaam tu
  Ndiyo mana nikasema usome na uelewe dhana nzima ya mtoa hoja,usichukue kipengere kimoja ambacho ni mfano tu na ukasema ndiyo hoja yenyewe
   
 16. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani hao benki ya dunia ni Mungu au biblia au msaafu wakisema kitu hakiwezi kuwa uongo au kubadilika?
   
 17. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hizi analysis nyingine!... Pengine ndio maana hatufiki.

  Sasa wewe ndugu yangu unaona kuwa population ndogo au land area ndogo(tena Arable land) ni disadvantage!... Hii mbona ndivyo sivyo. Watu na Ardhi ni rasilimali nyeti sana kwenye maendeleo. Jinsi gani unaziendeleza na kuzitumia hizo rasilimali ndio tatizo letu, lakini huwezi kuziita ni disadvantages when it comes to maendeleo. Hata hao China, sasa hivi wamarekani wenyewe wanawatamania soko lao la ndani la 1.3billion. Sembuse sisi 40million.

  Tuwe makini na utetezi wetu...
   
 18. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona kama unajichanganya vile?Unasema watanzania wameshiba porojo,wanatoa visingizio,wababaishaji,wanajifanya wajuaji,halafu unaelekea kukubaliana na hoja yangu kuwa GDP siyo kigezo pekee cha kupima utajiri na umasikini wa nchi,au?
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Yaani ni aibu tupu lakini Wakulu wetu hawaioni aibu hii maana wanaishi ulimwengu mwingine ndani ya Tanzania. 47 years of independence ati tunalinganishwa na Gaza Strip (Palestina), Sierra Leone, Somalia, na East Timor. Hizo nchi zikimaliza vita vyao watatupita na kusonga mbele yetu kimaendeleo. Hzi nchi ambazo tuko kundi moja zina maliasili gani kulinganisha na Tanzania? Hii ni Aibu kwa Watanzania na viongozi wetu;ingawa wao wana ka-nchi kao ndani ya Tanzania ambako sheria na makali ya maisha hayawagusi.


  Sasa Mtarajiwa, weka vigezo vyote hivyo ulivyosema na unavyovijua na uviorodheshe na kisha utuambie sisi tuko nafasi ya ngapi. Chukua kuanzia Rwanda kwenda mashariki hadi Kenya, na kushuka chini hadi Africa Kusini (Ondoa MAlawi iliyotajwa hapo). Je, kuna nchi gani yenye hali mbaya Kiuchumi, Miundombinu, na hayo ulosema kuliko Tanzania?
   
 20. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Niseme ukweli,
  Nikiwa nje ya Tanzania swala la GDP likitamkwa tu, furaha na amani moyoni vinatoweka. GDP GDP kwani wengine wamewezaje sie tushindwe? Why Tanzania? Kwanininiiiiiiiiii Tanzania? grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
Loading...