Tanzania's Foreign Policy

ewe membe,kwanini unakubali kutumwa na JK kutetea ufisadi wa BOT?
Ewe membe ulikuwa wapi kuzungumza zamani haya mathalani yameanza zaidi ya mwaka,
ewe membe mbona hautaki kusoma alama za nyakati?
ole wana wa watazania mafisadi,msidhani watanzania ni mbumbumbu
 
hatunyamazishwi ng'o! nasikia warioba alitoa ripoti ya hao mafisadi mwaka 1996 lakini mkakaa kimya sasa tumechoka, kila siku idadi ya mafisadi inaongezeka eg mkapa mwaka 96 hakuwepo kwenye list laliki sasa hivi yupo inamaana miaka ijayo list itakuwa na watu 111 je tutafika kwa hali hiyo? kwanini tukae kimya? Membe angalia kwenye list haumo ila ukiwatetea tutakuona mtu wa ajabu. Hakuna haja ya uchunguzi fisadi ni fisadi tu. Ona sasa mpaka Kapuya anamiliki mgodi wake mwenyewe huku watu hata ardhi ya kulima wananyang'anywa eti kupisha uwekezaji ambao wanafaidika wao, loh aibu gani hii?
 
Membe hawezi kuwajibu kwa nyodo watu ambao watusaidia 40% katika bajeti yetu, Yeye anafikiri wao wanafurahia uchafu wanaofanya na mawaziri wenzie?
Tushawachoka sasa akina Membe na wenzie.
 
Kwa sababu huyu mkuu rekodi yake kiuongozi ni safi, angetulia tu na kukaa kimya, hao mabalozi wakubwa wa dunia huwa hawahitaji kibali cha local government kuuliza yanayojiri,

Huyu hakuona waliyomfanyia Noriega na Saddam nini?
 

Leo mnakimbilia Ulaya kuitangaza TZ ili ipate kukamatwa zaidi ktk vitu ambavyo vinapatikana tanzania. Why hao wawekeshaji wasije jenga viwanda vya uzalishaji wa vitu ambavyo sisi hatuna i.e magari? Electonic parts na hata mazao yetu kuwa ktk finished product ndani ya nchi?

Hahaha sijui kama Mkandara unayakumbuka maandishi haya. They exist mzee. Keep it swinging mzee wangu
 
Jinsi habari hii ilivyo ripitiwa na HabariLEO:
Waziri alaumu mabalozi kwa kukiuka taratibu

Faraja Mgwabati
HabariLeo; Saturday,October 06, 2007 @00:02

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewalaumu baadhi ya mabalozi wa nchi za nje waliopo nchini kwa kuzungumzia masuala ya rushwa kwenye vyombo vya habari, kinyume cha masharti ya Mkataba wa Vienna, badala ya kuzungumza na Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kurejea kutoka ziara na Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani, Membe alisema inasikitisha kuona baadhi ya mabalozi hao wanasimama majukwaani na kuisukuma Serikali kutoa maelezo kuhusu masuala ya rushwa bila hata kuiuliza Serikali yenyewe. Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari asubuhi ofisini kwake, Waziri Membe, pia alikutana na mabalozi jana mchana kwenye Ukumbi wa Karimjee.

Aliwajulisha kuhusu hatua ambazo serikali inazichukua kuhusu tuhuma hizo na kuwataka mabalozi hao na wananchi kwa ujumla, kuwa na subira kwa kuwa uchunguzi unaweza kuchukua muda, lakini utakuwa ni wa uhakika. Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Membe alisema mabalozi hao wanakiuka kifungu namba 34 cha Mkataba wa Vienna unaomtaka balozi ye yote kwenye nchi fulani, kama ana tatizo lolote au haridhishwi na kitu awasiliane na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje.

“Sisi Balozi wetu hawezi hata siku moja kufanya hivyo… balozi wetu wa nchi za nje akifanya hivyo watamrudisha mara moja kwa sababu siyo sahihi kutumia majukwaa kwa balozi,” alisema Membe. Membe alisema anashangazwa na mabalozi hao ambao wanakuwa na wasiwasi na Serikali wakati marais wao juzi wameipongeza nchi kwa kupiga vita rushwa na wakaipa Tanzania fedha nyingi kupitia Mpango wa Akaunti ya Milenia ambao uko chini ya Serikali ya Marekani.

“Nashindwa kuwaelewa kama mambo wanayozungumza ni yao binafsi au wametumwa na nchi zao kwa sababu nchi zao zinatusifia, wao huku wanakuwa hawatuamini,” alisema Mwembe. Alisema serikali haiwezi kufanya mambo kwa kukurupuka kwa kutoa uamuzi ambao utawafurahisha mabalozi, lakini ukawaumiza watu wengine ambao hawahusiki na rushwa. Ndiyo maana suala la mgodi wa Buzwagi na Benki Kuu (BoT) linafanyiwa uchunguzi wa kina ili ukweli sahihi upatikane, alisema.

“It’s not fare (sio haki) kwa mabalozi hao kuilazimisha serikali kutoa maelezo wakati uchunguzi wa tuhuma za rushwa unaendelea,” alisema na kuongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inafanya uchunguzi.

“Nimezungumza na PCCB juzi na wameniambia kuwa tuhuma hizo za rushwa zinachunguzwa kwa umakini mkubwa na matokeo yake yatawekwa wazi kwa kila mtu na kama itabainika Membe anakula rushwa, basi atawajibishwa,” alisema.

Aliongeza: “Tusimlazimishe Rais kutoa uamuzi wakati uchunguzi unaendelea. Hii ni hatari anaweza ku-shoot (kupiga) hata vifaranga wasio na hatia,” alisema. Alitoa mfano kuwa wakati fulani baadhi ya jamaa zake walipomlazimisha kupiga ndege aina ya kanga wakati ndege huyo alikuwa ana vifaranga walipokwenda kuwinda kwenye shamba lake mkoani Lindi. Membe alisema katika matokeo ya uchunguzi wa PCCB kama kiongozi ye yote atapatikana na hatia, basi Rais Kikwete hawezi kumwonea haya, atamwajibisha kwa kuwa hakuna kiongozi mwenye ubia na serikali.

Alisema serikali imefanya mambo mengi katika kupambana na rushwa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha PCCB kwa kupeleka vijana nje kusomea jinsi ya kupambana na rushwa kitaalamu. “Hata Rais Bush (George W. wa Marekani) mwenyewe amemwambia Rais Kikwete juzi kwamba rushwa ipo kila nchi ila kinachotakiwa ni kufanya uchunguzi wa kina kwa tuhuma zinazotolewa dhidi ya serikali,” alisema.

Alisema matunda ya juhudi hizo yameanza kuonekana kwa Tanzania kushika nafasi ya 94 mwaka huu duniani kutoka 124 mwaka juzi katika kupambana na rushwa kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Kimataifa la kupambana na rushwa la Transparency International. Akiwa na mabalozi baadaye jana, Membe alisema: “Lazima uchunguzi ufanywe kwa makini ili hata mtuhumiwa naye apate haki ya kujitetea na aweze kusafisha jina lake na huu ndiyo utaratibu unaotumika duniani kote.”

Mabalozi walikuwa wakimsikiliza kwa makini. Baada ya maelezo hayo, Membe alikaribisha maswali na wengi wa mabalozi walinyamaza kimya kuonyesha kuridhika na maelezo hayo. Balozi wa Uingereza nchini, Philip Parham alisimama na kuelezea kufurahishwa na maelezo yaliyotolewa na Waziri Membe.

Katika mkutano huo na mabalozi, Membe pia alizungumzia masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika ziara yake na Rais Marekani, likiwamo la Zimbabwe. Katika suala la Zimbabwe, Membe aliitaka Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo kwa nchi hiyo ili wananchi wake wasiendelee kuteseka.

Pia alisema SADC inaamini kuwa kujitoa kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya unaotarajia kufanyika mwezi ujao Ureno, kama Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe atahudhuria siyo suluhisho la matatizo ya Zimbabwe.

Wiki chache zilizopita, Brown alitangaza kuwa hatahudhuria mkutano huo kama Rais Mugabe atahudhuria. Hata hivyo, akijibu hoja hiyo, Balozi Parham alisema kama Brown hatahudhuria kwenye mkutano huo haina maana Uingereza haitawakilishwa na pia kama Mugabe hatakwenda kwenye mkutano huo, nchi itawakilishwa na maofisa wengine wa nchi hiyo.

Source link: HabariLEO.

SteveD.
 
Nashindwa kuwaelewa kama mambo wanayozungumza ni yao binafsi au wametumwa na nchi zao kwa sababu nchi zao zinatusifia, wao huku wanakuwa hawatuamini," alisema Mwembe. Alisema serikali haiwezi kufanya mambo kwa kukurupuka kwa kutoa uamuzi ambao utawafurahisha mabalozi, lakini ukawaumiza watu wengine ambao hawahusiki na rushwa. Ndiyo maana suala la mgodi wa Buzwagi na Benki Kuu (BoT) linafanyiwa uchunguzi wa kina ili ukweli sahihi upatikane, alisema.

Haya jamani, wengine wanatembea nchi nzima wakisema WAPINZANI NI WAONGO, huku Zitto kafungiwa kwa kusema uongo, sasa huyu Membe katumwa na JK anasema wanachunguza!!!!!!!!!!!!!!!!, NASIKIA KUZUNGUZUNGU
 
“Sisi Balozi wetu hawezi hata siku moja kufanya hivyo… balozi wetu wa nchi za nje akifanya hivyo watamrudisha mara moja kwa sababu siyo sahihi kutumia majukwaa kwa balozi,” alisema Membe.
Balozi wetu huko majuu, atasema nini wakati huko watu hufuata sheria? Wewe umesikia leo mkimbiaji maarufu Marion Jones, amefikishwa mahakamani kwa makosa aliyotuhumiwa toka mwaka 2000, leo ni 2007 ametinga kwenye mkono wa sheria na maekubali kuwa na makosa, pamoja na umaarufu wake wote, sasa balozi wetu huko atawasema kitu gani?

Hivi ni kitu gani anafikiri ana-accomplish kwa kuwadanganya hao mabalozi? Kwani wao wajinga hawaijui bongo? Hilo gazeti limeandikwa na nani? Hiyo kampeni wanayoitumia kupoteza hela zao kama sio zetu walipa kodi, kwa nini wasizitumie kuanzisha kesi mahakamani ili mzizi wa fitina ukatwe? Kesi ikienda mahakamani Membe hatakuwa na shida ya kumuelezea balozi yoyote, wala mawaziri kwenda mikoani, kwa nini wanapoteza muda wa watu bure na hadithi za Abunuwasi, wakati wananchi tunao mkataba wa Buzwagi tayari?

Je huu mkataba usinge-leak ingekuwaje, tungeyasikia haya? Wapunguze hadithi sasa ni wakati wa kazi na matendo, waache hadithi!
 
FROM WHAT HAS BECOME THE NORM OF RESPONSE FROM THE GOVERNMENT RECENTLY, I'M INCLINED TO SAY COLLECTIVE STUPITIDY IS AT WORK, AND THAT'S PRECISELY WHAT THEY ARE UNVEILING BY TRYING TO BE CRITICAL ABOUT BUZWAGI CRITICS!! FOR WE KNOW, THE WISDOM OF CROWDS AND THE ANTICIPATIVE COLLECTIVE INTELLIGENCE IS OUT OF THE DOOR ON THEIR PART!!

SteveD.
 
1. Hivi wewe membe si ndiye ulikiuka maadili ya UWT na kufichua uovu wa Bosi wako Kitine, kwani huko UWT hakuna taratibu za kutiana adabu mpaka ukamuumbua bosi wako?.........hivi unajua heshima uliyojijengea kwa lile jambo?

2. sawa Geneva Convetion inawabana, however FACT inabaki kuwa FACT irregardles of whichever convetion...........hata Convention ikitoka mwezini haiwezi kuondoa FACTS walizosema, atleast wameweza kuuliza kile ambacho KODI za wananchi wao zinatumika/zinatarajia kutumika directly or indirectly.........Trust me Membe hawa wote waliotoa matamko wanakuwa supported na nchi zao.........usifikiri wamekurupuka tu.

3.Membe wewe ni mwanadiplomasia mahiri na.............i mean heshima mbele, twende mbele turudi nyuma vile vile, hivi hawa mabalozi waliongelea hayo masuala wakiwa wapiiii?...............who were the audience.......na mada ilikuwa nini?.........
 
Mods jamani tunaomba mu merge threads zinazofanana fanana

kama mko sharo kuhamisha threads kwa nini mko slow kumerge threads mkiombwa?
 
TANZANIA HAS GOT 2 FOREIGN POLICIES......!
\ (TRADITIONAL FOREIGN POLICY president's circular no 2 of 1964 & NEW FOREIGN POLICY 2001)
 
Kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake na nadhani nyote mliotoa hakuna aliekosea isipokuwa tunazungumzia kitu kimoja katika perceptions tofauti. It is all part of the jigswa puzzle:

1. Kunapokuwa na habari mbaya katika image ya nchi ni jukumu la ubalozi, wizara ya mambo ya nje na hata idara nyingine mbali mbali kujaribu kubadili hilo, njia zipo nyingi na kazi kubwa ya ubalozi ni ku-redress the negative image. Hivi ndio vipimo vinavyotumika kuangalia effectiveness ya balozi husika, in fact who knows kwa kuweka ukweli bayana unaweza vutia watalii na wawekezaji....precisely Membe's point!!

2. Ziara za muungwana ni ku-capitalise jitihada za balozi, hivi jamani mnadhani Mheshimiwa Rais ataibuka tu aende ziarani, it all begins with proper co-ordination ya ubalozi, idara za itifaki, ikulu na respective departments on the host governments, akiondoka rais wanaofuatia ndio wanacapitalize on the promises, pledges nk....Wawekezaji wakisikia from the horses mouth na ubalozi ukiwa effective kufuatilia ndio matunda yanaokana... UbAlozi mzuri ndio utafuatilia vizuri...Precisely Membe's point ''Tutawapima kwa kuleta wawekezaji''

3. '' Tengeza nyumba wapangaji watakuja tu'' sounds nice Mkandara lakini I am afraid though it is a true statement but incomplete, wakati mwingine you need wapangaji ili uweze kujikwamua upate fedha ndio ukarabati, they need to go hand in hand... Tuna uwezekano wa kupata mafuta as dalili zipo, uwezo wa ku-explore hatuna hivi tusiombe misaada nje kuwaalika wawekezaji kwa vile bara bara ni mbovu? Tuna gesi nyingi sana, utaalam wa kui-convert into usable energy hatuna hivi tusitangaze tender ya kampuni za kigeni kuja kuredress this kwa vile kuna matatizo ya umeme?! Waziri akisema mabalozi watapimwa kwa kuvutia wawekezaji kuna kosa gani? Kukarabati nyumba YES mkandara lakini wapangaji tunawahitaji as well...


For the record, Sera yetu katika foreign Affairs ni ECONOMIC DIPLOMACY, diplomasia inayosupport uchumi, Waziri akisema kipimo cha uchapaji kazi wa balozi zetu kitakuwa ni how effective the mission has been in implementing this, I think it's a commendable statement which comes from a higher authority.... Kumlaumu kwa kusema hivyo ni sawa na kumlaumu waziri wa Usalama wa Raia kwa kuwaambia Polisi kuwa kipimo cha utendaji wao wa kazi ni namna watakavyokuwa wamesaidia kupunguza uhalifu....


Mkuu Kulikoni,

With all due respect hoja yako ya kwanza na hii I 'm sorry that I will have to disagree with you completely.

Katika hoja zako mbili unagusia economic diplomacy!, ni ipi hio.

Tanzania tokea ipate uhuru hadi leo inategemea pesa ya wafadhili kuendesha shughuli zake na hata bajeti hisimamiwa na wafadhili hao.

Nafikiri umesoma kitu kinaitwa interenational relations theory, ni conceptual model gani imebuniwa na wizara au mawaziri tokea uhuru kuiweka Tanzania katika duru la nchi zilizoendelea au basi kupiga hatua fulani?

Pia umetaja masuala ya watalii lakini hawa watalii huletwa Tanzania na mawakala ambao wapo nje kwa mfano UK ambao huwalipisha fedha nyingi hadi kufikia paundi 2000 kwa wiki mbili tu wakiwa Tanzania.

Mimi naona hujaeleza kwa ufasaha hasa foreign policy ya Tanzania imesimama vipi, vinginevyo naona unakuwa kama unatoa blanket statements tu.
 
my meseji to MOFA.......! wekeni mtandaoni TZ NEW FOREIGN POLICY(2001)
ili watu/wananchi wajue sera ya nje ya nchi yao....! hope nimeeleweka>>>>!
 
mtandaoni utakuta sera za mifugo, maji, viwanda n.k lakini sera ya mambo ya nje haimo...!
 
my meseji to MOFA.......! wekeni mtandaoni TZ NEW FOREIGN POLICY(2001)
ili watu/wananchi wajue sera ya nje ya nchi yao....! hope nimeeleweka>>>>!

Mkuu,

Lakini hii si naona itakuwa updated au ..!

Maana leo ni 2008
 
Back
Top Bottom