Tanzanians to pay much more for power

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Tanzanians to pay much more for power
By A STAFF WRITER
THE EAST AFRICAN

Tanzania may have to implement another electricity tariff increase later this year to enable power utility, Tanesco, to operate profitably.

Although a substantial 21.7 per cent tariff increase was effected on February 1, 2008, this has been found to fall short of the cost recovery level that was requested by Tanesco.

The upshot is that the state controlled utility will continue to experience operational cash shortfalls, which could reach Tsh50 billion ($28.5 million) in 2008.

The details are contained in minutes of discussions between the government and a mission of the International Monetary Fund that visited the country in March this year.

While it is not anticipated that Tanesco will need subsidies in the current financial year, the government has recommended that the power utility considers cost-cutting measures.

Tanzania must get Tanesco to financial viability if the country is to enjoy a reliable electricity supply.

Last year, Tanesco had applied to electricity industry regulator, EWURA, for a 40 per cent power tariff increase.

It is understood that EWURA has agreed to consider another request for a tariff increase once Tanesco completes a cost of service study and takes measures to reduce non technical losses — notably theft of electricity.

Tanesco is currently reviewing its financial situation in view of EWURA’s ruling.

In the meantime, the power utility is using the private emergency power generators to meet intermittent power supply deficits.
Currently, the company is in the process of procuring its own 145MW gas-fired generation capacity.

Despite good rains, the financial situation of Tanesco remains vulnerable, partly because of failure to implement cost reducing measures in its financial recovery plan, including the buy out of IPTL, the conversion of its plant and the refinancing of the Songas expansion. Negotiations with IPTL’s main creditors are currently under way.

Tanzania’s energy budget has increased steadily in recent years mainly as a result of the emergency power projects, consisting mainly of leased and owned generators funded through the multilateral debt relief initiative from the IMF.

Although the economy has remained strong — averaging 7 per cent during 2001-2007, thereby outpacing the average for sub-Saharan Africa, intrinsic weaknesses have began to emerge lately.

Government expenditure has bloated significantly, financed mainly by a significant broadening of the revenue base and scaled up donor assistance.

This year’s budget was written against the background of uncertainties in donor financing. Consequently, the government may this year be forced to borrow more from the domestic market to substitute foreign financing.

The circumstances may force the government to introduce expenditure cuts to cushion the budget from the impact of temporary financing uncertainty.

Secondly, inflation has increased in recent months, mainly reflecting rising global food and fuel prices.

There are also risks that inflationary pressures could spread in an environment of rapid credit expansion.

Still, Tanzania’s performance ranks among the best for non-oil exporting countries in sub-Saharan Africa.
 
...jamani kinachotumaliza ni hii monopoly waliyopewa TANESCO,nafikiri watetezi wa hizi policy za umeme za sasa wanataka mpaka nchi nzima ifirisike ndio wabadilike,TANESCO inaua uchumi wa nchi nzima na ukweli hawana uwezo wa kuzalisha na kusambaza umeme its time watu binafsi waachie wafanye kazi kama makampuni ya simu yalivyoruhusiwa...faida za uhuru ni nini sasa? ni aibu kubwa na ujinga kwa wabunge wote wanaopinga kuruhusu watu binafsi kuwekeza kwenye umeme...monopoly is a killer!
 
Una maoni gani kuhusiana na mikataba kama ya IPTL, Net Group Problems, Richmond, Kiwira n.k. ambayo imesababisha TANESCO kushindwa kujiendesha kibiashara? Ukumbuke pia kwamba mikataba yote hii wataalamu wa TANESCO waliikataa lakini wakalazimishwa na 'viongozi' waikubali.

Katika nchi za wenzetu pamoja na kupiga kelele nyingi kupinga monopoly bado mashirika nyeti kama ya kusambaza umeme bado yako chini ya halmashauri za miji, states au provinces na siyo mikononi mwa watu binafsi. Unakumbuka lile scandal la ENRON? wale walikuwa ni watu binafsi na wanasambaza umeme basi wakaanza kufanya mambo ya ajabu ajabu ili kuwalangua watumiaji umeme, ilikuwa ni scandal kubwa sana. Hilo shirika lilishakufa. Matatizo mengi ya TANESCO, kwa maoni yangu yanasababishwa na viongozi, kuna matatizo ya ndani TANESCO lakini sidhani kama yanaongeza bei ya umeme kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na hii mikataba bomu.
 
Wengine sasa mtataka hata JWTZ tulibinaifishe. POLISI nayo ifuate na ikibidi hata IKULU na Bunge liendeshwe na watu binafsi. Jamani tutabinaifisha hata WAKE ZETU na watoto. Hawa Mafisadi kama wangeliweza kufanya hivyo basi wangelifuata hata wake za watu na watoto wao na Punda wao na .....
Hakuna upuuzi duniani kama kufanya hivyo. TANESCO imeliwa wee na sasa mzigo wanaubeba Wananchi. Heri itangazwe moja kwa moja kuwa TANESCO is there to stay na hakuna KENGE yoyote kuja kuleta KALUFUDI kake. Hutu tulufundi kama RICHMOND na kaka zake (utafikiri Babu Seya Family ya UMEME) walioufanya ndiyo umetufikisha hapa tulipo. Kwanza wavunje mikataba na kudai chetu na hapo waangalie uwezekano wa kuliendesha upya kwa ufanisi na hawa jamaa WAJITUME. Tanzania tunavyoTANUA kwa zamu sisi, laiti tungelichakalika hivyo hivyo, hata OMBA OMBA wetu wangelikuwa BOMBA.
 
Mkataba Mmoja wa Richmond wa 100MW kwa $172million, hizo pesa zingeweza kununua mitambo 5 ya 100MW=500MW, hivyo Tanzania kusingekuwa na Tatizo la umeme kabisa. Kwa Sasa Tanzania tunatumia 600MW, kama mikataba yote ikifutwa Tanesco, itaweza kusambaza Umeme hadi vijijini. Juzi juzi nilikuwa Venezuela, the President, Mr Chaves, kasambaza Umeme wa MW 1.5 ambao unatoa Ememe pamoja na Maji safi ( Steam turbine) kwa kila vijiji gharama ya steam turbine moja ni $0.9 million. Tanzania hiyo inawezekana , kwani tuna Gesi nyingi ambayo ingetumika vizuri basi umeme ungekuwa wa kumwaga na kuuza nje ya nchi. Pia kama Tanzania wangeamua kununua Mitambo kama hiyo tungekuwa naya 175 hivyo kila kona ya kijiji, kata, tarafa, wilaya mkoa kungekuwa na Umeme wa kumwaga pamoja na maji safi.
 
I proposed last year to fire Tanesco CEO, Dr. Rashid. The guy proves that he knows nothing about management. Tanesco inashindwa kujiongoza sababu ya cost, nilikuwa na expect Dr. Rashid atafute njia mbadala za kureduce cost on each sector ndani ya Tenesco. Kwanza kabisa ni reavaluate the whole Value chain and see if there is a need of revamping it. kisha ni kuangalia what part of value chain has cost bleeding problem? Sehemu ya kwanza inayo imaliza Tanesco ni labor cost na backward vertical intergration (kumiliki part za supply chain ambazo Tenesco sio expart wa hizo sector). Kuna mengi ya kutazama lakini hayo ni kwa big picture.

Hakuna organization dunia inayofanikiwa in a long run kwa kuhike up price bila kukocontrol cost. Nilikuwa nategemea watatengeza strategy itakayo ipa Tanesco cost efficient advantage. Wanachojali wao ni kuongeza bei per unit.

Serikali inabidi iondoe ushuru kwenye altenative energy, ili Watanzania tuliona abdonomal profit kwenye energy sector tuipeleke Tenesco kwenye coma kabisa. Nadhani tunaitaji more of sloar energy, wind energy na n.k. Haya yanaweza kuiamsha Tanesco wakafahamu kwamba muda wa free lunch umekwisha.
 
...kina Rashid hawajui chochote na doctorate zao na hata BOT ilimshinda,yaani i cant wait the day tanesco itakapokufa kabisa na kutoweka maana ni mwiba kwa maendeleo ya nchi na still bado wanajaza mitambo ya madiesel machafu kuendesha mitambo yao yaani wanaotetea hili shirika sijui lipewe pesa zaidi na serikali sijui wanafikiria nini?na hiyo alternative energy naona hawajaamka kabisa na hawana idea...tuna wind kibao na jua mwaka mzima all over the country lakini sioni strategy yeyote ya kufika huko,inatia uchungu sana kuwa na viongozi waliokosa vision kama hawa,na wanaolazimisha monopoly ya Tanesco wajue miaka 50 ya hawa jamaa peke yao TZ wameturudisha miaka 100 nyuma....acheni watu wazalishe,wasambaze na wauze umeme sio kuwapa hiyo haki Tanesco peke yake,competition ni muhimu sana and will avoid hawa wajinga kutupangia bei ya umeme maana supply & demand itafanya kazi yake naturally,Tanesco haiwezi survive kwa kupandisha bei za umeme kila siku na ikiendelea hivi tujiandae kwa major crisis ambayo ita bring down kila kitu.
 
Mkataba Mmoja wa Richmond wa 100MW kwa $172million, hizo pesa zingeweza kununua mitambo 5 ya 100MW=500MW, hivyo Tanzania kusingekuwa na Tatizo la umeme kabisa. Kwa Sasa Tanzania tunatumia 600MW, kama mikataba yote ikifutwa Tanesco, itaweza kusambaza Umeme hadi vijijini. Juzi juzi nilikuwa Venezuela, the President, Mr Chaves, kasambaza Umeme wa MW 1.5 ambao unatoa Ememe pamoja na Maji safi ( Steam turbine) kwa kila vijiji gharama ya steam turbine moja ni $0.9 million. Tanzania hiyo inawezekana , kwani tuna Gesi nyingi ambayo ingetumika vizuri basi umeme ungekuwa wa kumwaga na kuuza nje ya nchi. Pia kama Tanzania wangeamua kununua Mitambo kama hiyo tungekuwa naya 175 hivyo kila kona ya kijiji, kata, tarafa, wilaya mkoa kungekuwa na Umeme wa kumwaga pamoja na maji safi.

...mkuu inatia uchungu sana maana hata mtoto mdogo yeyote anaweza kujua bei halali ya mtambo mpya wa kutumia GAS wa 100MW just kwa kupiga simu tuu,lakini walichotufanya hawa mafisadi God knows,yaani ni aibu kubwa sana kwa hawa kina Richmond walichofanya na cha ajabu hakuna hata mmoja ambaye yuko jela au kesi inaendelea,tunawatetea monopoly ya Tanesco na kulalamika bei mbaya ya umeme huku ukweli tunajua mtambo wa 50m wamenunua bei mara tatu tena used,halafu cha ajabu tunawapa excuse eti wakubwa wa serikali ndio walilazimisha kwa hiyo mgt haihusiki na mbona hatukuwahi kusikia protest yeyote au kujiuzuru kwa kuingiliwa kazi...uwongo kwa kwenda mbele wote hawa must go kuokoa sector ya umeme.
 
Wengine sasa mtataka hata JWTZ tulibinaifishe. POLISI nayo ifuate na ikibidi hata IKULU na Bunge liendeshwe na watu binafsi. Jamani tutabinaifisha hata WAKE ZETU na watoto. Hawa Mafisadi kama wangeliweza kufanya hivyo basi wangelifuata hata wake za watu na watoto wao na Punda wao na .....
Hakuna upuuzi duniani kama kufanya hivyo. TANESCO imeliwa wee na sasa mzigo wanaubeba Wananchi. Heri itangazwe moja kwa moja kuwa TANESCO is there to stay na hakuna KENGE yoyote kuja kuleta KALUFUDI kake. Hutu tulufundi kama RICHMOND na kaka zake (utafikiri Babu Seya Family ya UMEME) walioufanya ndiyo umetufikisha hapa tulipo. Kwanza wavunje mikataba na kudai chetu na hapo waangalie uwezekano wa kuliendesha upya kwa ufanisi na hawa jamaa WAJITUME. Tanzania tunavyoTANUA kwa zamu sisi, laiti tungelichakalika hivyo hivyo, hata OMBA OMBA wetu wangelikuwa BOMBA.

....endelea kuwatetea hao mafisadi huku anayeumia ni wewe mwenyewe,akili yako inakutuma kwa kuendelea kukumbatia Tanesco basi ndio tutakomesha mafisadi na bei ya umeme itapungua...una mengi ya kujifunza kujua unachoongea hapo.
 
Misleading thread title. What is the actual direct cost incurred by the average non commercial consumer? What is the approximate indirect cost forgone as a result of rationing and other power mishaps? Until one gets these figures it is highly inadvisable to even consider such a conclusion that Tanzanians pay over the odds for their electricity.

Then again I am just playing the devil's advocate here BUT it will be helpful if someone could break down the costs associated with power in Tanzania.
 
Jamani Tanesco imekuwa Paralyzed na serikali yenyewe. Kuwabebesha lawama huku tukiiacha serikali inapeta ni kujifanya hatujui tatizo na kamwe hatutaweza ku solve tatizo.
Ni kweli kuna shida ipo katika management ya Tanesco lakini si kwa extent ambyo ingelifanya shirika liwe hoi hivyo.
Hata hivyo nakubaliana na wazo la watu binafsi kujiusisha na utoaji huduma za umeme, lakini kwa experince niliyonayo hii haiwezi kusolve tatizo la bei.
Hii nimeiona upande wa simu ambako tulidhani kwamba kwa kuwa na makampuni mengi tungepata unafuu wa bei. Lakini hawa wafanya biashara wako smart maana wanashirikiana hata katika mambo ya bei na as a result bei zimebaki juu sana na wala hakuna maana yoyote.
Hata hivyo ukweli unabaki pale pale kwamba hata serikali ikijitahidi kujivua katika hudma za wananchi haiwezi kujivua kwa haya yafuatayo: Maji. umeme, elimu, afya na mawasiliano.
Siku ikijivua kwa hayo kama ambavyo inajaribu kufanya tujue kiyama cha maendeleo yetu kimefika.
 
....endelea kuwatetea hao mafisadi huku anayeumia ni wewe mwenyewe,akili yako inakutuma kwa kuendelea kukumbatia Tanesco basi ndio tutakomesha mafisadi na bei ya umeme itapungua...una mengi ya kujifunza kujua unachoongea hapo.
__________________
"Fools argue, wise men discuss and sages listen" -- Lao Tse

Koba,
Napenda sahihi yako. Ila nashindwa kuelewa Mahusiano yako ya kuifanya TANESCO ni shirika pekee la Taifa bila ya kuleta UJINGA wowote kama RICHMOND au IPTL. Watafutwe Viongozi wazuri na wasiingiliwe maamuzi yao. Haya mambo ya kuiingilia mashirika ndiko kumetupeleka PABAYA.
Uwezo wangu wa kuelewa Namshukuru MUNGU kuwa Si MBAYA. Kinachofanyika siku zote ni hiki. Mafisadi wanaangalia shirika gani wanataka liwe leo. Wanachagua kiongozi Mzuri mwenye uwezo wa kuuwa shirika(ATC). Anakwenda na kuliuwa hilo shirika na baadaye wanakuja na kusema "ili tatizo liishe inabidi kubinaifisha hili shirika na kuleta ya watu binafsi.." Hili ndilo unataka wewe. Sasa kati yangu na wewe nani anakumbatia UFISADI? Au kati yangu mie na wewe nani anamuono wa mbali?
Lowassa alijua kuwa UKAME utakuja Tanzania. Hawakufanya kitu chochote mapema ili saa ikifika waje waunde RICHMOND. Hizi danganya toto na upuuzi mwingine tumeshaujuwa. Balozi mmoja hapo Dar aliwasha Generator la umeme na mwisho kulaani vikali kwa kusema "Miaka 40 mko huru na hamjajenga RELIABLE ENERGY SOURCES?..."
 
...IPTL na Richmond ni matokeo ya sera za umeme zilizopo na ndipo mafisadi wanatumia kula hapo,nakuhakikishia bila kubadili policy za umeme za sasa na kuruhusu competition kwenye hii sector umeme utaendelea kuwa bei mbaya,halafu naomba unielewe ninapoongea privatization sina maana lazima TANESCO lazima iuzwe inaweza kuendelea kuwa ya Taifa lakini lazima waruhusu wengine nao wafanye biashara kama TANESCO(nafikiri unajua kwa sasa mtu binafsi hawezi) .....mkuu bei itashuka tuu supply ikizidi demand na si vinginevyo(basic Econ)
 
uchambuzi makini mdau. tatizo la tanesco ni mgt tuuuuuuuu. kama mikataba mibovu inaingizwa pale kwa nini uongozi ukubali.ok, watajitetea political push. uendeshaji wa tanesco haundeani na mazingira ya soko. WHY? poor planning and organization structure.
hawawezi kufanya generation, transmission na distribution wenyewe ni upuuzi. hilo shirika ni mzigo kwa serikali lifumuliwe lijiendeshe kibishara na kwa faida. wako watu pale very unnecessary wanaongeza overhead costs na ufanisi sifuri.
tanesco ifumuliwe mapema iwe market driven, professionalism and profit making firm.
blah blah tuweke kando. serikali iwe na utaratibu wa kussuport disadvantageous population kupata umeme kwa bei nzuri through funding.
 
Tanesco is working very hard to find alternative source of power i.e

GAS from (1) Songo songo under Songas (2) Mnazi bay under Arthumas (3) Potentional Gas Reserves have been sighted at Mkuranga which are yet to be exploited. Independent power operators are already in place at (1) and (2) (i.e Songas and Arthumas)

COAL : Coal reserves have been identified at (1) Kiwira and Mchuchuma. Kiwira Mine is owned by Tanzanians (by majority share), KCP are known to have sourced their plants from China. On full operation KCP is expected to inject in the national grid an additional 200-230kwatts. As for Mchuchuma no competitive operator has been found as yet. Therefore this source is still open for a performant proposal.

HYDRO POWER: Ruhuji / Lumakali with potential of generating 200-240kW is in the government power master plan. Exploitation of same remains plunged by lack of funds

They are also trying the possibility of Gas turbines source of power producing 250wts capacity formally owned by EDF (France)

Maybe this will reduce all the dependency on what they have currently and even reduce power tariffs
 
hawawezi kufanya generation, transmission na distribution wenyewe ni upuuzi.

Nyauba,
Wewe ni nduguye LOWASSA? Hebu soma hapa chini na zaidi nimeandika hapo juu. SI kweli kwamba UTAWALA wa Tanesco una nguvu ya kuamua. Wamekuwa wakiingiliwa sana na serikali. Ni mwaka huu tuliona mvutano kati ya CEO wa Tanesco na yule Balozi m/k wa bodi. Mmoja akisema kiwanda cha sementi kirudishiwe umeme na CEO akisema KATA UMEME. Kilichotokea ni kiwanda kurudishiwa umeme. Ni kwa kitisho cha CEO kuachia ngazi ndicho kilisaidia kiwanda kulipa billi. Hapo ni kuwa CEO hakuwa mtu wao. Angelikuwa mtu wao kila kitu kingeliishia chini chini.
Nchi kama inchi inabidi kuwa na sheria na hizi zifuatwe. Mkapa hili neno SHERIA aliliuwa na matokeo yake ni haya. Sasa hata ufanyeje, utakuwa unajenga UKUTA na PAA zuri saaana na IMARA ila tu MSINGI wako MBOVU.
 
Tanesco is working very hard to find alternative source of power i.e

GAS from (1) Songo songo under Songas (2) Mnazi bay under Arthumas (3) Potentional Gas Reserves have been sighted at Mkuranga which are yet to be exploited. Independent power operators are already in place at (1) and (2) (i.e Songas and Arthumas)

COAL : Coal reserves have been identified at (1) Kiwira and Mchuchuma. Kiwira Mine is owned by Tanzanians (by majority share), KCP are known to have sourced their plants from China. On full operation KCP is expected to inject in the national grid an additional 200-230kwatts. As for Mchuchuma no competitive operator has been found as yet. Therefore this source is still open for a performant proposal.

HYDRO POWER: Ruhuji / Lumakali with potential of generating 200-240kW is in the government power master plan. Exploitation of same remains plunged by lack of funds

They are also trying the possibility of Gas turbines source of power producing 250wts capacity formally owned by EDF (France)

Maybe this will reduce all the dependency on what they have currently and even reduce power tariffs

Naima,
Haya yote ya juu ni mazuri saana kuandika na kuwaambiwa WASOMI ila mtu wa kawaida hapa Sikonge hataelewa unaongelea nini. Pili hii kitu inategemea sheria za nchi na VIONGOZI MAFISADI watakuwa na uwezo wa kiasi gani kuingilia utendaji wa TANESCO. Ndiyo maana nikasema ni heri TANESCO iwe kama TANROAD. Lijitegemee na kuendeshwa kwa WALAU BILA FAIDA WA HASARA. Viongozi kama ilivyo TANROAD waambwe kabisa " ... ehhh, nyie VIBAKA, mikono mbali na TANESCO..". Amini usiamini, umeme utakuwepowa kutosha na bei si kubwa. HAta wafanyakazi wenyewe wa TANESCO sidhani kama wanafurahia tatizo la umeme. SI nao wanaishi TAnzania na si TANESCO? Hata hivyo INAFURAHISHA kuona jamaa wanachakalika kutafuta UMEME WA UHAKIKA WA TAIFA. Kama na wewe ni mmoja wao basi niseme KILA LA KHERI.
Je, kuna mpango wa kuzalisha umeme kwa UPEPO? Nafikiri Kanda ya kati na Ufukoni mwa Bahari kuna faa sana kuweka haya ma-PANGA BOY kwani kuna upepo mkubwa tu (Zanzibar pia kama sikosei). Hebu anzeni kufikiria kwa hili pia na hapa huhitaji kitu zaidi ya kufanya marekebisho na kusubiri tu upepo uanze kazi na wenyewe huwa upo karibu kila siku.
 
Mimi si mmoja wao ila ... kampuni yetu inajaribu ku introduce huwo umeme wa panga boy ... maana TURBINES (WIND MILLS) tuna contacts from France na wanahitaji to introduce this in Tanzania
 
Wengine sasa mtataka hata JWTZ tulibinaifishe. POLISI nayo ifuate na ikibidi hata IKULU na Bunge liendeshwe na watu binafsi. Jamani tutabinaifisha hata WAKE ZETU na watoto. Hawa Mafisadi kama wangeliweza kufanya hivyo basi wangelifuata hata wake za watu na watoto wao na Punda wao na .....
Hakuna upuuzi duniani kama kufanya hivyo. TANESCO imeliwa wee na sasa mzigo wanaubeba Wananchi. Heri itangazwe moja kwa moja kuwa TANESCO is there to stay na hakuna KENGE yoyote kuja kuleta KALUFUDI kake. Hutu tulufundi kama RICHMOND na kaka zake (utafikiri Babu Seya Family ya UMEME) walioufanya ndiyo umetufikisha hapa tulipo. Kwanza wavunje mikataba na kudai chetu na hapo waangalie uwezekano wa kuliendesha upya kwa ufanisi na hawa jamaa WAJITUME. Tanzania tunavyoTANUA kwa zamu sisi, laiti tungelichakalika hivyo hivyo, hata OMBA OMBA wetu wangelikuwa BOMBA.

Ubinafishaji sio kitu kibaya babu tatizo ni njisi serikali yetu inavyojiingiza kichwa kichwa. Dunia inasonga mbele.Ukitegemea kuwa sera za ujaa zitakuwa na nafasi huko tunakokwenda, unakosea sana.
 
uchambuzi makini mdau. tatizo la tanesco ni mgt tuuuuuuuu. kama mikataba mibovu inaingizwa pale kwa nini uongozi ukubali.ok, watajitetea political push. uendeshaji wa tanesco haundeani na mazingira ya soko. WHY? poor planning and organization structure.
hawawezi kufanya generation, transmission na distribution wenyewe ni upuuzi. hilo shirika ni mzigo kwa serikali lifumuliwe lijiendeshe kibishara na kwa faida. wako watu pale very unnecessary wanaongeza overhead costs na ufanisi sifuri.
tanesco ifumuliwe mapema iwe market driven, professionalism and profit making firm.
blah blah tuweke kando. serikali iwe na utaratibu wa kussuport disadvantageous population kupata umeme kwa bei nzuri through funding.

Management inayoingiliwa katika kazi zake za kila siku na mafisadi toka mafisadi walio ndani ya chama na serikali kamwe haiwezi kuwa na ufanisi wa aina yoyote. Maamuzi ta IPTL, Richmond, Kiwira, net group prolbems n.k. kama yangeachwa yafanywe na management na board of directors ya TANESCO basi si ajabu hii mikataba yote isingesainiwa. Fisadi Mkapa pamoja na kuwa hajui chochote kuhusu management wala umeme akatuingizia wasouth Africa kwa mtutu wa bunduki pamoja na kuwa Watanzania wengi tulipinga uamuzi huo. Matokeo ya uamuzi huo tunayajua.

Mafisadi wakaenda kujadili mikataba ya IPTL, Richmond n.k. pamoja na kuwa maamuzi yao yalipingwa lakini na management ya TANESCO walitumia kura yao ya veto kulazimisha mikataba hiyo. Waziri au Katibu mkuu ambaye ana uwezo wa kutangaza kesho yake kwamba Managing director wa TANESCO ameondolewa kwa manufaa ya umma, huwezi kumpinga.

Sasa umefika wakati nafasi nyeti zote katika mashirika yetu nyeti kama TANESCO, board of directors ndiyo wawe wanapewa nafasi ya kuwahoji waombaji mbali mbali wa nafasi za juu katika mashirika hayo na wao ndiyo wawe watu wa mwisho kuamua ni nani kati ya hao waombaji ndiye anayestahili kupewa nafasi iliyotangazwa. Badala ya Rais kufanya hivyo na mashirika hayo yapewe uhuru wa kweli na si kuingiliwa ingiliwa na wanasiasa wasiojua chochote kuhusu mashirika hayo. Vinginevyo mashirika yetu hayatakuwa na ufanisi.

TANESCO inaidai Z'bar bilioni 22 lakini hawataki kulipa, na kwa sababu ya muungano. TANESCO wanakosa pesa nyingi ili kuboresha mitambo yao na pia kuongeza huduma kwa wale ambao hawana umeme. Mashule ya serikali, Mahospitali, Majeshi, polisi n.k. yanatumia umeme na bills kufika mpaka mabilioni, serikali hailipi na hili pia linainyima TANESCO nafasi ya kuboresha huduma zake muhimu.

Hatuwezi kubinafsisha hata mashirika nyeti kama TANESCO, na ubinafsishaji siyo siku zote huleta ufanisi, hata katika nchi za magharibi mashirika yanayoendeshwa n watu binafsi pia huanguka, mfano halisi ni ENRON na yako mengi tu yanayoanguka.

Nilishangaa wakati Net Group walipoingia TANESCO kama sikosei madeni ya taasisi hizo yalikuwa yamefikia bilioni 22. Mkapa akaamuru hazina walipe deni lote mara moja na net group wakapewa na percentage eti kwa kuwa ni wakusanyaji wazuri wa madeni ukilinganisha na wazawa!!!! Ni usanii wa hali ya juu na bila wanasiasa kukaa pembeni na kuwaacha huru watendaji wa mashirika hayo kufanya kazi zao, basi itakuwa vigumu mno kuona shirika la TANESCO linafanikiwa.
 
Back
Top Bottom