Tanzanian Surfers Loves News, Entertainment and Pornography

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,602
Its a sad truth but truth nevertheless. Today I was making rating based on Alexa on how much Tanzanians who surf do like to visit. Thanks to google and many other tools, I did not had to open every link and see what is inside (well I hate much of what is termed as "entertainment") but here are my discovery: Much of Tanzania Traffic travels towards social Entertainments/Sports, News and Pornography.

The few People who like to study more useful stuffs ranked very low. As a matter of Guess, Adobe ranked high because people would download Adobe flashplayer for Youtube videos. Only CNet narowly managed to be on the lower ranks of the list followed closely by eHow.

Since much of internet users in Tanzania are Youngsters and few older men, what is our picture of tomorrow?

Parents needs to do something for the kids. No am not talking of a home PRISM but teach kids how to make constructive use of time and bytes than destroying their minds with such things as porn!

Whats is your thought on this trend?
Source: Tanzanian Surfers Loves News, Entertainment and Pornography
 
Mie kwenye net naangalia sports and news zaidi.

Hapo unataka kuniambia they are not useful staff?

ndio maana jf ambayo ni social iko namba moja, global namba mbili na ma blog ya udaku yanafuatwa na rahatupu kwa ukaribu, we uliza clip ya wanafunzi wa cbe utapewa info mpk chumba walichokuwa, CTO
 
Last edited by a moderator:
hata marekani na uingereza udaku unapendwa sana, angalia e! entertainment(tv) na the sun (jarida) zinavofagiliwa
 
Mie kwenye net naangalia sports and news zaidi.

Hapo unataka kuniambia they are not useful staff?
EMT,
hapana lakini traffic kuwa kubwa maeneo hayo ni reflection kuwa hiyo ndiyo "major activity" ya Watanzania wengi mtandaoni. Kuangalia Sport sio issue as long as inabaki kuwa side issue na sio core. South wanaongoza kwa kutpita mambo ya finance na Teknolojia japo nao wana yao. No wonder SA wako mbali kifedha/kiuchumi na sisi tuko juu kiudaku ;)

Shocking fact ni kuwa Porno ni moja ya "Major activities"...Ongea na IT supports watakwambia BW zinavyoliwa ofisini na Waangalia ngono mtandaoni. Anyway wanawalazimisha System admins kuweka Cyberoam and the co!
 
ndio maana jf ambayo ni social iko namba moja, global namba mbili na ma blog ya udaku yanafuatwa na rahatupu kwa ukaribu, we uliza clip ya wanafunzi wa cbe utapewa info mpk chumba walichokuwa, CTO
Lazima tubadilike toka Udaku Republic mpaka Serious Republic. Else tutafit kuwa "Banana Republic"

Hapo red sijakupata vema @c6
 
Lazima tubadilike toka Udaku Republic mpaka Serious Republic. Else tutafit kuwa "Banana Republic"

Hapo red sijakupata vema @c6

huwezi kuelewa coz hujui mambo ya udaku
 
EMT,hapana lakini traffic kuwa kubwa maeneo hayo ni reflection kuwa hiyo ndiyo "major activity" ya Watanzania wengi mtandaoni. Kuangalia Sport sio issue as long as inabaki kuwa side issue na sio core. South wanaongoza kwa kutpita mambo ya finance na Teknolojia japo nao wana yao. No wonder SA wako mbali kifedha/kiuchumi na sisi tuko juu kiudaku ;)

Sijaelewa una maana gani unaposema "Kuangalia Sport sio issue as long as inabaki kuwa side issue na sio core." Kwa nini sports iwe side rather than core issue kwenye jamii? Do you know the amount of money nchi nyingine zina-invest kwenye sports?

Kwa hiyo, unakubaliana na wale walioondoa sports as core activity mashuleni? Kila wakati tunalalamika kuwa hatufanyi vizuri kwenye sports but we won't do better kama sports itaendelea kubakia side issue.

Kuna nchi nyingine zinajulikana tuu kutokana na sports. Most will associate Brazil with football, Kenya na riadha, n.k. Mataifa mengine kama China na Japan tayari yameona umuhimu wa kuchukulia serious michezo and thus, they are making huge investments kwenye sports.

Inawezekana kabisa kuwa South Africa wanaongoza kwa mambo ya finance na teknologia, but they have got financial institutions. Inawezekana teknologia yao iko juu zaidi na hivyo kuzalisha interesting activities on the internet. Lakini kwa sisi what is our biggest financial institutions zinazoweza ku-attract online followers? What is our biggest technology tunayoweza kujivunia?

Personally, I think sports itatusaidia sana kama tukichukulia serious. In fact, itasadia vijana na watoto kujiweka mbali na hayo mambo ya udaku, na badala yake ku-concetrate zaidi kwenye michezo. Itawasaidia vijana kutodhani kuwa siasa ni kila kitu.

Michezo itatujengea umoja na identity zaidi kuliko tuliyonayo sasa. Kama unavyojua taifa linaelekea kugawanyika kwenye vyama. Huko tuendako hali inaweza kuwa mbaya zaidi maana unawezakuta huna kinachokuunganisha na ndugu yako zaidi ya kuzaliwa tumbo moja.

Shocking fact ni kuwa Porno ni moja ya "Major activities"...Ongea na IT supports watakwambia BW zinavyoliwa ofisini na Waangalia ngono mtandaoni. Anyway wanawalazimisha System admins kuweka Cyberoam and the co!

Well, siyo Tanzania, bali kwa dunia nzima the most visited sites ni zile za porn. Kwenye official lists hawaweki hizo sites lakini they are the most visited ones.

Much of world traffic travels towards social entertainment, sports, news and pornography and Tanzania is not an exception.
So, to me this is not shocking, ikizingatiwa pia kuwa kwa tamaduni zetu maongezi ya ngono, n.k ni mwiko kujadiliwa kwenye jamaa, kwa hiyo watu wengi wanaangukia kwenye sites za porn.

Katika dunia na teknologia ya sasa, it is going to be extremely difficult to regulate what people read or watch on the internet. Mengine tunayajadili huku: https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/470391-review-demographics-population-and-youth-leadership-3.html
 
ndio maana jf ambayo ni social iko namba moja, global namba mbili na ma blog ya udaku yanafuatwa na rahatupu kwa ukaribu, we uliza clip ya wanafunzi wa cbe utapewa info mpk chumba walichokuwa, CTO

ujue nilipoiona hio clip ina zaidi ya lisaa limoja nikaona ngoja niigoogle kucheki net blog kibao wanayo. so wapo vizuri wanajua hadi hosting za kuweka video za masaa.
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa una maana gani unaposema "Kuangalia Sport sio issue as long as inabaki kuwa side issue na sio core." Kwa nini sports iwe side rather than core issue kwenye jamii? Do you know the amount of money nchi nyingine zina-invest kwenye sports?

Kwa hiyo, unakubaliana na wale walioondoa sports as core activity mashuleni? Kila wakati tunalalamika kuwa hatufanyi vizuri kwenye sports but we won't do better kama sports itaendelea kubakia side issue.

Kuna nchi nyingine zinajulikana tuu kutokana na sports. Kama mtu akitaja Brazil most will associate Brazil with football, Kenya na riadha, n.k. Mataifa mengine kama China na Japan tayari yameona umuhimu wa kuchukulia serious michezo and thus, they are making huge investment kwenye sports.

Inawezekana kabisa kuwa South Africa wanaongoza kwa mambo ya finance na teknologia, but they have got financial institutions. Inawezekana teknologia yao iko juu zaidi na hivyo kuzalisha interesting activities on the internet. Lakini kwa sisi what is our biggest financial institutions zinazoweza ku-attract online followers? What is our biggest technology tunayoweza kujivunia?

Personally, I think sports itatusaidia sana kama tukichukulia serious. In fact, itasadia vijana na watoto kujiweka mbali na hayo mambo ya udaku, na badala yake ku-concetrate zaidi kwenye michezo. Itawasaidia vijana kutodhani kuwa siasa ni kila kitu.

Michezo itatujengea umoja na identity zaidi kuliko tuliyonayo sasa. Kama unavyojua taifa linaelekea kugawanyika kwenye vyama. Huko tuendako hali inaweza kuwa mbaya zaidi maana unawezakuta huna kinachokuunganisha na ndugu yako zaidi ya kuzaliwa tumbo moja.Well, siyo Tanzania, bali kwa dunia nzima the most visited sites ni zile za porn. Kwenye official lists haweki hizo sites lakini they are the most visited ones.

Much of world traffic travels towards social entertainment, sports, news and pornography and Tanzania is not an exception.
So, to me this is not shocking, ikizingatiwa pia kuwa kwa tamaduni zetu maongezi ya ngono, n.k ni mwiko kujadiliwa kwenye jamaa, kwa hiyo watu wengi wanaangukia kwenye sites za porn.

Katika dunia na teknologia ya sasa, it is going to be extremely difficult to regulate what people read or watch on the internet. Mengine tunayajadili huku: https://www.jamiiforums.com/great-t...aphics-population-and-youth-leadership-3.html

mkuu sport hio hio inaweza kuwa pato au upuuzi. sisi sport tunapenda udaku wake tunakesha kwenye tetesi za transfer news wakati hata sheria za soka hatuhangaiki kusoma.

hao wanaowekeza kwenye michezo wanaisoma michezo vizuri kiundani na sio udaku wa michezo.

kuhusu dunia inachofanya na si tufanye sidhani kama ni uamuzi wa busara sisi tunatakiwa tuonyeshe mfano
 
............... Do you know the amount of money nchi nyingine zina-invest kwenye sports?

...................Kwa hiyo, unakubaliana na wale walioondoa sports as core activity mashuleni?

Kuna nchi nyingine zinajulikana tuu kutokana na sports. Most will associate Brazil with football, Kenya na riadha, n.k. Mataifa mengine kama China na Japan tayari yameona umuhimu wa kuchukulia serious michezo and thus, they are making huge investments kwenye sports.

Inawezekana kabisa kuwa South Africa wanaongoza kwa mambo ya finance na teknologia, but they have got financial institutions. Inawezekana teknologia yao iko juu zaidi na hivyo kuzalisha interesting activities on the internet. Lakini kwa sisi what is our biggest financial institutions zinazoweza ku-attract online followers? What is our biggest technology tunayoweza kujivunia?

Personally, I think sports itatusaidia sana kama tukichukulia serious. In fact, itasadia vijana na watoto kujiweka mbali na hayo mambo ya udaku, na badala yake ku-concetrate zaidi kwenye michezo. Itawasaidia vijana kutodhani kuwa siasa ni kila kitu.

Michezo itatujengea umoja na identity zaidi kuliko tuliyonayo sasa. Kama unavyojua taifa linaelekea kugawanyika kwenye vyama. Huko tuendako hali inaweza kuwa mbaya zaidi maana unawezakuta huna kinachokuunganisha na ndugu yako zaidi ya kuzaliwa tumbo moja.Well, siyo Tanzania, bali kwa dunia nzima the most visited sites ni zile za porn. Kwenye official lists hawaweki hizo sites lakini they are the most visited ones.

Much of world traffic travels towards social entertainment, sports, news and pornography and Tanzania is not an exception.
So, to me this is not shocking, ikizingatiwa pia kuwa kwa tamaduni zetu maongezi ya ngono, n.k ni mwiko kujadiliwa kwenye jamaa, kwa hiyo watu wengi wanaangukia kwenye sites za porn.

Katika dunia na teknologia ya sasa, it is going to be extremely difficult to regulate what people read or watch on the internet. Mengine tunayajadili huku: https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/470391-review-demographics-population-and-youth-leadership-3.html

Ingekuwa tunaongea ingekuwa rahisi zaidi ila inabidi nitaipu. Tutafanyaje bana.... inabidi usome tu.. ni mengi ila soma tu.

EMT niambie....

Ni nchi zipi hizo zinazoinvest sana kwenye sports? Je wananchi wake wana maoni gani juu ya sports (maoni ambayo yana mantiki)? Je nchi hizo zimeinvest vipi katika mambo mengine (proportionally)? Umetaja China, Japan, Brazil, Afrika Kusini na Kenya. Nitazichambua.....

CHINA, BRAZIL, JAPAN, AFRIKA KUSINI na KENYA.

China

China na nchi ya pili kwa uchumi duniani, Japan ya tatu, sijafuatilia Brazil ya ngapi (UCHUMI WAKE UNAZIDI UINGEREZA (kwa mujibu wa BBC)), Kenya (Namba moja kiuchumi E. A.) nitaielezea pia kwa kina kwa kuhusisha mambo nayofanya mimi binafsi.

China inapambana iwezavyo katika uchumi wa dunia. Inainvest katika biashara.. kwa maana ya viwanda, teknolojia sayansi kwa kiasi kikubwa. Saikolojia ya watu wa China ni juu ya superiority. China inajilazimisha (hongera zao) kuwa superpower kwa uchumi na hata sifa. Ngoja ninyooshe lugha.......

Vijana wa China pamoja na kuwa wanaangalia porno kama vijana kama sisi lakini nikwambie wameweka nguvu kubwa sana katika mambo mengine ya tafiti kuliko sisi... nazungumzia akili ya vijana wa China in proportion to China itself na Tanzania in its own proportion.... China wako juu sana kwa ratio (in my opinion). China inajenga bandari Bagamoyo. Wanatengeneza ndege zao za kijeshi.. wakiinvest pia katika michezo ni sawa.

Brazil.
Soccer ndiyo mchezo unaotajwa kuwa maarufu zaidi duniani. Brazil ndiyo nchi pekee kwa sasa ambayo haijakosa kushiriki fainali za Kombe la Dunia. Kwa kuwa soccer ni maarufu sana Brazil nayo inavuma sana kwa hili. Je unajua (najua unajua) kuwa wananchi wake kwa sasa wanaandamana kupinga "mapesa" mengi kutupwa kwenye soccer (FIFA World Cup)? Je wananchi hawa wana akili timamu na madai yao ni ya msingi? Marekani, China, India, Urusi wanaionaje Brazil? Soccer? Hapana. Brazil ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa (soccer ikiwa na mchango mdogo) zaidi Amerika ya Kusini. Brazil ina viwanda balaa... inatengeneza hata ndege za abiria... Inavuma kwa soccer kwa kuwa soccer inapigiwa kelele sana. Mashabiki wa soccer wana kelele.

Wakati bajeti ya Waziri Meghji (Fedha wakati huo) ilipoumiza watu... kelele zikaja... "Bajeti imetuudhi ila tumepozwa na Taifa Stars ilipoifunga Burkina Faso." Bajeti imepita haijapita?... Imepitaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! Asante! (Wachezaji walipelekwa bungeni).

Japan.

Ya tatu kiuchumi duniani. Viwanda. Maelezo yake ni kama China. Mengine mengi unajua juu ya JAPAN... angalia muundo wa arguments zangu then extrapolate. Tanzania inakimbilia ushabiki wa michezo (siyo michezo)....Ushabiki wa burudani na kufuata mikumbo siyo kuunda burudani. Uwanja wa Taifa wa soccer uliwekewa nguvu sana na China na siku ya kwanza tu ya ufunguzi baadhi ya mashabiki waling'oa koki za mabomba.

Kenya.
Inavuma kwa riadha. Sana tu. Je hili ndilo kuu? Hapana. Najiuliza kwa akili ya Kizungu..: "Wanyamapori... pundamilia wazuri, twiga, simba, tembo etc wanapatikana zaidi Afrika... interesting... nasikia kuna watu wanaitwa Wamaasai... nasikia ni noma hao...... kuna lugha inaitwa Kiswahili..."

EMT niambie hao wanyama wako wapi zaidi? Kiswahili kinazungumzwa wapi? Wamaasai wako wapi? Nasikitika kusema kuwa wako Kenya. Kiswahili kinazungumzwa Kenya (Microsoft... Choose Windows language (XP, Vista...).. (Kiswahili Kenya)). GMT+3 (Nairobi). IT East Afrika inakuwa practised zaidi Kenya (hata kama ni propaganda).

Mimi ni Graphics Designer.. sasa najifunza animation privately.... kwa nyanja zote hizi Kenya wametuacha sana. Kuna baadhi ya mambo yanaweza kutoa taswira ya nchi... miongoni ni matumizi ya teknolojia kama hizi.. kwa Tanzania chuo serious cha animation ni MediaOne pekee achana na propaganda za DIT... acha nijifunze mwenye. Kenya vyuo kibao (well maybe 10).

Afrika Kusini
Nchi yenye nguvu zaidi kiuchumi Afrika. Ukitaka DVD ya trial au full ya Adobe Master Collection kwa Afrika utaipata Afrika Kusini pekee (kwa sasa). Animation pekee yenye urefu wa feature film kutoka Afrika ni ya Afrika Kusini: Adventures in Zambezia, nyingine inatoka mwaka huu na ni 3D stereoscopic. Kirikou iliyovuma hapa TZ ni ya Mfaransa Michel Ocelot. S. Afrika inang'ara kwa mengi makubwa hasa ya kiviwanda na Mzee Mandela (apone haraka) na si michezo, mashabiki wa michezo wanadhani inavuma sababu ya Siyabonga Nomvete (Enzi hizo)!!

MSIMAMO WANGU JUU YA MICHEZO (Je inafaa mashuleni?)

Kwa nchi changa kama zetu ni hatari sana michezo ikawa mbele kwa kiasi nikionacho sasa. Nchi ZOTE zilizoendelea duniani zimeendelea kwa sababu ya viwanda ama raw materials zinazofeed viwanda. Elimu inayochagiza tafiti za kisayansi na teknolojia inakuza sana uchumi na uwezo wa nchi katika kukabiliana na mashinikizo au mashindano ya kiuchumi. Michezo inalipa zaidi kama tayari kuna backbones za maendeleo mengine.. vinchi kama Cameroun vinavuma kwa soka Afrika lakini ni masikini sana. Soka haliisaidii Nigeria wala Mali wala Burkina Faso wala Misri, wala Ivory Coast wala Senegal. Mashabiki wapo hakuna uchumi (wa maana).

Burudani na Michezo Tanzania...
Ukiangalia vizuri participation kubwa ya Tanzania katika michezo ni ya kishabiki/kiushabiki zaidi ya kiuchezaji. TZ ukisema michezo unazungumzia soka. Ukizungumzia soka la ndani unazungumzia udaku wa soka. Udaku wa soka ni Simba na Yanga. Magazeti yanajaribu (Na kufanikiwa) kudanganya/kupumbaza wasomaji kwa kauli kama "Simba ni noma... Yanga ni bomba mbaya... Zamalek kukiona cha mtema kuni....." Basi ukiangalia wasomaji wanavyofukuzana kununua Championi na Bingwa utashangaa.. habari yenyewe Mbuyu Twite amwashia Rage indiketa.. inauma sana. "Waliondelea" au "kusoma" wanashabikia Man U. Mwakani kombe la dunia.. chagua Brazil au Spain.

Ndiyo lazima tuburudike lakini nikwambie kuna vijana wamekuja nyumbani kwangu kutaka kujiunga facebook (kuna kompyuta hapa) ilhali hajui hata kuclick mouse ya kompyuta.. sitanii. Networking is good lakini vijana wa sasa wanawaza sana starehe (entertainment). Wenye facebook wenyewe wameinvest. Nakumbuka bajeti ya mwisho ya Mustafa Mkulo kama Waziri wa Fedha (Bajeti ya serikali ya mwaka) ilikuwa inazidiwa na utajiri wa mmoja wa waasisi wa facebook Mark Zuckerberg.

Michezo ina faida mbalimbali za kiuchumi na zaidi za kiafya na saikolojia. Wanafunzi washiriki michezo. Ila msingi mkuu wa nchi usiwe michezo.. wala burudani isiwe na nguvu kama sasa...

Kama Taifa tunahitaji brains katika sayansi, technolojia, tafiti, uzalishaji na ndipo michezo itafaa. Kila mtu mzima kwa namna fulani anajihusisha/amejihusisha/ana msukumo fulani juu ya ngono lakini wenzetu wameweka nguvu kubwa sana katika mambo mengine zaidi ya hili. Hata umalaya Ulaya sasa ni biashara na watu wanalipa kodi na si burudani tu na kustarehe bila faida za kiuchumi.

WATANZANIA TUONGEZE NGUVU KATIKA SAYANSI/TAFITI, TEKNOLOJIA, KILIMO, VIWANDA etc na TUPUNGUNGUZE KUFANYA STAREHE na KUTUMIA MUDA MWINGI KWENYE SOCIAL NETWORKS.

"Ukitaka kujua juu ya Taifa lijalo angalia vijana wa sasa." - Ngugi wa Thiong'o.
 
Last edited by a moderator:
Magembe R. Malima,

Sidhani kama nchi nyingi zinazoendelea zinajua nguvu ya michezo katika maendeleo ya taifa. Nafikiri tatitzo kubwa tulilonalo ni kwamba hatuchukulii michezo kama sekta ya maendeleo inayojitegemea na uhusiano wake na sekta nyingine za maendeleo. Bado tunachukulia michezo kama burudani na ushabiki tuu na si vingenevyo.

Lakini kwa mataifa mengine michezo ni sekta mpya inayojitegemea na inayokua kwa kasi. Sidhani kama Marekani walindaaa Fainali za Kombe la Dunia, na China Olympics for the sake of it. Siku hizi mpaka vyuo vinatoa degrees in sports. Bakground yangu ni sheria. Mara ya kwanza kabisa nilipoona chuo kinatangaza kwenye prospectus Masters of Laws in Sports nilishangaa sana and thought I will never pay for such a course. Nilidhani eti labda kutakuwa na module ya football ambapo nitajifunza FIFA's Laws of the Game kama off side, corner, nk.

But it was completely different subject focusing primarily on sports as an emerging new commercial industry and how the law should respond to it. Baada ya miaka kupita courses kama hizi zimekuwa hot cake sana kwa nchi husika. Sports is now a special branch of law kwa nchi nyingi. Lakini kwa hapa kwetu bado tunaona sports as not an independent industry ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa nchi.

Hii ni kwa sababu bado hatuchukulii na bado hatuonyeshi nia ya kuchukukulia sports za a distinct industry which deserve a special attention. Kwa mfano, Rais wetu alikuwa huko kwenye klabu ya Sunderland kuona kama wanaweza kuanzisha sports academic Tanzania. Itafanikiwa kweli kama bado tunachukulia sports kama ni kwa ajili ya afya na saikologia?

Nilidhani kwa mtu wa IT kama wewe ungeona umuhimu wa sports kama path nyingine ya ajira, uwekezaji na uhusiano wake na sekta nyingine kama merchandising, media na broadcasting, licensing, etc. Nilidhani kwa mtu wa IT kama wewe ungeona umuhimu wa sports katika kutumia ICT katika nyanja na ngazi zote. Siku hizi kuna mpaka wanaospecialise kwenye Sport Graphic Designing ambapo unatakiwa kujua how the digital sports media works.

Wenzetu kwa kutambua sports kama industry imesaidia kuanzishwa kwa makapuni makubwa ambayo yanafanya kazi na premium sporting brands kutoa digital sports services in the emerging new sporting markets. Makampuni haya yanafanya kazi na vilabu vya michezo, wachezaji, vyama vya michezo, kutengeneza desktop and mobile sites, applications, digital and markerting programmes, products, services, and advertisement. Lakini wewe as a graphic designer bado unaona sports ni kwa ajili ya afya na saikologia tuu? I thought graphic designing is a creative job?

Michezo kama sekta inayotambuliwa rasmi inaweza kusaidia sana kwenye kuongeza ajira na biashara kuanzia wanamichezo wenyewe, mameneja, personnel, media, wafanya biashara, graphic designers kama wewe, n.k. Lakini bado vyama vingi vya soka barani Afrika, kikiwemo kile cha kwetu, havioni kuwa kufanikiwa kuchezea, kwa mfano, Fainali za Kombe la Dunia ni zaidi ya prestige. Hatuoni kuwa hiyo nafasi inaweza kutumika kama business proposition kwa sababu bado hatuoni kama sports inaweza kuwa a viable business opportunity na kutoa mchango mkubwa kwa taifa.

Kuna mtu mmoja twitter alikuwa anahoji kwa nini Taifa Stars isiwe inatengenezewa jezi zake na makampuni kama Nike, Addidas, nk? Sasa kama tunadhani soka ni kwa ajili ya afya na saikolojia kwa nini makampuni makubwa kama Nike yapoteze pesa zao kutu-sponsor? Si heri wajikite kuendelea kuwa-sponsor Tahiti ambao pamoja na kuwa wachezaji wake ni wafua nazi lakini wako serious na soka na wanaichukulia kama ni profession which can generate income to the country?

Nimefuatilia sana kinachoendelea Brazil. Originally protests zilikuwa dhidi ya kupanda kwa nauli Sao Paolo, lakini baadae ikasambaa miji mingine kwa sababu mbali mbali zikiwemo rushwa, huduma mbaya za afya na gharama za ku-host fainali za kombe la dunia. I am sure kama mambo yangekuwa safi kwenye hizo sekta nyingine, then wala wasingepinga kuandaa hizo fainali. Common sense ni kwamba hakuna haja ya kuwekeza kwenye kuandaa mashindano makubwa kama hayo kama sekta nyingine zinayumba. Lakini hii haina maana kuwa kwa kuwa sekta nyingine za uchumi zinayumba basi tusi-pursue other opportunities. It is about how they prioritized.

Napingana na wewe kuwa Brazil inavuma kwa soka kwa sababu mashabiki wa soka wa huko wana kelele sana. Really? Tofauti na nchi nyingine nyingi, soka ni kama sehemu ya utamaduni wa Brazil. The fact kuwa ni part ya culture yao haina maana kuwa wanapiga kelele. Indeed, mwanzoni, Brazil hawakuwachukulia soka kama biashara. Lakini hivi karibuni kumekuwa na utajiri mpya unaongia Brazil kutokana na uwekezaji kwenye soka, udhamini na broadcasting. Ni juzi tuu British Telecommunication imeingia mkataba na waendeshaji wa ligi kuu ya Brazil kuonyesha live matches za ligi ya Brazil huko Ulaya kwa mara kwanza.

Pamoja na wachezaji wengi bora wa Brazil kukimbilia kwenye ligi za Ulaya, bado wapo wengi pia wanarudi nyumbani kutokana na ligi yao kuboreshwa na kuwa ya kibiashara zaidi. Kwa mfano, inadaiwa kuwa sababu za Neymair kukaa Brazil kwa muda wote huo kabla ya kuamua kwenda Ulaya ilitokana na kulipwa £400,000 kila mwezi. Hapo klabu yake ilikuwa inalipa asimilia 20 tuu ya mshahara wake, huku asimilia 80 ikilipwa kupitia sponsors, through his images rights (maana nasikia anamiliki 50% of his image rights). Pia kutokana na sheria mpya za UEFA on home grown players kuna dalili ya kupungua kwa wachezaji wanaoenda kuchezea timu za Ulaya.

Sina maana kuwa as a nation we should only focus on sports to the detriment of science and technology, research and production. Indeed, we should use every brain available. Lakini kwanza tusisahau kuwa hata kwenye sports kunahitajika science, technology, research and production na siyo kujikita kwenye kuboresha afya tuu na saikolojia tuu. As a graphic designer, I am sure you won't mind using your technological know how in making money kupitia vitu kama hivi: http://designm.ag/inspiration/showcase-sports-in-graphic-design/

Sports inaweza kuchangia sana kwenye national development in many ways if it is taken seriously as a distinct industry. "In most African countries, sport is seen as a service programme and not as a potential industry to generate revenue but on the contrary, most countries see sports as a financial liability": Play the Game: Using Sports in National Development

Pili, as a nations, we have talents whose their talents can be converted into business opportunities na kuchangia kwenye maendeleo ya taifa. Kama tukiweza ku-convert hobbies na ushabiki tulio nao kwenye michezo mbalimbali, then there is a potential of creating successful businesses.

Lakini kama tunatendea ku-focus on traditional understanding of sports kama njia ya kuimarisha afya tuu na saikologia, then probably we are not thinking creatively how we can convert what we love into business. Juzi juzi hapa nilikuwa naangalia documentary moja ya Hip Hop ilivyokuwa converted from street culture into a multibillion dollar industry. Kwa sasa sports and the entertainment industries remain largely untapped in Africa, but they may have a potential of becoming multimillion dollar industries.

Hata hivyo, ili tuweze kuvuna pesa huko tutahitaji watu wa IT kama wewe kundokana na traditional understanding kuwa sports ni kwa ajili ya ku-maintain afya na kuboresha saikologia. Tunahitaji IT experts ambao wanaweza kutumia their expertise not only in the traditional technological industries bali pia in the new emerging industries kama sports and entertainment, ambazo kama zikitiliwa mkazo kibiashara zaidi zinaweza kuchangia sana kwenye maendeleo ya taifa.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo mmeshindwa kuelewa entertainment,i.e burudani na starehe ..sasa kama %kubwa ya vijana Tz wanapenda burudani na starehe haijalishi ni aina gani unaona future gani huko mbele?

Fanyeni kazi kwanza,invest kwenye mambo ya maana hata hao wanaowekeza ktk burudani na starehe walianza kutengeneza vichwa na siyo starehe ..
 
Magembe R. Malima,

..... Itafanikiwa kweli kama bado tunachukulia sports kama ni kwa ajili ya afya na saikologia?

Nilidhani kwa mtu wa IT kama wewe ungeona umuhimu wa sports kama.................... licensing, etc. Nilidhani kwa mtu wa IT kama wewe ungeona umuhimu wa sports katika kutumia ICT katika .................. Siku hizi kuna mpaka wanaospecialise kwenye Sport Graphic Designing ambapo unatakiwa kujua how the digital sports media works.

Wenzetu kwa kutambua sports kama industry imesaidia ................................... markerting programmes, products, services, and advertisement. Lakini wewe as a graphic designer bado unaona sports ni kwa ajili ya afya na saikologia tuu? I thought graphic designing is a creative job?

............................ graphic designers kama wewe, n.k. Lakini bado ...........................

Kuna mtu mmoja twitter ...................... Sasa kama tunadhani soka ni kwa ajili ya afya na saikolojia kwa nini makampuni makubwa kama Nike ...............................

Nimefuatilia sana kinachoendelea Brazil. Originally protests zilikuwa dhidi ya kupanda kwa nauli Sao Paolo, lakini baadae ............................. rushwa, huduma mbaya za afya na gharama za ku-host fainali za kombe la dunia. I am sure kama mambo yangekuwa safi kwenye hizo sekta nyingine, then wala wasingepinga kuandaa hizo fainali. Common sense ni kwamba hakuna haja ya kuwekeza kwenye kuandaa mashindano makubwa kama hayo kama sekta nyingine zinayumba. Lakini hii haina maana kuwa .................... It is about how they prioritized.

Napingana na wewe kuwa Brazil inavuma kwa soka kwa sababu mashabiki wa soka wa huko wana kelele sana. Really? Tofauti na nchi nyingine nyingi, soka ni kama sehemu ya utamaduni wa Brazil. The fact kuwa ni part ya culture yao haina maana kuwa wanapiga kelele. ....

Pamoja na wachezaji wengi bora wa Brazil kukimbilia kwenye ligi za Ulaya, bado wapo wengi pia wanarudi nyumbani kutokana na ligi yao kuboreshwa na kuwa ya kibiashara zaidi. Kwa mfano, inadaiwa kuwa sababu za Neymair kukaa Brazil kwa muda wote huo kabla ya kuamua kwenda Ulaya ilitokana na kulipwa £400,000 kila mwezi. Hapo klabu yake ilikuwa inalipa asimilia 20 tuu ya mshahara wake, huku asimilia 80 ikilipwa kupitia sponsors, through his images rights (maana nasikia anamiliki 50% of his image rights). Pia kutokana na sheria mpya za UEFA on home grown players kuna dalili ya kupungua kwa wachezaji wanaoenda kuchezea timu za Ulaya.

Sina maana kuwa as a nation...........................Lakini kwanza tusisahau kuwa hata kwenye sports kunahitajika science, technology, research and production na siyo kujikita kwenye kuboresha afya tuu na saikolojia tuu. As a graphic designer, I am sure you won't mind using your technological know how in making money kupitia vitu kama hivi: http://designm.ag/inspiration/showcase-sports-in-graphic-design/

Lakini kama tunatendea ku-focus on traditional understanding of sports kama njia ya kuimarisha afya tuu na saikologia, then probably we are not thinking creatively how we can ..............................

Hata hivyo, ili tuweze kuvuna pesa huko tutahitaji watu wa IT kama wewe kundokana na traditional understanding kuwa sports ni kwa ajili ya ku-maintain afya na kuboresha saikologia. ..........
Ningependa nitolee ufafanuzi mambo haya, ambayo kwayo, naona "Jeshi limetumia nguvu kubwa mno katika kuzima maandamano":

GRAPHIC DESIGN AS A CREATIVE INDUSTRY (Artistic Creativity Vs Business Creativity)

Sentensi "Graphic Design is a Creative Industry." ni ya kweli lakini maana yake inaishia katika ubunifu wa sanaa basi. Ubunifu katika biashara hauna uhusiano na creativity katika graphic design bali katika kila profession iwe graphic design, sheria, elimu, michezo, afya, utamaduni, viwanda n.k. Kwa kifupi BUSINESS CREATIVITY ndiyo ENTREPRENEURSHIP.

Mimi naweza kuwa very creative kama Graphics designer but with very poor entrepreneurial skills/spirit. Katika link uliyoweka http://designm.ag/inspiration/showcase-sports-in-graphic-design/ picha zinazooneshwa hapo zinaonesha tu artistic creativity lakini juu yake kuna link inayosema... "Learn how to earn $125 or more per hour as a freelancer - Click Here" Hii sasa ndiyo business creativity. Career yoyote inaweza kufanya ubunifu kama huu. Naamini kwa sasa hakuna mkanganyiko tena wa neno CREATIVE katika sentensi "Graphic Design is a Creative Industry."

GRAPHIC DESIGN/IT in SPORTS

"Nilidhani mtu wa IT kaka wewe ungeona......" EMT macho ya mtu wa IT/Graphic design hapa najisema mimi sasa hayaishii kuona opportunities za pesa/biashara/uwekezaji katika mambo ya "maana" tu bali hata katika michezo kama unavyosema. Uzito au umuhimu wa uwekezaji katika Sports graphics ni very contextual... ila sii-skip kwa kuwa tu ni sports. MJadala sasa ni nini...maelezo yangu yako katika aya ya mwisho ya bandiko langu hili.

KELELE ZA MASHABIKI WA MPIRA
(Siyo mashabiki wa Michezo)

Si kweli kuwa mashabiki wa Brazil ndiyo wenye kelele zaidi duniani ndiyo maana Brazil inavuma zaidi kuliko nchi zingine katika soka. Kama ingekuwa hivyo basi Uingereza ndiyo ingevuma zaidi kwa kuwa nadhani hakuna mashabiki wenye mikiki-mikiki kama Waingereza. Kelele nazozizungumzia ni za mashabiki wa soka duniani kote. Na kelele hizi haziishii katika sauti za juu ndani na nje ya viwanja... kelele hizi ni pamoja na mavugu-vugu/fukuto yote yanayoambatana na mpira wa soka. Soka kama mchezo ndiyo mchezo unaopendwa na watu wengi zaidi duniani hivyo ni rahisi sana kusikia habari zake mtaani. Hii ina maana wababe katika medani hiyo watavuma...wababe wa soka ni akina nani...labda Hispania, labda Ujerumani... ila Brazil wana historia ndefu na wanavuma zaidi... watu wengi (hadi mashabiki wepesi) wanamjua Pele ila ni wachache sana wanamjua Franz Beckenbauer. Respect to Diego Mara.

Nachosema mimi ni kuwa Brazil ni zaidi ya soka na nasisitiza Brazil ina nguvu katika uchumi kwa mbali ukilinganisha na soka ila soka ndiyo inapigiwa chapuo sana kwa kuwa uchumi hauwekewi loud speakers na watu wengi (duniani pote) wakiona habari za uchumi katika media wanapoteza interest hivyo habari nyingi zinawapita. Michezo kama golf ina nguvu baadhi ya maeneo ambako soka ina nguvu (bahati mbaya ndiyo sehemu kubwa duniani) hutasikia sana michezo hii. Ulizia Cricket ama Rugby New Zealand au Australia.... noma. Au basketball Marekani.

Ni kweli kuwa soka kwa Brazil ni kama utamaduni. Si Brazil tu bali Amerika yote ya Kusini na Kati... Uruguay (Mabingwa wa kwanza wa Kombe la Dunia), Chile, Mexico, Argentina etc. tofauti na India, Sri Lanka...... (that region) in exception to bara Arabia na Mashariki ya mbali.

FAIDA ZA MICHEZO (AFYA na SAIKOLOJIA tu Vs Uchumi na Ajira) - SPORTS AND GAMES

Afya na Saikolojia
Mtu anayedhani kuwa michezo ina faida za Afya na Saikolojia pekee basi hajui au hana hata idea kidogo juu ya uchumi wa michezo na aina ya michezo. Haijalishi mtu huyo ni mimi ama la. Kwanza si kweli kuwa michezo yote inahusisha nguvu ya mwili na ndiyo maana kwa Kiingereza husemwa maneno mawili (matatu): "SPORTS and GAMES." Sidhani kama Tiger Woods anajenga mwili kiviiiile kwa Golf... au wacheza Chess au Pool au Bao, labda mind sharpness pekee (Si saikolojia hii, Saikolojia inayozungumzwa ni Tranquility/Serenity). Kwa kifupi SI KWELI KUWA FAIDA ZA MICHEZO NI AFYA NA SAIKOLOJIA PEKEE bali hata UCHUMI kama nisemavyo hapa chini.

Uchumi
Mbali na michezo hata sanaa zingine huwa zinajumuishwa katika eneo hili la burudani, na watu wengi hudhani kuwa burudani ni kitu cha mwisho (regardless wako right au wrong), kwa mfano, ndiyo maana magazeti yasiyo ya michezo huweka michezo katika ukurasa wa mwisho na pili toka mwisho, taarifa za habari katika radio ama TV husomwa mwishoni.

Kama ulivyosema "I am sure kama mambo yangekuwa safi kwenye hizo sekta nyingine, then wala wasingepinga kuandaa hizo fainali." hata mimi sina tatizo na michezo ama sanaa zingine as long as kuna mambo nayoyasisitiza yanapewa priority ambayo bahati mbaya starehe na burudani ndiyo vinaongoza kwa sasa (specifically kwa Tanzania) na honestly hii ndiyo MADA KUU YA MWEKA THREAD na si michezo pekee ambayo wewe na mimi tunabishania hapa.

Brazil, S.A. etc walioandaa kombe la Dunia si kwa prestige pekee bali uchumi na UKWELI NI KUWA SABABU za KIUCHUMI ndizo zina msukumo wa kwanza. Sasa hoja zangu ni nini kama nakiri jambo hili la uchumi...... namalizia... na ili ku-narrow down mjadala paragraph hii inawahusu zaidi Watanzania.. (Kama Thread ilivyokusudia):
_____________________________________________________________

Kama Taifa tunahitaji brains katika sayansi, technolojia, tafiti, uzalishaji na ndipo michezo itafaa. Sioni namna yoyote Tanzania itaendelea kwa anasa nizionazo kwa vijana na watu wa umri wa kati katika michezo na burudani. Internet yaweza kutumika kujifunza hata masomo/tafiti zaidi ya kuchat na kuweka mapicha facebook kama wafanyavyo watu wengi na hili ndo nalolalamikia. Hakuna namna Tanzania itaendelea bila kuweka mbele elimu itakayopelekea ukuaji wa uchumi wa uzalishaji (manufacturing economy) na hata kama burudani indirectly au directly inaweza kufeed manufacturing industries bado Tanzania haina uwezo wala uwezekano wa kuwa na saikolojia (mindset) ya kuwa na maendeleo ya michezo kwanza ambayo yataboost uchumi. Hakuna namna. Ndiyo maana hata hizo nchi tunazotaja kufaidika kimichezo zina kitu kingine mkononi kwanza (manufacturing economy), science and tech ndipo michezo ama starehe (entertainment) inakuja kuweka nguvu. Vinginevyo tutaishia kuwa wachuuzi katika nchi yetu wenyewe na mashabiki wa nchi zingine.
_______________________________________________________
 
Last edited by a moderator:
hao wanaowekeza kwenye michezo wanaisoma michezo vizuri kiundani na sio udaku wa michezo.

kuhusu dunia inachofanya na si tufanye sidhani kama ni uamuzi wa busara sisi tunatakiwa tuonyeshe mfano
EMT ,
majibu mengi yapo hapa na summary yake ni kuwa kama mpira kwako ni chanzo cha fedha hakuna shida kutumia hata masaa kumi. Lakini itakuwa si busara kwa mtu anayefanya kama leisure kutumia muda wote huo badala ya kitu ambacho ni productive!
 
Last edited by a moderator:

Kama Taifa tunahitaji brains katika sayansi, technolojia, tafiti, uzalishaji na ndipo michezo itafaa. Sioni namna yoyote Tanzania itaendelea kwa anasa nizionazo kwa vijana na watu wa umri wa kati katika michezo na burudani. Internet yaweza kutumika kujifunza hata masomo/tafiti zaidi ya kuchat na kuweka mapicha facebook kama wafanyavyo watu wengi na hili ndo nalolalamikia. Hakuna namna Tanzania itaendelea bila kuweka mbele elimu itakayopelekea ukuaji wa uchumi wa uzalishaji (manufacturing economy) na hata kama burudani indirectly au directly inaweza kufeed manufacturing industries bado Tanzania haina uwezo wala uwezekano wa kuwa na saikolojia (mindset) ya kuwa na maendeleo ya michezo kwanza ambayo yataboost uchumi. Hakuna namna. Ndiyo maana hata hizo nchi tunazotaja kufaidika kimichezo zina kitu kingine mkononi kwanza (manufacturing economy), science and tech ndipo michezo ama starehe (entertainment) inakuja kuweka nguvu. Vinginevyo tutaishia kuwa wachuuzi katika nchi yetu wenyewe na mashabiki wa nchi zingine.
Me love this :)
 
EMT ,
majibu mengi yapo hapa na summary yake ni kuwa kama mpira kwako ni chanzo cha fedha hakuna shida kutumia hata masaa kumi. Lakini itakuwa si busara kwa mtu anayefanya kama leisure kutumia muda wote huo badala ya kitu ambacho ni productive!

Mie siongelei mpira tuu bali naongelea michezo kwa ujumla.

Na hapo ndipo ninapoliona tatizo.
 
Back
Top Bottom