Tanzanian Political Opposition is Not Ready Yet!

Pamoja na juhudi zetu kubwa za kuking'oa CCM, ukweli ni kuwa vyama vya Upinzani havijajiandaa vizuri kuliongoza Taifa letu.

Hili linatokana na ukweli kuwa havina watu wa kutosha ambao wanaweza kuwa Wabunge na kuendelea kwa migongano na kukosekana kwa watu wenye nguvu za kukubalika na jamii na hasa majimboni kuwa Wabunge.

Ni bahati mbaya sana Mzee Victor Kimesera mgombea uchaguzi wa CHADEMA Kiteto, yupo hoi bin taabani Dar kwa ajili ya matibabu. Wengi tumekimbilia "sumu" wengine watasema lwao. Lakini ukweli ni kuwa kama Mtoa uhai angemtwaa Malaika wake, je CHADEMA wangemsimamisha nani? Do opposition have a back up plan?

Kama sikosei, Mzee Kimesera anaweza kuwa na umri kati ya miaka 65-72. Hivyo basi CHADEMA wamekimbilia kumpa tunu hiii mtu mzee. Uzee si hoja au dhambi, bali jee hapakuwa na mtu mwingine yeyote ila Kimesera? Kumbukumbu zangu ni kuwa yeye Kimesera aligombea Kiteto 1995, hivyo miaka 12 baadaye, anaendelea kuwa mgombea pekee mwenye utashi na kukubalika kwa wananchi wa Kiteto?

Leo hii miye nimeshupalia Kikwete avunje Bunge na baraza la Mawaziri. Akifanya hivyo na kuitisha uchaguzi mkuu baada ya miezi 6 au hata mwaka mmoja, je Upinzani una watu wa kutosha wenye uwezo na ushawishi kukubalika katika majimbo? au ni kusubiri mabaki kutoka CCM?

Nilipoleta ile mada ya Chadema must Reform na Focus 2010, niligusia vitu kama hivi, je kina Mnyika, Kitila na Zitto, mko tayari kuchukua nchi nzima?

Zaidi la hofu ambalo ndili linalofikia kusababisha wananchi waendelee kuchagua CCM (Zimwi likujualo) ni ukweli kwamba hata kama Upinzani ukishika hatamu, je unauwezo kuongoza nchi? wanawatendaji wa kutosha wanao waamini kufanya kazi na kutekeleza mikakati na sera za vyama hivi vikichukua madaraka?

Si nia yangu kuviogofya au kuvunja nguvu za upinzani, ila ni ukweli usiopinguika na hali halisi! Upinzani upo tayari kimaneno, lakini kiutendaji sidhani hata kama wana uwezo japo 40%. Upinzani umejaa misuguano na kikubwa ambacho wanafahamika sana sasa hivi ni kuhusu vita vya ufisadi vya Slaa na Zitto.

Swali ni hili, ikiwa CCM kesho watajirudi na kujisafisha kuhusiana na Richmond, BOT, ATCL, RADA na IPLT, je upinzani utakuwa na hoja gani kujiuza? watakimbilia Katiba? au ndio kula ruzuku ambazo no kodi zetu?

Napenda kutoa hoja!

Rev.

Masuala uliyozungumza hapa sio makosa ya upinzani peke yake. Ni makosa ya chama tawala na wananchi kwa ujumla.

Tungeweza kuuliza je CCM hiko tayari kuachia vyama vya upinzani kuwa madarakani au kupata ushindi katika uchaguzi wa kihalali?

Mtu anashindwa uchaguzi akiwa chama cha upinzani na akijiunga na CCM anashinda kwa kura nyingi. Je CCM imemuongezea ujuzi gani au kipaji gani cha uongozi kufaa kuchaguliwa?
 
Kiteto ni mfano mzuri kwamba kumbe wananchi wakiamua upinzani unashinda. Kata zote za mjini CHADEMA ilishinda, Huko ndio wanapojua maana ya ufisadi. CCM wamecheza rafu huko vijijini ndani ndani kwa wamasai wasiojua hili wa lile kuhusu ufisadi. Wanachujua ni ng'ombe zao. Inaelekea CHADEMA wameshindwa pia kulinda vizuri kura huko remote areas. Hebu waje watueleze kwa kina hapa ilikuwaje, tazama matokeo hapa: http://www.chadema.net/uchaguzi/matokeo/kiteto/index.php

Hapa ilikuwa ni kabla ya matokeo maruhani ya asilimia 15 iliyobaki

Asha

Dada Asha,

I beg to differ. If 75% or Watanzania wanaishi vijijini are mis-informed about opposition and Ufisadi, do you blame CCM who had a department of mass mobilization for the failure of Chadema to sell itself in rural areas?

Naomba urudie makala yangu ya Chadema must reform na inabidi tuongeze wigo wa kusema kujiuza kwa Upinzani uanzie vijijini hata kama hawana pesa.

Strategy moja ingekuwa ni kuanza kidogo kidogo kwenye maeneo ambayo ni dhahiri wana nafasi ya kupata viti vya Bunge!
 
Mawazo yangu the opposition has a very long way to go and to make matters worse the road is very rough na yenye maharamia wengi na wa kila aina.

jambo muhimu wameamua wamefanya muungano, muungano huu usiwe wa mdomo na wa kwenye makaratasi tu, uwe muungano wa vitendo action speaks louder than words.

Watu wengi wanasema muungano kama huu hauwezekani reason being kila mtu yupo kujitafutia kivyake, ni wachache sana wana maslahi ya nchi hii katika akili na mioyo yao when they are aspiring for a political position. Kinachohitajika ni wanasiasa ambao wana ifeel hii nchi in thier veins and I also belive that this country has a lot of briliant people who are ready to do a lot for this nation
 
Tanzanian Political Opposition is Not Ready Yet! Sijui kama hilo ni swali au unashangaa. Nadhani ili uwezi kushinda kwenye haya mambo ya uchaguzi wa kisiasa lazima uwe na vitu viwili, mtu na something to talk about ambacho kitagusa jamii nzima. Siyo lazima uwe ni kiongozi mzuri. Kwa mawazo yangu Tanzanian Political Opposition is ready.
Sikupenda kuongelea hii issue mapema kwani bado nina kazi ya kupambana na Obama usiku na mchana. Kwa mawazo yangu, mbinu anazotumia Obama hazina tofauti na za CCM. How you can deal na jambo kama hilo, ni kuwa-educate watu kutoka kwenye mental slavery. Na jambo kubwa ambalo CCM wanafanya ni ku keep watu poor, uneducated, and ignorance wakija wakati wa uchaguzi kama wanamsukuma mlevi. Kama Obama akisema haoni tofauti ya ku-reject and denounce, you educated the people that there is a big difference. Na kama wewe mwenyewe hujui kama kuna tofauti, utawezaje kuwaondoa CCM madarakani?
Kuna mambo mengine watu wanaongea humu nadhani hata viongozi wa upinzani wakienda huko vijiji wanayasema. Kwa mfano CCM (Chama cha Majambazi) au Chama cha Mafisadi. Can you real be an agent for that na kuwaambia watu hayo mambo? Kwa mafano, ukienda Mpanda ukawaambia CCM ni chama cha mafisadi msiwachague, wananchi watangalia mwenyekiti wao wa shinda, mbunge wao, na kama hawalingani na maelezo yako watakuona wewe ni mweu tu. Ukiwaambia eti RA ni fisadi, kwanza hawamjui na hata huko Igunga hawajui RA kama fisadi wanajua kama ni mtu ambaye anawasaidia kwenye shida zao. Kwa hiyo ukienda Igunga unaweza kuwapa HOPE yakupata zaidi ya wanachopata toka kwa RA, inakuwa ngumu kwa sababu you do not have records of doing anything, you must be very good like Obama. Mara nyingi huwa sipendi kuongea hapa kwa maana watu wengi huwa hawanielewi, kama nilivyosema hapo juu "do the math".. list down mafisadi wote unaowajua ndani ya CCM halafu gawanya na idadi ya wanachama wa CCM ukipata ratio, jiulize can you carry that issue as an agenda? It might be true kuwa uchumi unaathiriwa sana na mafisadi lakini how can you prove kwa uneducated civilians? Kama unapingana na mimi chukueni hiyo a.k.a sera ya mafisadi muone kama mtashinda uchaguzi hata mmoja.
Nina mambo mengi sana ya kuongelea ila kwa muda muafaka huko mbeleni naona kuna watu wameshatumwa humu ndani.
 
Refer my post kuhusu upinzani na kiteto.
Rev umegusa center point. Nilisema ya kwamba upinzani wanatumia 1960s strategy in 2008. Upinzani hawa leaders wa kutosha na hawafanyi juhudi zozote kurecrute new leaders. Mfano angalia John Mnyika is young, energetic and intelligent. He will grow inside politics, and that will make him strong politician. But the question is how many John Mnyika au Zitto kind of politician in Upinzani?

Sasa upinzani wamejaza wazee, ambao wako katika deminish point. So far najua upinzani hawana tactic zozote za kurecrute new leaders,majority ya watanzania doesnt know anything about Upinzani. Nilisema kutumia helcopter sio njia, kusimama majukwaani na kusema JK mwizi sio njia.

Upinzani need to focus on long term plan, kwanza fight on the grassroot. Mpango wa kuchukua muuza machungwa mkamgombanishia kiti ili awe mbunge, ni strategy ninayoita loosing strategy.

Rev. Kuna mengi ya kufanyika na nadhani ni bora zaidi kuanzisha chama kimoja kipya kuliko kuvibadili vyama vingi feki.Ushauri wangu ni baadhi ya wasomi walio nje na ndani ya nchi kukutana pamoja kisha kuanzisha new party or something. Lakini Upinzani will never take us anywhere. CCM inakwenda mtoni i wish upinzani wangejua hilo, lakini i guess njaa ndio tatizo.
 
Mawazo yangu the opposition has a very long way to go and to make matters worse the road is very rough na yenye maharamia wengi na wa kila aina.

jambo muhimu wameamua wamefanya muungano, muungano huu usiwe wa mdomo na wa kwenye makaratasi tu, uwe muungano wa vitendo action speaks louder than words.

Watu wengi wanasema muungano kama huu hauwezekani reason being kila mtu yupo kujitafutia kivyake, ni wachache sana wana maslahi ya nchi hii katika akili na mioyo yao when they are aspiring for a political position. Kinachohitajika ni wanasiasa ambao wana ifeel hii nchi in thier veins and I also belive that this country has a lot of briliant people who are ready to do a lot for this nation
Unazungumzia muungano gani? Muungano unao make sense ni ule ambao mnasema tukichukua kura zetu tukaziweka pamoja tutashinda. Kwa sasa unaweza ukaunganisha vyama vyote na CCM wakaamua kuwapa 10% ya kura zao na bado vyama vya upinzani vikashindwa. Wanahitaji something to talk about hata kama ni uongo kama wa Obama.
 
Refer my post kuhusu upinzani na kiteto.
Rev umegusa center point. Nilisema ya kwamba upinzani wanatumia 1960s strategy in 2008. Upinzani hawa leaders wa kutosha na hawafanyi juhudi zozote kurecrute new leaders. Mfano angalia John Mnyika is young, energetic and intelligent. He will grow inside politics, and that will make him strong politician. But the question is how many John Mnyika au Zitto kind of politician in Upinzani?

Sasa upinzani wamejaza wazee, ambao wako katika deminish point. So far najua upinzani hawana tactic zozote za kurecrute new leaders,majority ya watanzania doesnt know anything about Upinzani. Nilisema kutumia helcopter sio njia, kusimama majukwaani na kusema JK mwizi sio njia.

Upinzani need to focus on long term plan, kwanza fight on the grassroot. Mpango wa kuchukua muuza machungwa mkamgombanishia kiti ili awe mbunge, ni strategy ninayoita loosing strategy.

Rev. Kuna mengi ya kufanyika na nadhani ni bora zaidi kuanzisha chama kimoja kipya kuliko kuvibadili vyama vingi feki.Ushauri wangu ni baadhi ya wasomi walio nje na ndani ya nchi kukutana pamoja kisha kuanzisha new party or something. Lakini Upinzani will never take us anywhere. CCM inakwenda mtoni i wish upinzani wangejua hilo, lakini i guess njaa ndio tatizo.
Ahsante,
Umeongelea mambo mawili ambayo ndiyo ninavyofikiria mimi, watu na agenda. That's it.
 
Sasa hapa Mnyika alikuja hapa akawasihi wenye interest na upinzani wawasiliane nae- sasa hata JF hakuna aliyemjibu!

We stay 'there' na kusema 'wale dhaifu'- sasa kama sii mimi na wewe ni nani ataimarisha upinzani?

Watz tunapenda chakula kilichoiva tu- yaani tupakue na kula!

Ila kulaumu- ni wa kwanza!

Mzalendohalisi. I see where you coming from, however people doesn't join Upinzani for the reason of hating CCM. Watu kwanza wanatazama Policy za upinzani, Upinzania wana weak policy on everything. Most viongozi wa Upinzani wapo pale kwa purpose ya kazi na sio kuchallange uongozi wa CCM, wengine wana join sababu ya dhiki zao za maisha. So, its not about kujiunga, it is about their policy and tactic za uchaguzi

Kingine, walio madarakani kwenye Upinzani wapo kwa muda gani? 15 yrs or more. Why? Sababu ndio waanzilishi and they believe kwamba they own it. Mfano Cheyo alikwenda mahakamani kufight nafasi yake ya uchairman. Sasa why bother kujiunga na upinzani hewa?

Ndio maana nikasema the better way ni kuanzisha chakwetu kipya, Jambo movement part (JMP)
 
Now people are talking. Siku Leo Lwekamwa alipoisigina katiba ya Tanzania alionekana mwendawazimu, lakini waliokuwa wanajua yaliyomo ndani ya katiba na wenye akili, hawakumwona mwenda wazimu. No doubt Katiba inatakiwa kuwa ya watanzania wote, lakini sasa hivi katika si ya watanzania wote, kama nikipanga wadau wa katiba hiyo kutoka juu naona walala hoi wako chini kabisa wanaonufaika kwanza kabisa Serikali(mihimili yote mitatu), CCM, vyama vya siasa...............sisi ni wa mwisho kabisa. That is how the britons wanted it to be in order that the colonies can be smoothly colonised. Katiba yetu ilikuja kutoka Lacanster na Msekwa akawekaweka viraka.
As to opposition, watanzania wako tayari, mazingira yameiva lakini katiba bado hairuhusu, na opposition bado hawajawa na better strategies za kubadilisha katiba. There is still enough room for opposition to play so as to change the constitution, sasa hivi wakisema haiwezekani tutakuwa tunadanganyana tu, kuna wanasheria wazuri tu upinzani na Tanzania ambao wanaweza kuweka case ndani na nje ya Tanzania na katiba inaweza kubadilishwa.
Katiba ya sasa ni mbaya, lakini ubaya wake tutauona zaidi kama opposition wakiingia madarakanni na kuitumia. Tungeshika adabu kama Mrema au Lowassa wangekuwa rais kwa kutumia katiba hiyo. Sasa hivi ni kudra ya mungu tu ndio ina tulinda.
 
Now that Richmond is kind of off the shelves and BOT-EPA is doing so so, what is opposition doing during this vacuum of scandals and vita vya ufisadi?

It is amazing that the main theme on Mkutano wa Wanawake wa Chadema, the focus was to wail about Chenge, Lowassa and ufisadi and nothing else that can be of value to Mwanamke or Taifa!

Has opposition run out of policies and the only thing they can capitalize on to sell themselves is Ufisadi?

Je hivi ndivyo walivyo?
 
Kulikuwa na watoa mada zaidi ya watano. Huyo mmoja tu ndio alizungumza kuhusu ufisadi. Wapo waliozungumza masuala ambayo unasema wangezungumza. Wapo waliozungumza mpaka ukombozi wa mwanamke kiuchumi na ndipo ilipofanyika harambee ndogo iliyokusanya milioni kumi kwa ajili ya wakina mama walioko kwenye maisha duni.

Kuna mwanamke yoyote aliyekuwepo atupe mada zingine zilizotolewa?

Mi nilifanikiwa kupata hiyo moja
 
Hata media coverage ya mkutano wenu unaonyesha hoja kubwa ilikuwa ni ufisadi. Wewe, Kitila, Zitto na Mnyika kubalini kuwa sasa hivi hamna cha kutuuzia Watanzania mpaka skendo lingine liamke!

And that is why people do not take you serious as a party of group (opposition) that looks into leading Tanzania.

You will have several shining stars, people who can stand by themselves but when you create a combination so called Upinzani, it is a joke, sorry to be blunt about it!
 
Rev Kishoka
Mara nyingi nakusoma maoni yako na nayaheshimu,kuhusu hili nafikiri umepitiwa kidogo.Kuuza policies kuna mda wake na hili la ufisadi sasa hivi ndio topic inayoongolewa vijijini. Last week nilikuwa kyela nimekwenda vijiji 3 tofauti katika tarafa 2 tofauti ambazo ni unyakyusa na ntebela, hoja za wanavijiji hivyo ni kero ya michango inavyohusishwa na ufisadi unaosababisha serikali kukosa uwezo wa kutoa huduma za msingi.

Vilevile hujazuiwa wewe kuingia kwenye siasa aidha kwa wewe kuanzisha chama ambacho kina sera zilizo bora zaidi au kuwania uongozi kwenye chama unachoona kinakufaa na kukidhi matarajio yako badala ya kujikita kukatisha tamaa kwa wenzako ambao wamejitolea kuwania uongozi.
 
Kumbuka wakati wanawake wenyewe wanaeleza kuhusu Kongamano waliweka bayana kuwa mambo mengi zaidi yangefanyika zaidi ya masuala ya ufisadi tu: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/7/habari3.php

Unasema upinzani hawana ajenda, mbona ziko hapa! Sera za CHADEMA http://www.chadema.net/nyaraka/index.php

Walizungumza pia kuhusu BAWACHA http://www.chadema.net/mabaraza/bawacha/index.php

Tatizo hapa si Wanawake wa CHADEMA hakuwa na ajenda; suala ni waaandishi wa habari tu wenyewe ambao waliona cha muhimu zaidi ni Kauli ya Mbowe kuhusu ufisadi. Hata mambo mengine ambayo Mbowe aliyazungumza kuhusu jinsia na nafasi ya wanawake katika maendeleo ya taifa hawayakuandika.

Ndio maana nikasema hapa wanawake wengine waliokuwepo watueleze yaliyojitokeza.

Najua katika kongamano hilo sera za CHADEMA kuhusu masuala ya wanawake na jinsia zilijadiliwa.

Asha
 
Rev Kishoka,
Rai yangu kwa wenzetu mlioko nje ya Tz muanze sasa kuwa active na affairs za nchi yetu.Hiyo kazi msiwaachie wapinzani pekee yao, nyie mnaweza kushiriki hata kwa kusupport ngos za kitanzania kufundisha uraia ili watu wajikomboe kifikra waijue nguvu ya karatasi za kura na haki zao za kiraia. Hii kazi inahitaji moyo wa kujitolea na ndio maana mimi nawaunga mkono viongozi wa upinzani waliojitokeza hadi sasa wanatoa mchango mzuri.
Nashukuru mwanakijiji tayari anatoa mchango mkubwa wa mawazo kupitia makala zake mbalimbali.Hata kenya mnayoiona ina mwamko mkubwa wakenya wenzao walioko huko nje wameshiriki kikamilifu kwenye mageuzi makubwa tunayoyaona sasa.Tusibezane tushikamane kuinua uelewa wa wapiga kura wetu. Mimi binafsi kila nikipata mwanya wa kuongea na wanavijiji najitahidi nitoe kilicho kichwani mwangu kuelemisha ninapopata mwanya.
 
ili la kubadilisha katiba ili iendane na mfumo wa vyama vingi mi nadhani ni la muhimu sana katika kuleta upinzani wenye nguvu, ila mh kitila anakwepa kuliongelea hili, lets face it, hata kungekuwa na kina zitto milioni moja chadema, kwa katiba hii hatuendi popote, and ccm knows that, tunao vijana wengi shupavu, wasomi wenye moyo na taifa hili sema we hujui sababu hujafanya research, nadhani chadema wana vision nzuri lakini inakwamishwa na mfumo tata wa katiba yetu, na siamini kama kufichua ufisadi ndo kunaiweka chadema kwenye siasa, inabidi tupanue wigo wetu wa kufikiri zaidi ya hapa.
 
Rev Kishoka
Mara nyingi nakusoma maoni yako na nayaheshimu,kuhusu hili nafikiri umepitiwa kidogo.Kuuza policies kuna mda wake na hili la ufisadi sasa hivi ndio topic inayoongolewa vijijini. Last week nilikuwa kyela nimekwenda vijiji 3 tofauti katika tarafa 2 tofauti ambazo ni unyakyusa na ntebela, hoja za wanavijiji hivyo ni kero ya michango inavyohusishwa na ufisadi unaosababisha serikali kukosa uwezo wa kutoa huduma za msingi.

Vilevile hujazuiwa wewe kuingia kwenye siasa aidha kwa wewe kuanzisha chama ambacho kina sera zilizo bora zaidi au kuwania uongozi kwenye chama unachoona kinakufaa na kukidhi matarajio yako badala ya kujikita kukatisha tamaa kwa wenzako ambao wamejitolea kuwania uongozi.

Nsaji,

Kwanza nashukuru kwa kuwa msomaji mzuri na hata kuyachambua maoni yangu. Pili ni haki yako kutofautiana nami kuhusiana na ninayodai kuwa yafanyike ili upinzani ujiuze na kukomaa.

Sina nia ya kuwa mwanasiasa kwa kuanzisha chama au kuwa mwanachama wa chama fulani na nafikiri umebaini hivyo kwa kuwa siku zote nimeweka mbele utaifa wangu na kubainisha mambo ambayo ni muhimu yafanyike kwa Taifa na hata kuhoji vyama vyote, kilicho madarakani CCM na vya upinzani kuwa wao lengo lao ni nini.

Ndiyo, ni kweli wimbo ulio bora sasa hivi ni "ufisadi". Lakini mnachoshindwa kukiona ni hili, 2010 iko jirani na Upinzani haujaweza kushika hata robo ya Bunge letu na kuna kila dalili kuwa yaliyotokea 2005, ukiachia mambo ya rushwa na nguvu za CCM, CCM watachaguliwa kwa kishindo tena na wapinzani watarudi kulalamika.

Mimi ninahamasisha 9rejea hoja zangu a Focus 2010 na Chadema must reform) kuwa Vyama vya siasa ni shurti vijiuze kisera kwa kuhakikisha upanzi wa mbegu unaanzia kwenye vijiji, nyumba kumi, kata, tarafa, wilaya, mkoa na mwishowe taifa.

Ama upinzani unahitaji uwe 'selective" katika kazi zake na kuangali a ni vipi wanaweza kujijenga kisera na utendaji na kupata ufuasi wa kweli siku ya kupiga kura na sui kujazana kwenye mikutano halafu zikija pilau za CCM, wapiga kura hugeuka na kuipigia kura CCM tena.

Asha kaniambia niende kwenye website yao nijue Chadema, kwa nini anipe kazi hiyop ya kwenda kubonyeza website na kuanza kusoma sera? same thinking is being applied by Mtanzania na hasa aliye vijijini.

TANU ilimng'oa mkoloni kwa kusema tunataka Uhuru kujitawala. CCM ikashamiri kwa kuhakikisha kuwa kuanzia ngazi za vijijini, mashuleni na kokote kule somo na tukuzo kuhusu CCM linafanikiwa.

Sasa Upinzani leo unasema kazi yao kubwa ni kuing'oa CCM, lakini hawana wanachosema watafanya kumuonyesha Mtanzania kuwa wao ni bora kuliko CCM.

Upinzani ni dhaifu na unaonekana kuwa ni mkondo mwingine wa watu kujipatia riziki kama walishindwa kuzipata riziki hizi kupitia CCM na Ufisadi. Utitiri wa vyama vya Upinzani ambavyo vingi havina hata ushirikiano na kuishia kuhujumiana na kufanya mambo kama CCM ndiko kunakofanya CCM ionekane kuwa ni mashujaa wa milele kwa Mtanzania.

Hebu fikiria hata kama ni rushwa au takrima, ilikuwaje Lowassa ambaye amefikia kuliletea Taifa letu hasara kubwa kwa kuingia mkataba bomu na kuzorotesha uzalishaji mali kutokana na kuchelewa kwa kupatikana kwa umeme wa ziada, leo anapokelewa kwa vifijo na nderemo?

Inakuwaje leo wananchi wanashangilia kwa dhati Kikwete kubadili mawaziri badala ya kumzomea na kmhoji kwa nini aliendekeza viongozi wabovu? Kwa nini wananchi tunakuwa wagumu kudai uwajibikaji katika ngazi zote za kiutendaji za serikali kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa uwajibikaji unafanyika mara moja?

Vyama vingi vimeanza tangu 1992, huu ni mwaka wa 15 tangu mfumo huu uanze, lakini upinzani unapata shida kubadilisha mawazo ya Watanzania. Anzia chaguzi za Serikali za mitaa, njoo uwakilishi wa majimbo hata Urais.

Kama Upinzani ungelenga kubenjua na kupata minimum ya 35% ya kura za udiwani, ubunge na hata uraisi, hivyo kuhakikisha kuwa 35% ya uwakilishi wa Udiwani na Ubunge uko mikononi mwa Upinzani (if they can get more than 35% representation or votes that will be great, but they need to set a minimum goal which can be achieved easily), basi safari ya mageuzi ityakuwa inaonekana kuwa ina maana na si viini macho!

Mfano mdogo kuhitimisha, nilipoleta mada ya Chadema must reform, nilikuwa naleta msukumo wa kujenga chama ambacho hakifanani na CCM katika mfumo mzima wa kiutendaji na kisera. Ukiangalia kwa dhati, mfumo wa Chadema, CUF, TLP, UDP, NCCR na vyama vingine vyote ni 100% mfumo wa kuundwa na uendeshaji wa CCM.

Sasa ni vipi watu wataona tofauti ikiwa mifumo yote inafanana na matatizo ya kugombea uongozi au migongano inafanana na ya CCM na kibaya zaidi ni kuwa vyoama vyagombea ruzuku kati ya viongozi wao?

Opposition needs to come with something new to sell themselves to win reasonable seats on local government and parliamentary elections. Waiting for anothe ufisadi story however relevant may be is not helping! we have an evidence;- KITETO
 
Nsaji,

Asha kaniambia niende kwenye website yao nijue Chadema, kwa nini anipe kazi hiyop ya kwenda kubonyeza website na kuanza kusoma sera? same thinking is being applied by Mtanzania na hasa aliye vijijini.

TANU ilimng'oa mkoloni kwa kusema tunataka Uhuru kujitawala. CCM ikashamiri kwa kuhakikisha kuwa kuanzia ngazi za vijijini, mashuleni na kokote kule somo na tukuzo kuhusu CCM linafanikiwa.

Sasa Upinzani leo unasema kazi yao kubwa ni kuing'oa CCM, lakini hawana wanachosema watafanya kumuonyesha Mtanzania kuwa wao ni bora kuliko CCM.

Upinzani ni dhaifu na unaonekana kuwa ni mkondo mwingine wa watu kujipatia riziki kama walishindwa kuzipata riziki hizi kupitia CCM na Ufisadi. Utitiri wa vyama vya Upinzani ambavyo vingi havina hata ushirikiano na kuishia kuhujumiana na kufanya mambo kama CCM ndiko kunakofanya CCM ionekane kuwa ni mashujaa wa milele kwa Mtanzania.

Vyama vingi vimeanza tangu 1992, huu ni mwaka wa 15 tangu mfumo huu uanze, lakini upinzani unapata shida kubadilisha mawazo ya Watanzania. Anzia chaguzi za Serikali za mitaa, njoo uwakilishi wa majimbo hata Urais.

Mfano mdogo kuhitimisha, nilipoleta mada ya Chadema must reform, nilikuwa naleta msukumo wa kujenga chama ambacho hakifanani na CCM katika mfumo mzima wa kiutendaji na kisera. Ukiangalia kwa dhati, mfumo wa Chadema, CUF, TLP, UDP, NCCR na vyama vingine vyote ni 100% mfumo wa kuundwa na uendeshaji wa CCM.

Sasa ni vipi watu wataona tofauti ikiwa mifumo yote inafanana na matatizo ya kugombea uongozi au migongano inafanana na ya CCM na kibaya zaidi ni kuwa vyoama vyagombea ruzuku kati ya viongozi wao?

Opposition needs to come with something new to sell themselves to win reasonable seats on local government and parliamentary elections. Waiting for anothe ufisadi story however relevant may be is not helping! we have an evidence;- KITETO

We kweli kishoka!

Sasa ulitaka nisikuonyeshe sera za kwenye mtandao kwani we upo kijijini hapa? Si uko mtandaoni!

Walioko vijijini wanapata vitabu vya sera, wewe uko hapa hebu acha uvivu, soma hizo sera kwanza kabla ya kusema upinzani hauna sera.

Kama umesoma na bado unasema upinzani uko sawa na CCM chama cha Mafisadi basi kweli we ni kishoka, unasahau.

Wapinzani wanatafuta rizki gani wakati ruzuku yao ni kidogo kupindukia? Labda hiyo CCM inayojichotea bilioni 2 kila mwezi za walipa kodi kulipa makada wake

Wakati CCM inapata zaidi ya milioni 2000 kila mwezi; CHADEMA inapata milioni 56 kwa mwezi!

Asha
 
Hivi kwa nini tusianze mass action ili kudemand katiba mpya au mabadiliko ya katiba? Tuanzishe vuguvugu kubwa kwani kama hawataki kusiklixza kwa maneno then lazima watakua tayari kwa kutumia movements
 
Back
Top Bottom