Tanzanian Olympians

BiMkubwa

JF-Expert Member
Jan 9, 2007
529
97
Msaada tafadhali waTanzania,

Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa Olympics ila kuna jambo linanitatiza hapa. Leo ni siku ya nne tokea mashindano ya swimming yalianza kufanyika. Sijui ni wangapi wana taarifa kuwa tumepeleka watanzania wawili kwenda kushindana katika kipengele hiki cha mashindano haya.
Katika ujuzi wangu mdogo wa computer, nime-search, google, you name it, kutafuta taarifa za watanzania hawa. Yaani details za heats, na waliweza kufikia level gani licha ya kwamba siwategemei kufurukuta mbele ya Michael Phelps. Ila angalau taarifa zao tuzipate ili tujue whats happening.

Kwa mwenye taarifa atueleze jamani. Au ndio walienda kutimiza wajibu? Nina doubt kama walikuwa na any olympic times katika dossier zao. I just need to know.
 
Bi Mkubwa, tumepeleka waogeleaji wawili mwanaume na mwanamke. Kuna mmoja anaanza mashindano leo alhamisi (kwa kwetu Bongo) na mwingine siku ya Ijumaa, lakini sijui wanashiriki katika mashindano gani ya kuogelea. Hawa viongozi waliktakiwa watoe details za hao wanamichezo 10 kama ni wakimbiaji, waogeleaji na mabondia wanashiriki katika mashindano yapi ya kuogelea, kukimbia masafa gani na ngumi za uzito upi, labda hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo.
 
Nimewatafuta katika heats zote na hawaonekani! Wala hatujaambiwa wanaogelea umbali gani au mtindo gani? Wao ni waogeleaji tu, period. Ingawa matumaini ni madogo basi angalau tungeonyesha seriousness tunapotoa habari zao(kutokujua specialization yao ni disrespectful)!
 
Bi Mkubwa, tumepeleka waogeleaji wawili mwanaume na mwanamke. Kuna mmoja anaanza mashindano leo alhamisi (kwa kwetu Bongo) na mwingine siku ya Ijumaa, lakini sijui wanashiriki katika mashindano gani ya kuogelea. Hawa viongozi waliktakiwa watoe details za hao wanamichezo 10 kama ni wakimbiaji, waogeleaji na mabondia wanashiriki katika mashindano yapi ya kuogelea, kukimbia masafa gani na ngumi za uzito upi, labda hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo.

Kuna waogeleaji na wakimbiaji, hakuna mabondia kwasababu ya scadal ya madawa.
Nimeweka summary nzuri hapa::)
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=16764
 
Msijali sana kutokana na matokeo ya michezo, kwani habari zilizopatikana ni kuwa vijana wetu wanaendelea vyema na ile kazi muhimu iliyowapeleka huko ya kusukuma kete! Ala!
 
Mwanaume Ameshidwa Kwenye Mchepuo Wa Kwanza Alikuwa Hana Viwango Mta Mia Wanogelea Kwa Sec 7 Yeye Kumi Na Kenda, Os Yuko Out
 
Msijali sana kutokana na matokeo ya michezo, kwani habari zilizopatikana ni kuwa vijana wetu wanaendelea vyema na ile kazi muhimu iliyowapeleka huko ya kusukuma kete! Ala!

China ukitiwa hatiani kwa kazi hii ni EXECUTION
 
China ukitiwa hatiani kwa kazi hii ni EXECUTION

Mbona Masanja yupo jela? ila ni vibaya sana katika michezo kuingiza biashara hii ya kuhuni. Ukifuatilia viongozi wengi katika sekta ya michezo. Namkumbuka Bw. Gulamali (Yanga), Masanja (Simba), ... Mabondia wetu huko Mauritius nk nk
 
Back
Top Bottom