'Tanzanian of Asian origin' ndio kabila gani hilo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Tanzanian of Asian origin' ndio kabila gani hilo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KyelaBoy, Apr 7, 2009.

 1. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2009
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu hapa Tanzania kuna ubaguzi wa rangi unaoendeshwa na hawa ndugu zetu wahindi.

  Kwa wasomaji kuna vijarida vya matangazo vinavyotolewa bure kwenye sehemu za kazi jamaa zetu hawa kwa makusudi kabisa wanapo post matangazo yakuomba kazi hujitambulisha kama mtanzania mwenye asili ya kiasia hii maanake nini kwa maana sijawahi kuona mtu akijitangaza kuwa mtanzania kutoka mbeya au bukoba anaomba kazi ,hii inakera na huu ni ubaguzi wa rangi,pia utakuta tangazo la kazi linadai mtu ajue gujarati,hivi kweli Gujarati ni lugha inayotumika kwa kazi hapa Tanzania.

  Na cha kuhuzunisha zaidi ni pale unapoenda hospitali ya Agakhan Hospital na Shabani Robert secondary school kwenye form zao kuna sehemu ya RACE unatakiwe uijaze ,huu nao ni ubaguzi .

  kinachoshangaza ni kuwa haya mambo yanafanyika ilihali vyombo vya dola vipo na havifanyi lolote je Wizara ya Afya ina maana haijui na pia vipi Wizara ya Elimu?

  Huu ni ubaguzi wa hali ya juu,kwa Mswahili akisema tu anataka upendeleo kwa watu weusi inakuwa nongwa lakini wahindi wao wanapojitofautisha hakuna kelele,Watanzania tuamuke,
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  nachangia kwenye hiki kipengere cha kujaza fomu.Unajua mkuu, kwa siku hizi kuna kitu kinaangaliwa nacho ni diversity - kujua race, sex, religion, hata umri na kabila.Hii yote ni kujua ni watu wa aina gani wanatumia huduma husika na kama kuna haja ya kutumia mbinu za ziada kujua kwanini watu fulani tu ndiyo wanatumia na je nini kifanyike kuhakikisha wengine nao wanatumia.

  Kuhusu hayo mengine ya wahindi kwa kweli sina comment maana nimeona hata nchi nyingine hasa za Uarabuni wakitaka watu wa dini au kabila/descendancy fulani. Labda wana sababu zao. Hata mimi kwa shughuli zangu naweza kuhitaji mtu mwenye sifa fulani ambazo ukiona utaita za kibaguzi.
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi kati ya neno WAHINDI na WATANZANIA WENYE ASILI YA KIASIA lipi ni bora kwako?

  omarilyas
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Sifa (qualifications) na "Race" ni vitu viwili tofauti. Kama unahitaji kwa mfano web master kuna haja gani ya kusema awe Mhindi au Mwarabu? Huu ni ubaguzi full stop. Usijaribu kufanya spining hapa. Ni ukweli usiopingika kuwa hawa Wahindi-Watanzania wenzetu hawataki ku-intergrate na sisi weusi.
   
 5. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Swali lako ni kama mtu aliyeuliza "Ugali na chakula ni kipi bora kwako?"
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli wanajitambulisha kama Tanzanian of Asian ORIGINAL? Nauliza tu!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  nadhani umeona my main point - Nadhani kama umeahi kufanya research utajua kuwa kuna important au vital statistic which needs to be captured.Ndiyo nikasema in order to have an outlook on diversity utaona kuna taarifa fulani zinaweza kuhitajika. Hiyo nyingine ULIYO UNDERLINE ni by the way to and was by no means meant to insinuate anything much less kushabikia ubaguzi.What is spinning here au labda sijui maana ya spining unifahamishe?
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi ungependa wafanye nini ndio uone kuwa wame-integrate na nyinyi weusi?

  Hivi kuna sheria inayomkataza mtu kutaja kabila lake au asili yake anapoomba kazi?

  Utamziuiaje mwajiri BINAFSI kuajiri mtu amtakae wakati ni yeye ndiye atakayeemlipa na ndiye anaelewa ni mtu wa aina gani ndiye atakayemfaa? Kama sisi wamatumbi, ambao ndiyo wengi, tunashindwa nini kususia biashara na huduma zote zinazotolewa kwa misingi ya kutubagua? Au kwa nini tusianzishe huduma au biashara shindani zisizobagua na hivyo kuwavuta wamatumbi wenzetu?

  Amandla.......
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Anachozungumzia WoS ni kwamba kuna wakati inatakiwa kujua athari za magonjwa fulani kwa watu wa race fulani. Kwa mfano inajulikana kuwa watu weusi wanasumbuliwa zaidi na Sickle Cell Anemia. Hii bila shaka ilijulikana kutokana na takwimu zilizoweka wazi "race" za watu wanaoumwa huo ugonjwa. Ukijua hiki ni rahisi zaidi na kufuatilia kuona kama kuna sababu za kipekee ( diet etc.) zinazofanya kundi hilo lisumbuliwe zaidi. Si spinning bali ni hali halisi. Ingawa mimi nina wasiwasi kama sababu hii ndiyo hasa inayowafanya watu wa Aga Khan kuchukua takwimu lakini haiondoi uhalali wake.

  Amandla.......
   
 10. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #10
  Apr 7, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira (Tanzania Employment Act) ni kinyume cha sheria kumbagua mtu yeyote wakati wa kumuajiri kwa kumtaka awe wa kabila, dini, itikadi ya kisiasa au uraia/asili ya nchi yeyote ile! Unaweza kuwashtaki hao wanaotaka Mtanzania mwenye asili ya Kiasia, kwani huo ni ubaguzi, na Tanzania hakuna ubaguzi!
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sawa,Mkuu.

  Lakini utawashtaki vipi wakati wao hawakusema wanataka mtu wa kabila,dini,itikadi ya siasa au uraia/asili ya nchi yeyote bali wamesema wanataka mtu anayejua kigurati? Kama mmatumbi, mzungu au mtu yeyote yule akisema anaijua lugha hiyo, wao watamuajiri. Sababu za kufanya hivi zinaweza kuwa nyingi tu. Kama duka bidhaa zake kubwa ni Saree na Salwar Kamiz basi lazima wateja wake wengi watatoka bara Asia. Hawa si lazima wote wazungumze kiswahili fasaha maana wengine inawezekana wanafanya kazi katika balozi zao, mashirika ya kimataifa au wameolewa na watu wanaofanya kazi huko! Mfanyabiashara makini atatafuta watu wakaoweza kuwabembeleza wanunue bidhaa zake. Kwa mmatumbi anayetaka kuuza Sari basi itambidi ajifunze kigujarati. Sasa kama baada ya kuijua hiyo lugha na kutimiza masharti yote akajikuta bado kazi hapati bila sababu za msingi itakuwa haki kufikiria kuwa rangi yake, kabila lake au asili yake ndiyo imekuwa kikwazo. Huo utakuwa ni ubaguzi. Lakini si huu wa kudai lugha!

  Kwani mtu akisema anahitajika mtu anayejua kifaransa nae tutamshitaki kuwa anataka watu wa Afrika Magharibi tu kwa hiyo ni mbaguzi?

  Amandla.....
   
 12. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijui kati yao nasi nani amemuathiri mwenziwe lakini na sisi huwaita hivyo mara nyingi hasa kwenye matukio.
   
 13. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mku ungeongeza hivi "Isipokuwa katika nafasi ya Urais" ungekuwa karibu na ukweli.
   
 14. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2009
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Ubaguzi wa hawa jamaa unakwenda mbali mno. Wanapalilia toka kwenye roots; mfano utaona hapa Dar kuna 'DAR ES SALAAM INDIAN SCHOOL', shule hii watoto wetu hawasomi. Kwenye shule hii kuna mitaala gani tofauti na Forodhani au Bunge?
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  wewe dar es salaam indian school wanasoma watu wote wewe mpeleke mtoto wako kama anaongea kihindi
   
 16. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #16
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Obama aliposhinda Urais mlishangilia kuwa Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika kashinda, wahindi wakidani hivyo kuna ubaya gani? wacha wajinadi ili iwe rahi sisi kuwatambua hawa waTanzania WENZETU wenye asili ya KIASIA.
   
 17. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Very good debate na ninadhani inagusia sehemu mbili muhimu:

  -Ancestry- kwani mtu akiwa ni chotara wa kihindi, kiarabu au kizungu, lazima Mtanzania mweusi atamwuliza we asili yako ni wapi? Na atataja. Obama ni chotara na tulifurahi kuona mtu mwenye asili ya kiafrika (siyo African American bali African descendant) anachukua nafasi ya urais. Sasa kwa wenzetu wanachodai ni kuwa wao ni Wantanzania kwanza na pili wana asili ya Kihindi. Kuna ubaya gani hapo? Tena mi ndo nafurahi wakitumia neno hili kwani wamejiweka watanzania kwanza.

  - Ajira na ubaguzi: nadhani katika tangazo kuandika wanahitaji mtu anayeongea kigujarati they are actually walking a very fine line. Kwa kutumia mfano wa Fundi, wanaweza kujustify kwa nini wameweka sharti hilo, kwani hata ukitaka kazi katika Arusha tribunal ya Rwanda wanatangaza kuwa lazima uongee Kifaransa. Lakini mwajiri atakaposhindwa kujustify basi tunaweza ku-petition, lakini nadhani ni kitu kigumu.

  Mi nadhani kama wamekuwa wagumu ku-intergrate kama unavyodai, basi ni vyema kuwaacha na kuona kama watafika mbali kwani asilimia kubwa ya Watanzania ni weusi. Lakini mi sidhani kama tunaweza ku-generalize kuwa hawataki kuintegrate, wapo wasiotaka, wapo wanaotaka, kama vile wapo wazee wetu ambao hawataki mtoto wao aoe au aolewe nje ya kabila lao. No difference at all, hata tukibaguana weusi kwa weusi.

  Kumalizia tu - kuhusu suala la Indian School, kwani International school au French School hamuisemi? Hakuna tofauti, wote wanafundisha kwa kufuata mitaala wanayoitaka na kwa masharti wanayoitaka wao. Hapo French school, usipojua kifaransa mtoto hawezi kujiunga.

  Tuache kulilia ubaguzi kila wakati.
   
 18. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa;kwasababu katika suala la kazi ni sifa(qualifications) za mtu kwa mujibu wa aina ya kazi yenyewe na hakuna room ya wewe dini gani,ethnic group.
   
 19. L

  LaVerite Member

  #19
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Usidhani hatujui jinsi surveys zinavyofanywa na statistics zinavyochukuliwa. Unachukuaje statistics za 'race' kwenye tangazo la kazi linalosema muombaji awe anaongea 'gujarati' au awe Tanzanian of Asian origin? Wahindi wanajisikia 'superior' na hawataki ku-intergrate na sisi hilo liko wazi.
   
 20. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanakijiji!
  Hii thread imetoka wapi? Huko mnakotupeleka ndiko siko na mimi simo ''bora mimi sijasema'' Mwanahaki nakuomba acha porojo! Ubaguzi hapa TANZANIA upo tena ni wa ajabu? Wachache kuwabagua wengi na bado wanapeta. Hakuna watu wabaguzi duniani kama wahindi(Indians). Ukiachilia mbali wale waliolazimishwa kuolewa na wamatumbi huko Unguja mpaka wakaamua kumwua KARUME miaka 35 iliyopita!

  Hakuna aliyeolewa na kama yupo ujue ni koko na jamii imemtenga. He/she is an outright outcast and of the lowest cast. Kama wenyewe kwa wenyewe wanabaguana kichizi sembuse nyie Nyani/Kima!! Kama kuna mwenye kubisha ametumwa kama kawaida kwa kupewa Chauro na mavi ya watoto.

  Kule Uganda wanajua alichowafanyIa yule General/Field Marshal Id Amin Dada 1972 . Mpaka leo hii imewaletea Ugandans heshima na utu wao walirudishiwa heshima kwa kwenda mbele!!!

  They have corrupted CCM period!!!! Haiwezekani mtu akawa na uraia wa India,Uingereza, Canada na Tanzania and then mnaleta za kuleta.

  Nimekua na kusoma na wahindi mpaka Europe na USA HAWA watu wanastahili aliyowafanyia Idd Amin. 1967 Nyerere kataifisha mali zao Ruksa kawarudishia matatizo yameanzia hapo!!!! Maumivu ya kichwa yanaanza taaratibu!!!! Kufanya kosa si kosa!!! Kosa kurudia kosa!!

  These bastards are doing capital flight mchana kweupee!!! kwa kwenda mbele BOT under Ben Ndullu and the corrupted CCM - bandits are just smiling na nyie mnasema 2004 Employment and Labour Relations Act inakataza ubaguzi!!!!KILA SIKU IN THE PAPERS KWENYE MATANGAZO YA AJIRA WANATAJA UMRI NA UZOEFU HUO SIO UBAGUZI NA SHERIA HIYO HAYO SI IMEKATAZA ehhee!!

  Go to hell!! Because your father told me a lie in the month of july with a single pie!!!!!! Wajameni !!!!!
   
Loading...