TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

Sidhani kama hao ni majambazi. Hicho ni kikosi maalum ambacho kimetumwa kufanya hiyo kazi. Majambazi wengi huwa hawaui moja kwa moja kwanza hutishia na kuona kuwa unafuata masharti yao, huu ni mpango kabambe ambao umefanyika kutokana na misukosuko ya kisiasa nchini Tanzania.


Mafisadi hawawezi kuacha hivi hivi na wataendelea kuwashughulikia wapambanaji wote ambao wana orodha yao. Tanzania ya sasa sio ile ya zamani ambapo watu walikuwa huru kwenda popote bila kuwa na wasi wasi hayo ndio matunda ya BWM, JK na Chama Cha Majambazi. Na kwenye mazishi watakuja kuwasanifu.


Jiulizeni kwa nini wale waliokuwa moto wa mapambano siku hizi wako kimya?


RIP Prof. Jwani.
 
Kwa jinsi ambavyo nchi yetu imekuwa na mauaji ya mfulilizo huku police wetu wakichukulia kuwa ni issue tu ndogo ya kawaida, mie sasa natangaza nia ya kuwa mkimbizi nje ya Tz. Wiki iliyopita nikichangia post fulani iliyotumwa humu JF nilisema jijini Dar mauaji kwa sasa ni zaidi ya yale ya jo-bug. Sasa hili la proph limevuma sana kwa sabubu alijulikana kwa nafasi alizokuwa anashikilia. Kwa watu wa kawaida ndio usiseme wanauawa kila kukicha. Nina rafiki yangu aliyeuawa kwa mazingira kama haya ya prop mwezi huu wa may28. Majambazi yaliingia nae getini na kumuulia ndani ya gari yake hata kabla haijazimwa. Simu zake zilizoporwa ziliendelea kuwa hewani hadi siku iliyofuata bila police kuweza kuwanasa hawa wauaji. Inauma sana, inasikitisha sana. Tz tutaendelea kuwa shabaha ya magenge ya nyang'au mpaka hapo tutakapo pata uongozi wa kuweza kutiisha nchi. Kwa sasa ni kama tu hizo post za uongozi zipo wazi.
 
Dah!!

Jamaa alikuwa jirani yangu kwa muda mrefu sana mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini; alikuwa jirani mzuri sana ambaye nina hakika majirani zake wa sasa watamkosa sana.

Mungu ailzae pema roho yake.

Je kwenye kesi ya Rwanda yeye alikuwa anateteta upande upi wa kesi? Upande unaoshabikiwa na serikali ya Rwanda au upande unaopingana na matakwa ya serikali ile.
 
habari nilizozipata zinasema prof.mwaikusa mwalimu wa sheria na mwanasheria aliyebobea wa chuo kikuu cha dsm amefariki dunia baada ya kuvamiwa na watu wanaosemekana kuwa ni majambazi alipokuwa akirejea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. prof.mwaikusa pia alikuwa rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowakilisha kuhusu mgombea binafsi. mwenye data zaidi atujuze. rip prof.mwaikusa.

OOOh, my God. Na hiki kidogo tulichonacho tunapokonywa. Tuna idadi ndogo sana ya watu waliofikia kiwango chake katika tasnia ya sheria.
Haya ni mambo ambayo yanarudisha nyuma maendeleo ya Tanzania na Afrika kwa ujumla. Wataalamu WENGI wa TZ/AFRIKA WANAKUFA MAPEMA hivyo hawatumiki kwa muda mrefu kama ilivyo katika bara la Ulaya.

WITO: SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI WA KINA, ILI WATAKAOBAINIKA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA.

POLENI WATZ NA WAAFRIKA WOTE, TWAMUOMBA MUNGU ATUFARIJI NA KUTUFUTA MACHOZI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
 
good !!!mi nahisi wanakula nao ndugu yangu

Niwa pe hili la kidokezo cha POLISI KAWE...kama mmeona kwenye tv majuzi pikipiki walifunga barabara kisa polisi kukataa kwenda kwenye tukio huku gari 2 ziko nje na mafuta full kujiachia.....
baada ya kelele zile wakatoa gari moja walipofika kituon wakaja na masharti wanaenda wenyewe wakaambiwa nenda na mmoja anaekujua wakataa wakadai waelekezwe amuwezi amini waligeuza lile gari wakarudi...Baada ya muda mchana akaja mama mmoja samahani kama ilikuwa siri pale kituon saa kumi na moja yule mama anauza michicha anajulikana akaja akatukana sana wanapikipiki wakataka kumpiga kabla ya sie wenye upeo kumchukua..kumficha buchan..baada ya muda tukamtoa aeleze kilichomsibu kutukana ..wakamwekea ulinzio mama akaanza kumwaga nyie wenyepikipiki mnauwana wenyewe twendeni niwaonyeshe pikipiki mlipoificha..chumba cha jiran na wamekuja usiku saa 11 wanashindana ilale hapa au lah....akasema waliomuaa wako hapa hapa kijiwen tanki bovu na wanaendesha pikipiki...wapuuzi sana nyie ndio maana hata askari wamewadharau...anyway tatizo kubwa la askari wetu waqnataka pesa mbele biola pesa akuna msaada


Majuzi nina sehemu kimara za biashara wamiba nikamchukua mlinzi nikamweka ndani nilipofika kimara kituona wakakataa kumpokea ati mpaka wafanye uchunguzi nikawaambia ammpokei akaniita dada mmoja nimpe alfukumi..nikatoka nikampigia mkuu wa kituo kimara,nikapiga kwa mhe sana..nikawaeleza na kumpa namba za yule dada na wanaume wanazovaaga pale mbele gafla nikaona wanamchukua wanamweka ndani wakanifwata wanadai niwape alfu tano ya mafuta kumpeleka mbezi nikawambia mwacheni hapo alafu bosi wenu atakuja kumbeba

So kila sehemu ni chafu chafu zinanuka vituo vingi vya polisi vinanuka hongo rushwa usipomjua mtu ama kuwa na pesa ni aiubu ama imekula kwako

Hadithi nzuri lakini hazina mtiririko............hata hueleweki..!
 
OOOOOH Maskini nina majonzi makubwa huyu mwenzetu alikuwa mtetea haki kwelikweli mungu awalaze pema ,oooh tutafanya nini Kova anasema amewamaliza majambazi huku watu wengi wanauawa kila kukicha jamani nchi hii tukimbilie wapi
 
Hali Inatisha nyumbani Wakuu JF..........................

Kuna mada hapa ilikuwa inaelezea jinsi ambavyo Dara HAIKO salama na hasa kwa watu wanapokuwa wanarudi majumbani kwao maeneo ya Mbezi Kunduchi etc etc..................na sasa tunaona hivi hivi tunapoteza moja ya HAZINA za Taifa hili.................Damn!

RIP Prof Mwaikusa...............poleni sana wafiwa
 
Usalama wetu kwa sasa ni mdogo sana, kama watu tutakuwa tunauana as simple like this ndugu zangu inatia wasiwasi maishani, yaani unatoka nyumbani unaenda kazini huna uhakika kama utarudi salama - duh. Hii ndiyo amani na utulivu tunaoimba kila siku?

Tunachosema tu pole kwa Mjane, Watoto na Wana familia wote - Lakini je sisi kama jamii hatuna mchango wetu juu ya tukio hili?
Tumwachie mwenyezi mungu, Tuache vyombo vya dola vifanye kazi yake, tukae kimya bila kujitetea as if tunasubiri hukumu mahakamani? tufanyike kipi? maana leo ni huyu marehemu baada ya miezi 2 utasikia mwingine tena. Tanzania yetu ndiyo hiyo inamogoka taratibu.
 
Jamni hii inasikitisha sana.Hivi hao wanaojiita JWTZ kwa nini na hao wasihusishwe na ulinzi wa raia na mali zao.maana kwa mtazamo wangu naona hawana kazi zaidi ya kuchukua mishahara tu.Ethiopia nchi inalindwa na wanajeshi na kila wakati utawaona wakizunguka kuhakikisha usalama upo.Jamani serikali ifanye mabadiliko kwa hawa watu sio kusubiri mpaka vita itokee.
Mungu zilaze roho za marehemu mahali pema mbinguni.
 
Je alikuwa na Mlinzi pale nyumbani kwake?

Je hao wauaji wameiba nini kutoka kwa Prof?
 
"Kampenda zaidi" ndio amuache achinjwe hivyo na mwanae? Yani sisi tunaompenda kidogo tunamwonea hurumu huyu Mungu anaempenda zaidi hana huruma, Mungu gani? "Awatie nguvu katika wakati mgumu" wakati mguu saa ngapi tena, wakati mgumu ni pale wakikatwa roho, ndio pale Mungu angetaka angeibuka akawatia nguvu marehemu, hakutokea, bado tunamsubiri? Hata polisi walikuja baadae.


umenifanya nicheke kidogo

kweli tumeumbwa tofauti
 
Sidhani kama hao ni majambazi. Hicho ni kikosi maalum ambacho kimetumwa kufanya hiyo kazi. Majambazi wengi huwa hawaui moja kwa moja kwanza hutishia na kuona kuwa unafuata masharti yao, huu ni mpango kabambe ambao umefanyika kutokana na misukosuko ya kisiasa nchini Tanzania.


Mafisadi hawawezi kuacha hivi hivi na wataendelea kuwashughulikia wapambanaji wote ambao wana orodha yao. Tanzania ya sasa sio ile ya zamani ambapo watu walikuwa huru kwenda popote bila kuwa na wasi wasi hayo ndio matunda ya BWM, JK na Chama Cha Majambazi. Na kwenye mazishi watakuja kuwasanifu.

Jiulizeni kwa nini wale waliokuwa moto wa mapambano siku hizi wako kimya?


RIP Prof. Jwani.

Tusi argue kwa emotions jamani...huyu mtu kweli kauawa na mazingira ya kifo chake ni kweli yanatia mashaka lakini si busara kuanza ku point watu au taasisi katika hili kwa sababu tunaujua upande mmoja tu wa maisha ya profesa (profesheni yake) hatujui upande wa social life yake....inawezejakana waliomuua wana visasi na familia au nayeye mwenyewe...SIKUBALIANI NA KUANZA KUJAJI SUALA HILI KISIASA KWANI NADHANI TUMEKUWA NA WATU WENGI TU HAPA WANAOIKOSOA SERIKALI WAZI WAZI...SHIVJI, LATE CHACHAGE, HAROUB, Baregu...et
Nikisoma taarifa nchi nyingine juu ya mauaji ya watetea haki naiweka serikali ya TZ kwa awamu zote katika mstari wa uvumilivu uki kompea na kenya , zaire nk hata kama inaua watu lakini si utamaduni wake ku deal na wapinzani kwa staili ya kuua
wote hawa mbona wasiuwawe? iweje leo huyu ndio aonekane ana impact ya ajabu!!!! siamsini katika hili KIRAHISI RAHISI...MAISHA YA MTU HAYAISHII KWENYE PROFESHENI YAKE TU
tusiwe wepesi wa kutupia kila lawama serikali .....ni kukosa akili ya uchambuzi
Pole kwa wanafamilia, pole kwa wafanyakazi wenzake na wanasheria....pole kwa watz wote
mix with yours
 
habari nilizozipata zinasema prof.mwaikusa mwalimu wa sheria na mwanasheria aliyebobea wa chuo kikuu cha dsm amefariki dunia baada ya kuvamiwa na watu wanaosemekana kuwa ni majambazi alipokuwa akirejea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. Prof.mwaikusa pia alikuwa rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowakilisha kuhusu mgombea binafsi. Mwenye data zaidi atujuze. Rip prof.mwaikusa.

r.i.p prof.
 
Not acceptable pls. We deserve better than this!

Mkuu i can assure you, this is what will happen. Not acceptable for sure, but believe me nothing will happen. Kama ikitokea lolote itakuwa sawa na kesi ya Zombe, at the end of the day mtu atakuwa huru. Matokeo ya kesi ya nyani kwa ngedere. Ukiangalia juu juu utaona kuwa kuwa walioua si majambazi na sidhani kama jamaa alikuwa politicians. Hili ni fundisho kwa wasomi wanaojifanya kuunga mkono opposition. Unajua kuna mawili hapa. Kuua hoja na hoja ya kuua, haya mawili yanazunguka kwenye issue nzima ya mgombea huru. Ukiangalia hiyo ndio ilikuwa mwiba mchungu kwa baadhi ya watu, ingepita hoja hiyo basi utukufu wa baadhi ya watu ungekuwa umefika mwisho. waliokuja na hoja nzito na za kweli in favour ndio hao wameanza kuwa eliminated.
 
It is shocking how these murders and attacks go on unabatted. There is a wave of the so called 'Majambazi' ambushing people at there entrances in the Mbezi Beach and Kunduchi area. According to some of the victims police know this group but are unable to get them!!! With such firearms 'ulinzi shirikishi' can not work.
Poleni sana ndugu wa marehemu. John alikuwa mtetezi wa wawanyonge toka akiwa mwanafunzi. Ni kweli Mungu amempenda zaidi. Polisi ifanye kazi kukamata genge hili.
 
Tunatumai ni kifo cha kawaida sio chenye mkono wa mtu..
..SOTE TU MAVUMBI NA MAVUMBINI TUTARUDI...pumzikeni kwa amani

Mkuu, thread inasema kauwawa na "majambazi", sasa utasemaje ni kifo cha kawaida na hakina mkono wa mtu???? kina mkono wa hao wanaoitwa majambazi
 
Dah! Inasikitisha!
Nimekumbuka enzi zake akifundisha adm law, then mgombea binafsi...inauma.
Poleni sana wafiwa!
 
Mwanakijii hapa Bongo kama ukiwa intellingent hapakufai. Nawashauri nyie mlio intellingent mkae huko huko majuu, otherwise ni kujitafutia matatizo, kingine ni kuwa kimya kuwa kama zuzu ukiona mambo yanaenda ovyo kaa kimya tu.

Bongolander

Huu ni ushauri gani unaompa mzee mwanakijiji? sasa unataka nani aipiganie nchii kama si yeye?
 
Back
Top Bottom