TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

RIP Prof. Jwani Mwaikusa.

Tunakubali kifo kitamkuta kila mmoja wetu, ila Serikali ina haki ya kikatiba kuwa linda raia wake.
Kwa serikali yetu jambo hili ni kinyume chake. Polisi ndo wanaolinda majambazi!!! Eti siku hizi wanasema watu walinde mitaa (polisi jamii)

Poleni wafiwa, Mungu awatie nguvu na imani katika wakati huu mgumu. Tulimpenda lakini yeye kampenda zaidi. AMEN.
 
Tatizo letu kubwa ni kwamba crimes nyingi sana za homicide zimekuwa zikichukuliwa kwa urahisi rahisi tu kama ajari za moto, magari, au mauwaji ya ujambazi na kwa kadri ninanvyojua mimi polisi wetu ama kwa uzembe au makusudi ama kwa kutokuwa makini na kazi zao wamekuwa wakihalisha na kufunga mafaili ya homicide kama ajari au ujambazi wa kawaida.

Ninadhani ni wakati muafaka tukaanza kuwa na desturi ya kuchunguza kwa undani na kuweza kufanya hivyo inabidi ajira za jeshi la polisi au kitengo cha homicide zikaangaliwa upya ili watu wanaoajiliwa wawe watu makini na siyo drop outs au watu waliofeli mitihani yao kwenye ambao wanatafuta upolisi kama last resort katika kutafuta riziki.
 
Mkuu sifahamu hata muuaji mmoja, lakini naweza kusema hakuna mnyarwanda anayeweza kuja kumuua huyo jamaa kwa kuwa judge tu wa ile mahakama. Tusiumize vichwa kwa sasa, he is already dead, in weeks and months ahead tutajua muuaji ni nani, for sure hata kamatwa and life will go on. Hii ndio haki Tanzanian style.


Not acceptable pls. We deserve better than this!
 
HABARI NILIZOZIPATA SASA HIVI NI KWAMBA HII NI ASSASSNATION. Hawa wauaji waliingia nyumbani, wakapiga risasi kadhaa kuwascare wanafamilia walio kuwa ndani. Baada ya hapo wakamshoot risasi ya kichwa na kumuua.
Katika kurusha rusha risasi za kuscare waliokuwa ndani wakampiga risasi mtoto wake aliyekuwa nje , na kumuua. Mtoto huyo anaitwa Gwamaka
Wakiwa wanatokomea, wakamwona mpitanjia ambaye walihisi (nadhani ) amewaona naye wakampiga risasi nyingi kiasi cha kusambaratika ovyo.
RIP Proffessor Jwani Mwaikusa.
Tunaomba polisi ifuatilie motive ya mauaji: Je ni visa? Ni political? au ni mambo ya Rwanda?

Sasa kwa mambo haya wameitaji majambazi wakati hawajaiba chochote? they should say black and white ni MAUAJI.
 
yes,inaonekana kama ni planned assasination.polisi tafadhali fanyeni uchunguzi.
isije ikawa ni mafisadi,maana wana mtandao mkubwa na wako tayari hata kutoa uhai wa binadam.
MUNGU AILAZE ROHO YA PROF.MWAIKUSA MAHALI PEMA PEPONI.

haki haitapotea kamwe!

Another actors; sijui itakuwa season ya ngapi?
 
Poleni wafiwa. Kama alitetea hoja ya mgombea binafsi, nina wasi wasi kuna mkno wa wale wale, wabongo tunatawaliwa na jinamizi ambalo silielewi, nguvu za giza..for how long will this last. Kutawaliwa kimafia ni risk kubwa jamani! Nadhani mwisho wetu ni mbaya!
 
Mungu awatie nguvu na imani katika wakati huu mgumu. Tulimpenda lakini yeye kampenda zaidi. AMEN.
"Kampenda zaidi" ndio amuache achinjwe hivyo na mwanae? Yani sisi tunaompenda kidogo tunamwonea hurumu huyu Mungu anaempenda zaidi hana huruma, Mungu gani? "Awatie nguvu katika wakati mgumu" wakati mguu saa ngapi tena, wakati mgumu ni pale wakikatwa roho, ndio pale Mungu angetaka angeibuka akawatia nguvu marehemu, hakutokea, bado tunamsubiri? Hata polisi walikuja baadae.
 
Poleni wafiwa na Watanzania wote kwa kumpoteza mtu muhimu katika familia yake na taifa kwa ujumla. Ni wazi haya ni mauaji na wala sio ujambazi, lakini wahusika lazima waelewe kwamba ipo siku watalipa wao na vizazi vyao.

R.I.P Prof Mwaikusa, tutakukumbuka.
 
Ndo keshakufa hivyo. Hakuna cha kufanya isipokuwa hao waliomuua hukumu yao ni hapa hapa duniani siku sio nyingi. Polisi inapaswa kubeba lawama zote. RIP Prof.
 
Kama namsikia IGP Akiongea na watu wa tasnia ya habari "Nimawaeten blah blah ....then nitaunda tume ya watu 7 kuchunguza mauaji haya blah blah..."

Kila siku huwa tunafanya kazi kwa stahili za kizimamoto.
 
Kutoka Michuzi Blog:


BREKING NYUUUUZZZZZ: PROFESA MWAIKUSA AUWAWA JIJINI DAR
Marehemu Profesa
Jwani Timothy Mwaikusa


Habari zinasema Wakili na Mwanasheria nguli na Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Jwani Timothy Mwaikusa amefariki dunia baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akirejea nyumbani kwake maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.

Prof. Mwaikusa pia alifanya kazi katika mahakama ya kimataifa ya I.C.T.R Arusha na alikua rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowasilisha kuhusu mgombea binafsi.

Kwa wale waliosoma literature A- Level kama mimi, Prof. Mwaikusa pia alikua mwandishi mzuri wa poems ambazo wengi wetu tulizijibia mitihani.
Pamoja nae pia ameuwawa mwanae aliyekua akitoka nje kumfungulia geti, na mtu baki aliyekua akipita njia.

Kwa jicho la kawaida tu, haya yatakua mauaji ya kisasi au ya kumnyamazisha kuhusu jambo fulani kwakua habari za awali zinasema wauwaji hao hawakuiba kitu chochote

Na Mdau Nkundwe Mwakilema

NILIYOYAFAHAMU:
Career:
* Professor of Law, Faculty of Law, University of Dar es Salaam 1999
* Mkono & Co Advocates since 1998
* Advocate, High Court of Tanzania since 1988
* Managing Editor of the Tanzania Law Reports.
Qualifications:
* Ph.D., School of Oriental & African Studies, University of London, UK, 1995
* LL.M, University of Birmingham, UK, 1985
* LL.B (Hons), University of Dar es Salaam, Tanzania, 1981.
 
Nilianza kumfahamu Prof Mwaikusa tangu ile kesi ya akina Juma Duni ya kutaka kuipindua Zanzibar. Profesa makini kwelikweli, anachagua kwa umakini maneno ya kuzungumza, ametulia sana, alikuwa na nidhamu sana ya kazi yake. Aliwaheshimu sana wanasheria wenzake ambao wengi aliwazidi kitaaluma na kielimu.

Mungu ailaze roho yake pema peponi...well, kwa bahati mbaya watu makini ndio wanatangulizwa kwanza mbele ya haki ili mabazazi waendelee kupeta. Hao majambazi sijui wanajua ni kwa kiasi gani Taifa limepoteza mtu makini? Na naendelea tena kujiuliza, inakuwaje wavamie nyumba yake usiku? Alikuwa na benki nyumbani kwake? Ukweli unatabia ya kujitenga na uongo...ipo siku ukweli utawekwa bayana
 
Akiwa anakaribia kutaja mgombea binafsi naomba nimnukuu RAIS,DK KIKWETE

Mimi napenda niwaonye kabisa yoyote atakaeshabikia ama kutaka kufanya kitu kitakachotutenganisha
nawaambia kweli hii serikali si sehemu ya kutafuta umaarufu,,nasema hili nikimaanisha nawambia ili mtu asishangae ..kuna walioanza chokochoko tuliwashugulikia na wengine (

tumewasahau)

kabisa

Mwenye akili utajua ana maana Gani!!!nawaambia ukweli tutakushugulikia mpaka mwisho..mi nawaambia msidanganyike bwana kitu kikija kwangu nikisema no ni no hata iweje..utahangaika kwa haki za binadamu ,,mahakama kuu na vyombo vingine vya sheria nikisema no itaishia no

DK KIKWETE TUELEZE PROF WETU ALIPO...HILI JAMBO WANA JF SI LA KUCCHUKULIA MZAHA HATA KIDOGO..ATUITAJI KUISHI NA SERIKALI YA WAUWAJI..UTAMUUA KILA MTU SIKU YA MWISHO BABAKO ANAKUKANA UTAMMALIZA???





Nadhani unaamanisha wakati alipokuwa anakaribia kumtaja mgombea mwenza.
 
Back
Top Bottom