Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 408
Habari ambazo zimeingia sasa hivi ni kuwa Prof. Jwani Mwaikusa ameuawa. Pamoja naye taarifa zinadokeza kuwa mwanae pia ameuawa. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizo kwa karibu ili kuweza kupata taarifa za uhakika zaidi.
Wengi tunamfahamu hivi karibuni katika kesi ya wagombea binafsi akiwa mmoja wa walioitwa kuwa "marafiki wa mahakama" yeye akitetea haki ya wagombea binafsi na kusisitiza kuwa mahakama ina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. Siku za karibuni amekuwa ni mwanasheria katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda na mmoja wa wanasheria waliobobea wa Katiba amefariki duniani.
Taarifa zinadokeza kuwa mauaji hayo yametokea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.
Taarifa bado zina kiza kuna uwezekano wa zaidi ya watu wawili kuwa wameuawa kwenye tukio hilo..
sina details zaidi.. vyanzo vyetu vinafuatilia..
Hapo kwenye bold kama ni kweli we need to think twice.....! Gen. Nyamwasa, Prof. Mwaikusa.......who is next?