TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

..what a sad news! Mwe...MUNGU wape moyo wa matumaini familia na ndugu wa mpendwa wetu JWANI!

Usalama katika nchi hii ni ZERO, majambazi wanatamba na kupoteza roho za watu kadri wapendavyo. Hii si ajabu kwani baadhi ya Police yasemekana wamo kwenye payroll za majambazi:embarrassed1:

Ndugu yake kanielezea kwa simu mazingira ya kifo: Prof Jwani alikua anarudi nyumbani kwake alipoingia getini, majambazi wawili unknowingly waliingia naye. Wakamlazimisha kushuka kwenyee gari yake, hakushuka na ndipo walipoanza kummiminia risasi na kumuua. Mtoto wake akaja ili atoe msaada (bila shaka baada ya kusikia milio ya risasi) nae pia kamiminiwa risasi na kufa. Pia inasemekana jirani yake naye katika jitihada za kutaka kuja kutoa msaada naye kauwawa!!! :embarrassed1: UKAGONE MALAFYALE!

MUNGU MWENYE REHEMA NA NEEMA NYINGI, WASAMEHE WALIOFANYA KITENDO HIKI CHA KIKATILI NA KUTOA ROHO YA MPENDWA WETU!!!!
So, so, so sad and shocking. Nilikuwa sijaamini nilivyosoma kwa mara ya kwanza.
This sounds more like a planned assassination to me - not just ujambazi wa kutaka kupora.
 
habari hii ni kubwa ,tafadhali mwenye uhahikika alete taarifa ya kuthibitisha haya mabo mazito
 
Tunatumai ni kifo cha kawaida sio chenye mkono wa mtu..
..SOTE TU MAVUMBI NA MAVUMBINI TUTARUDI...pumzikeni kwa amani
 
habari hii ni kubwa ,tafadhali mwenye uhahikika alete taarifa ya kuthibitisha haya mabo mazito

ndiyo habari iko hivi. Mwanzoni kulikuwa na michanganyo ya majina ya Maprof. wengine.. kama Mwandosya na Mwaikyusa.. lakini sasa taarifa ni za uhakika zaidi.
 
RIP Prof.......... Ila watanzania lazima tukubali hiyo tunayooiita siku zote amani na utulivu ni mazingaombwe as everybody is insecure. Ndio maana nyumba nyingi especially in Dar ni kama magereza. Kuta futi kumi, razor wire on top magrill mpaka kwenye paa. Wamasai na vijikampuni vya ulinzi ili mradi it is just chaos!!!!!!!!!!!

Inasikitisha watu wengi wamepoteza maisha kwa uvamizi wa hawa majambazi and it seems bado sio ishu!!!!! Kuna kipindi nilikuwa likizo hapo Boko kila usiku kulikuwa na nyumba imevamiwa tena saa mbili jioni. Polisi wanatokea two hours later!
 
..what a sad news! Mwe...MUNGU wape moyo wa matumaini familia na ndugu wa mpendwa wetu JWANI!

Usalama katika nchi hii ni ZERO, majambazi wanatamba na kupoteza roho za watu kadri wapendavyo. Hii si ajabu kwani baadhi ya Police yasemekana wamo kwenye payroll za majambazi:embarrassed1:

Ndugu yake kanielezea kwa simu mazingira ya kifo: Prof Jwani alikua anarudi nyumbani kwake alipoingia getini, majambazi wawili unknowingly waliingia naye. Wakamlazimisha kushuka kwenyee gari yake, hakushuka na ndipo walipoanza kummiminia risasi na kumuua. Mtoto wake akaja ili atoe msaada (bila shaka baada ya kusikia milio ya risasi) nae pia kamiminiwa risasi na kufa. Pia inasemekana jirani yake naye katika jitihada za kutaka kuja kutoa msaada naye kauwawa!!! :embarrassed1: UKAGONE MALAFYALE!

MUNGU MWENYE REHEMA NA NEEMA NYINGI, WASAMEHE WALIOFANYA KITENDO HIKI CHA KIKATILI NA KUTOA ROHO YA MPENDWA WETU!!!!

Mkuu Lwikunulo,

Kwa kuwa wewe huko karibu na ndugu yake, hebu tujuvye basi kama hao the so called majambazi walichukua chochote? Hii ni muhimu kujua ili tuweze kutafuta kiini cha mauaji kama kweli ulikuwa in ujambazi, ni visasi au government at work!!!!!

Tiba
 
Why many important persons in the society die, mostly in dubious circumstances, and indeed when their contributions are mostly needed!!!

Oooh my Lord, You Are The One, The Only One, Alfa & Omega...We cry to You, forgive our Professor's soul for any misdeed he had done when on this Earth.... we human beings are weak in body and soul,and subjected to certain frequent failures... we have already done the same since Your Son Jesus Christ taught us to forgive and have mercy on our fellows.....he departed when we, Tanzanians need him mostly...his expertise in the Legal arena,especially in Constitutional Law and Administrative Law will take long to be matched by his fellow academicians...

MAY HIS SOUL REST IN PEACE...AMEN
 
Hawa majambazi watatumaliza kunahaja ya kujiuliza bado tunahitaji kuwa na jeshi la polisi ? R.I.P Prof Mwaikusa
 
Waliokwisha kusoma kitabu kinaitwa "the man of the people" wanaweza kuelewa mambo haya vizuri. Ni vizuri kama walivyouliza wengine je, majambazi hao wamechukua nini? Je, alikuwa na mali sana?
 
Nyambala kama uko ughaibuni umetulia,bora ukae huko huko maana Dar inatisha kweli.
Unaweza kuwa na peza za ufisadi,lakini standar ya maisha ni POOR !

Kuanzia hospitali,barabara ,ajali na ujambazi .Watu wanapoteza maisha kirahisi sana Tanzania
 
habari nilizozipata zinasema prof.mwaikusa mwalimu wa sheria na mwanasheria aliyebobea wa chuo kikuu cha dsm amefariki dunia baada ya kuvamiwa na watu wanaosemekana kuwa ni majambazi alipokuwa akirejea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. prof.mwaikusa pia alikuwa rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowakilisha kuhusu mgombea binafsi. mwenye data zaidi atujuze. rip prof.mwaikusa.

Kwa maoni yangu kifo chake kimekuja late i was for long time waiting to hear who will be first to be eliminated, sad to see it is him, na kitanyamazisha wengi. Lakini wenye akili wanajua ni nani wamemuua na wasio na akili pia wanajua kuwa si majambazi, bado hatujaambiwa kuwa wameiba nini kama kweli ni majambazi, na lengo la mauaji bado "halijulikani". Tusubiri taarifa zitakazotolewa usikie unafiki wa sisi watanzania.
Kwanza utasikia alikuwa msomi hodari, alitetea katiba kwa moyo wote, tumesikitishwa sana na kifo chake, jeshi la polisi litafanya uchunguzi na wahusika watachukuliwa hatua kali. It will end there.
 
Nilianza kumfahamu Prof Mwaikusa tangu ile kesi ya akina Juma Duni ya kutaka kuipindua Zanzibar. Profesa makini kwelikweli, anachagua kwa umakini maneno ya kuzungumza, ametulia sana, alikuwa na nidhamu sana ya kazi yake. Aliwaheshimu sana wanasheria wenzake ambao wengi aliwazidi kitaaluma na kielimu.
 
yes,inaonekana kama ni planned assasination.polisi tafadhali fanyeni uchunguzi.
isije ikawa ni mafisadi,maana wana mtandao mkubwa na wako tayari hata kutoa uhai wa binadam.
MUNGU AILAZE ROHO YA PROF.MWAIKUSA MAHALI PEMA PEPONI.

haki haitapotea kamwe!
 
yawezekana kitendo cha kuchukua upande kinyume na uliopigiwa debe na wakuu ulikuwa ni kujitia kitanzani? itabidi na wengine waanze kufikiria misimamo yao.
 
RIP Prof.

Kuna angalizo lililofanywa na wanahabari wa gazeti la 'Mwananchi' waliongelea kuhusu mfumuko wa ujambazi kati ya makongo, salasala, mbezi juu na mbezi shamba....tutaona matukio mengi ya kusikitisha LABDA SERIKALI ijipange vizuri na hasa kipindi cha kampeni ambapo rasimali zote [pia rasilimaliwatu -kama vyombo vya usalama] utamaduni waonyesha kwamba uamishiwa katika kampeni za wanasiasa[Rejea chaguzi za 2005 et al]
 
yawezekana kitendo cha kuchukua upande kinyume na uliopigiwa debe na wakuu ulikuwa ni kujitia kitanzani? itabidi na wengine waanze kufikiria misimamo yao.

Mkuu, with all due respect naomba usianze mambo yako ya kuingiza kila kitu kwenye siaza tafadhali... IT IS TOO EARLY!!!
 
Back
Top Bottom