isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,125
- 6,250
Hakika,Kweli kabisa na vilabu vingine vina kurasa zao kabisa ila ukizitafuta unapata ukakasi kujua kama kweli ni page official ya timu, unakuta haina mpangilio na mtiririko mzuri wa machapisho.
Wachezaji nao ni muhimu sana kuwa na kurasa zao tena muhimu kuajiri na admin ambaye atakuwa ana uhakika wa kupakia taarifa za mchezaji, nadhani watanzania wengi wangekuwa wanawafatilia na hii ingewapa hata dili za kutangaza bidhaa au huduma za kampuni mbalimbali.
Tanzania tuna mfano mzuri sana; Mbwana Samatta, kiukweli post na caption zake siku hizi zinanifanya niamini kuna mtu tofauti na yeye anayeendesha page yake na kama anasimamia mwenyewe kiukweli yupo njia sahihi. Post zake za hivi karibuni nyingi zinaandikwa kwa Kiswahili fasaha na hata Instagram translator ina uwezo wa kutafsiri kwa 80% kilichoandikwa kwenda Kiingereza. Kubwa zaidi sasa ana Logo inayomtambulisha na post nyingi za matukio maalumu huwa zinafanyiwa poster design na kuwa na logo yake. Watu nyuma yake wanafanya kazi nzuri sana.
Kuna mapinduzi yanatakiwa katika suala la kimtandao na kidigitali kuendana na kasi ya teknolojia na soko huria.
Tafakari klabu inaitwa Victoria Football Club huku handle za Twitter na Instagram ni @victoria_fc_waletee unakuta @victoriafc au @fcvictoria hazijachukuliwa alakadhalika kwa wachezaji.