Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Wakuu habari za kuaminika kwamba kanumba amekutwa saa 9 usiku amekufa kwenye gari lake.source tbc jambo.RIP KANUMBA.
 
Inasemekana amepigwa na kitu kizito kichwani baada ya tafulani ya kimapenzi.
 
Wadau habari ni za kweli! redio nyingi zimeshatangaza kifo chake,kilichobaki tumuombee kwa mwenyezi Mungu amuweke panapostahili!
 
Twendeni taratibu jamani; kuanza kudai huyo binti "kamuua" tunaenda mbali sana. Inawezekana kabisa ni accidental death. Maana wengine wanaseema "kauawa" ni kana kwamba kulikuwa na mipango na nia ya kufanya hivyo. Yaani, hili haliangukii hata kwenye crimes of passion kama ndivyo lilivyotokea. Twendeni taratibu na huyu binti mdogo tusianze kumshakizia mzigo wa mauaji wakati hatujui nini hasa kilitokea kati yao. Lets get the details before we form opinions.

Kama Wanjiru, yule mkimbiaji maaarufu wa Kenya aliyefariki baada ya kujirusha toka ghorofani baada ya kufumaniwa na mkewe. RIP Steven Kanumba
 
MILLAD AYO.COM:

Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, millardayo.com itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.



Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.



‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.



Hapo chini ni baadhi ya kauli nilizokutana nazo kwenye facebook wakati huu na chini yake ni maneno ya mwisho STEVEN KANUMBA kuyaandika kwenye kurasa zake za facebook na twitter.
Page ya Mwigizaji Mainda.

.

ALIYOYAANDIKA YA MWISHO MWISHO KWENYE PAGE ZAKE ZA FACEBOOK & TWITTER
Hivi ndivyo ukurasa wake wa facebook unavyoonekana.

.

.

.

Hii ndio ilikua tweet yake ya mwisho.

 
Back
Top Bottom