Tanzania Zanzibar Vs Tanzania Tanganyika

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,277
8,492
Jina Tanganyika limepotea. Inapotokea Tanganyika kutajwa ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi hutajwa Tanzania Bara. Je Tanzania bara ndio nchi gani?

Natamani kuanzia sasa Tanganyika irudi na ndani ya Muunga iitwe Tanzania Tanganyika.

Tanzania Visiwani inajulikana kwa uasili wake, yaani Tanzania Zanzibar why not Tanzania Tanganyika? Kwa nini?
 
Jina Tanganyika limepotea. Inapotokea Tanganyika kutajwa ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi hutajwa Tanzania Bara. Je Tanzania bara ndio nchi gani?p

Natamani kuanzia sasa Tanganyika irudi na ndani ya Muunga iitwe Tanzania Tanganyika.

Tanzania Visiwani inajulikana kwa uasili wake, yaani Tanzania Zanzibar why not Tanzania Tanganyika? Kwa nini?
Zitakapotoka fulana zilizoandikwa Tanzania Tanganyika tufahamishane!
 
lakini mimi napendelea tuitwe Watanganyika kutoka nchi ya Tanganyika silipendi jina Tanzania Bara...
 
Anamaanisha kwenye Muungano,nje ya Muungano ni Tanganyika.

Sideeq, haswaa umenena; Ndani ya Muungano tutambuliwa kama Tanzania Tanganyika na sio Tanzania Bara. Kwani nchi yetu iliyomezwa na muungano ilijulikana kama BARA, hapana ni TANGANYIKA.

Kwa hiyo tuwe na Tanzania Tanganyika na Tanzania Zanzibar ndani ya Muungano. Nje ya hapo basi sisi ni waTanganyika.
 
lakini mimi napendelea tuitwe Watanganyika kutoka nchi ya Tanganyika silipendi jina Tanzania Bara...

Hakika sisi ni WaTanganyika na wao ni WaZanzibar. Hakuna mtu anayeitwa Mtanzania Bara au M-Bara.
 
Back
Top Bottom