Tanzania yetu ndio nchi ya furaha

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,763
35,201
Nikiwa njiani najisomea na kusikiliza habari tofautitofauti za kijamii, kisiasa, kiuchumi toka mataifa tofauti; nimejikuta nikimshukuru Mungu kuwa mtanzania.

Hakika Tanzania yetu ndio nchi ya furaha.

Tumebarikiwa kuwa na waasisi bora wa taifa waliotuachia misingi imara isiyotikisika, tumajaliwa kuwa na viongozi bora wanaoendeleza yale yaliyoanzishwa miaka baada ya miaka.
Tumejaliwa kuwa na umoja ulioweza kuvunja kabisa ukabila na ukanda, leo haijalishi ulizaliwa wapi unaweza kuishi, kufanya kazi, kuoa/kuolewa, kumiliki mali... sehemu yoyote ile inayokupendeza.

Haijalishi wewe ni wa imani gani unaweza kuishi na kuwa huru popote hata kwa wale wenye imani tofauti na wewe bila hofu.
Tanzania mkristo anaweza shiriki na waislamu kwenye ibada hata muislamu kushiriki na wakristo kwenye ibada bila tatizo wala vita

Tumshukuru Mungu kwa mazuri ya nchi yetu, tushikane na tushirikiane kuboresha na kudumisha yaliyo mema

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
 
Mama D unakosa sana na hii inflation

USSR
 
Nadhani umeficha kichwa chako ndani ya kibuyu, hebu kitoe uone hali halisi.
 
Mama D unakosa sana na hii inflation

USSR

Katika hali yoyote bado Tanzania ni ya thamani ileile kwangu

Tupambane kupangua makwazo kila mtu kwa nafasi yake
 
Nadhani umeficha kichwa chako ndani ya kibuyu, hebu kitoe uone hali halisi.

Kabla sijakitoa, na wewe fanya ukusanye watu wa nyumba yako, familia na ukoo wako ukahamie kule kuzuri unapopaona bora kwako
 
Unadhani nchi kama nchi ina shida basi,tatizo ni Hawa binadamu wanaoitwa wanasiasa!
 
... lakini kuna bomu inabidi mheshimiwa SSH alitegue kwa umahiri wa kiwango chake ... ili tuvuke hapa tulipo!

MBOWE SI GAIDI!
👊:cool:✌️💥
 
Tanzania ndio mama yetu, tumlinde kwa akili moyoni na za mwilini

Back
Top Bottom