Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,459
- 2,829
Nimekuwa nikijiuliza maswali mepesi au maswali magumu kutegemeana na akili yangu na kwa jinsi ninavyoona mambo yanavyokwenda Tanzania kuhusu Sekta ya Kilimo na Kifugo ambazo zinagusa Zaidi ya 60% wa wakazi wa nchi hii.
Wakati nawaza tunatokaje, jana nikakutana na taarifa Wakulima wanalamamika kuuza maziwa lita moja sh.700 mkoani Tanga, Iringa kuna kiwanda kinanunua maziwa lita Tsh 800. Maziwa haya baada ya huchakatwa yanauzwa kwa wastani wa Tsh 3200 kwa lita kwa bei ya jumla na wastani wa sh. 4,000 kwa lita kwa bei ya reja reja.
Ukilinganisha na New Zealand mwaka 2017 “The dairy sector contributes $7.8 billion (sawa na tril 11.4) (3.5%) to New Zealand's total GDP. This comprises dairy farming ($5.96 billion) (wakulima wanavuta Tril 8.74)and dairy processing ($1.88 billion) (viwanda vya kusindika maziwa vilipata Tril 2.76).
Hapa kwetu tuna tuna tajiri mmoja toka pemba anauza maziwa “reconstituted” baada ya kununua raw powdery milk toka india.
Bank ya kilimo kwa nini tusiwe na mkakati walau wa uhakika wa soko la "mpemba" anaechakata zaidi ya lita laki 1 kwa siku. Kama angenunua kwe bei nzuri, tunetengeneza ajira ngapi kwa soko la viwanda vya"mpemba". Tukifikiri kwa uchumi jumuishi ambao uwepo wa viwanda, kwanini vifaidishe india kununua maziwa ya unga ambayo yanakuwa reconstituted hapa kwa soko la ndani.
Kili nikifungua redio au TV mbona taarifa za wizara ya kilimo na wizara ya mifugo, wizara ya viwanda, wizara ya fedha hazi-address issue kama hizo. Au mimi siwazi sawia?
Kwa mwenye majibu anisaidie majibu ya maswali yafuatayo
Ni kwa kiwango gani tunatumia mkakati wa kitafiti (utafiti wa wazi au wa kificho) ya kwa ajili ya kukuza sekta ya kilimo& ufugaji kuwa za kibiashara na sekta zinazoingiliana na kilimo (mabenki, bima, usafirishaji, umeme, TBS, viwanda, TRA, maji, afya)?
Ni namna gani Tanzania kwa malengo ya muda mfupi na muda mrefu tunakuwa na taarifa za wakati ili kuwa na mkakati wa kukuza uchumi wa wakulima na wafugaji ili kutokea hapo viwanda vya ndani vifaidike na malighafi za kilimo/mifugo ili sekta zingine nazo zikue?
Tunatumia mfumo gani wa taarifa (information systems) ili Tanzania ikue kitaasisi kwa mfumo unaojinasibu na makuzi ya ukuaji wa kilimo na ufugaji ili kipato cha uchumi wa kati kiwe dhahiri zaidi katika maisha ya Watanzania?
Mkakati wetu wa kimaamuzi ukoje ili maamuzi tunayoamua yawe na mguso kwa wakulima na wafugaji wetu?
Ni kwa namna gani Tanzania ina mkakati wa muda mfupi na muda mrefu kukuza uchumi wetu ikiwemo kupunguza imports na kuongeza exports za mazao ya kilimo na ufugaji?
Benki ya maendeleo ya kilimo na Benki ya uwekezaji (TIB) wao wana picha gani ya kuhakikisha uwekezaji wa sekta ya kilimo walau unatuvusha kuhakikisha Watanzania na ukubwa wa li-nchi hili tunakwenda mahali kwa kuwa exporters wa agro-products.
Mwisho, BOT wataalamu wa analysis na kutoa reports za trend ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Kwa kuchungulia figures hizi hapa chini tena, tunawezaje walau kufanya hata 10% ya kinachofanywa na New Zealand? Just 10% kwa exports za maziwa baada ya kupunguza trade deficit ya kuagiza maziwa ya zaidi ya bil 100 kila mwaka? (Maana kwa Afrika Tz ni ya pili kwa wingi wa mifugo na tuna mifugo mingi kuliko New Zealand. )
https://twitter.com/theworldindex/status/1186661362338009088?s=08
Nikichukua New Zealand tena katika sampuli;
Latest export figures from Beef + Lamb New Zealand (B+LNZ) show New Zealand's red meat exports (excluding veal and co-products) were up $1.2 billion (sawa na 1.7 Tril)(21 per cent) on 2016-17 to over $6.7 billion (sawa na 9.8 Tril) in 2017-18 on the back of sustained high value per tonne and increased volume for lamb, mutton, and beef.
JPM huwa anauliza Watanzania tunakosea wapi. Watanzania tunakwama wapi. Wapiga kura wengi wa wanasiasa wengi akiwemo Rais JPM ni wakulima. Ni kwa namna gani nao tunawaingiza kwenye equation ya kukuza kipato chao ili wanapotumia nguvu yao ya kunua huduma na bidhaa wawe na mchango kupitia kodi zao za manunuzi ya bidhaa na huduma.
Wakulima wakinunua (kama wanavyonunua wafanyakazi) tu huduma za maji, umeme, bima za afya, wakawa kwenye mifumo ya pensheni.
Wakalipoa kodi ya nyumba kama makazi bora na kulipia watoto wao shule. Serikali inaondokana na kuhudumia mahitaji ya msingi yaliyo katika matajiri hawa kama tu uwiano wa manunuzi ya "maziwa au nyama" yataendena na uwiano kwa New Zealand
Ni namna gani tunakuwa na mkakati walau kwenye exports za maziwa na nyama kwa mwana kuna $ kadhaa zina-flow in?
If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle. - The Art of War by Sun Tzu, 6th century BC.
Adui zetu ujinga na umasikini tunawakabili kwa kiwango kipi kwa kujua kwenye equation ni sehemu ya kwanini tunakwama. Au hatujatambua hilo??
Nawaza tu.
Mungu ibariki Tanzania.