Tanzania yetu kwa sasa imekuwa na UCHWARA mwingi kuliko uhalisia

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,742
Ndio tanzania yetu kwa sasa imekuwa na UCHWARA mwingi kuliko uhalisia. Yaani unakuta mtu anayejiita mwanasiasa naye ni uchwara hamna kitu anachokifahamu vizuri au anachosimamia isipokuwa mihemko na ubinafsi. Chama nacho ni uchwara, hakina msimamo unaoeleweka au misingi ya chama kinaendana na mwenyekiti uchwara ambaye ni mwanasiasa uchwara. Ana ubepari au ujamaa uchwara. msimamo wake nao unakuta ni uchwara, elimu yake ni uchwara, maisha yake ni uchwara. falsafa uchwara na huku akijidai mzalendo uchwara.

Yaani hawa wanasiasa "ZILONGWA MBALI, ZITENDWA MBALI" Hakuna ambacho wanasimamia kinachoeleweka isipokuwa tu maslahi yao binafsi. wengine wanaenda mbali kabias na kudhani kuvaa bendera na madera, tai na vitambaa vyenye bendera ndo uzalendo huku ukiwaangalia ni very uchwara.

Hii nchi tumefikia hata wananchi nasi tumekuwa uchwara tu wabunge wanasimamia maslahi uchawara kwa kupitisha bajeti uchwara. Wanajenga hoja uchwara na kutoa misimamo uchwara kwa ajili ya ubinafsi wao tu. Inaumiza sana. Nasi tumekuwa wananchi uchwara. tunanyanyaswa maana hatuna nguvu. Tuna mapenzi uchwara. Itikadi uchwara na hata hatujali. Yani ukiangalia ni TAIFA UCHWARA NA MAMBO UCHWARA TU.

Nami nimeandika thread uchwara na kujifanya kichaa uchwara.
 
Mleta mada umenena vyema sana, wengine hufikiri kuvaa skafu au keweka bendera ya Taifa mabegani ndio uzalendo! Shame!
 
Muarobaini wa UCHWARA unadhihirika kila kukicha, HITAJI LA KATIBA MPYA mambo yawekwe sawa. Nakiri hapa kwamba CHAMA TWAWALA hakiwezi hata kidogo kutotoa UCHWARANI walikotufikisha. Vinginevyo basi tusingekua tunaelekea kuzima kwa spidi hii. Mambo ya hovyo hovyo kila kona. Kama Haiti vile.

Mwishowe sio tu kwamba amani ikitoweka tutaijutia, la hasha, Taifa litasambaratika
 
Yaani mpaka dikteta, pia tulimpata uchwara! Na nchi akaiendesha kiuchwara uchwara tu!
 
Na waleta mada hapa JF uchwara, na mada zao ni uchwara. Wachangiaji uchwara na hata wasomaji ni uchwara tu.
 
Back
Top Bottom