Tanzania yetu kuwa na watu zaidi ya milioni 200, Mungu tuepushe na gharika!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,785
Tanzania yetu ni moja kati ya nchi zinazoongoza Duniani kwa ongezeko la watu, kwa mujibu wa statista mwaka 2100 nchi yetu itakuwa zaidi ya watu milioni 200 na moja kati ya nchi kubwa kwa idadi ya watu Duniani.

Najiuliza hao watu watakula nini? Wataishi wapi na kulala wapi? Duh, sipati, nitakuwa nimeshaenda hata hivyo, nyie fyatueni tuu, kazi kwenu ukichukulia IQ haiongezeki sijui mtatua vipi matatizo, Tanzania watu zaidi ya milioni 200? Duh!

1577104673992.jpeg
 
hehee, bado vyanzo vya maji vinakuaka miti ya kukata mikaa nayo inaeisha muda si mrefu, bado ajira hakuna, wenye akili ndogo wanazaliana kwa kasi, hawajui hata kupanga kesho yao itakuwaje ila ndio wanazaliana kama sungura, mungu tuepushe na hli janga
 
Mbona nafasi za kuishi zipo nyingi tu...
Hii nchi ni kubwa sana itaweza kubeba hata milioni 500

Swala siyo nafasi ya kuishi, swala ni kwamba wataishije? Watakula nini? Kazi watafanya wapi, wataishi wapi? Kumbuka watahitaji maji ya kunywa, umeme, nyumba za kuishi, Dar ya leo tuko kwenye milioni 5 lkn inatushinda, hao milioni 250 wataishije?
 
Fyatua wewe acha uzembe, huoni hata Mwenyekiti wetu wa Taifa kubwa anasisitiza hilo maana elimu bure, viwanda bwerere na uchumi unakua kwa zaidi ya 7% na tukiwa wengi unaweza kukua hata kwa 12%

Tanzania inaweza kubeba hata watu 500mil kwasasa tuko. wachache eneo kubwa na mapoli tele hayana watu..Fyatua watoto acha uzembe wewe..
 
Bila elimu ya uzazi... Kwa kweli tunaelekea kubaya. Rate ya kuzaliana iko juu sana. Wakati wa Uhuru tulikuwa 9 million le zaidi ya 55 million.
 
Swala siyo nafasi ya kuishi, swala ni kwamba wataishije? Watakula nini? Kazi watafanya wapi, wataishi wapi? Kumbuka watahitaji maji ya kunywa, umeme, nyumba za kuishi, Dar ya leo tuko kwenye milioni 5 lkn inatushinda, hao milioni 250 wataishije?

JPM anajenga nchi wewe fyatua acha uoga, Elimu bure, maji kila kona, mabarabara ya juu, midaraja, huduma za afya bora kabisa haijawahi kutokee hospital kila mtaa, SGR, mameli, vivuko, maviwanda tele kila kona..

Fyatua Fyatua Fyatua mama tena tafuta mbegu ile ya mapacha kila mwaka unapiga wawili, wanakua miezi 6 unabeba nyingine..Nchi hii iliibiwa sana na sasa inakwenda mbele kwa speed na in 10yrs -20yrs lazima tuwe na population ya kutosha hatuhitaji wahamiaji..
 
Bila elimu ya uzazi... Kwa kweli tunaelekea kubaya. Rate ya kuzaliana iko juu sana. Wakati wa Uhuru tulikuwa 9 million le zaidi ya 55 million.

Halafu watu huwa wanaongelea mafanikio ya Botswana au Namibia kiuchumi ila wanasahau wenzetu wako wachache Namibia na Botswana wote wana watu chini ya milioni 2 wakati nchi zao zina ukubwa karibia sawa na nchi yetu.
Binafsi naamini kama sasa hivi tungekuwa chini ya milioni 10 tungekuwa mbali sana kiubora wa maisha.
 
Ukiiangalia hiyo graph hapo utagundua asilimia 80 ya hizo nchi zenye population kubwa miaka ya 1950 ndio nchi zilizokuwa na nguvu kiuchumi.

Pia ukiangalia kwenye miaka ya 2020 nchi zenye nguvu kiuchumi zimepungua kwenye hiyo graph hadi kufikia asilimia kama 50.

Ukifika mwaka 2100 zitapungua kufikia kama asilimia 30 na Africa ndio tutakuwa tunaongoza kwenye chati.

Hii inatuonesha kwamba dunia imebadilika nchi zilizoendelea sasa zinawekeza katika technolojia na si wengi wa watu. Ila Africa tusipokuwa na mipango madhubuti, Duh! sijui itakuwaje.
 
Si Mungu wenu JPM amewapa amri ya kufyatua? Fyatueni tu unalalama nini?
Tanzania yetu ni moja kati ya nchi zinazoongoza Duniani kwa ongezeko la watu, kwa mujibu wa statista mwaka 2100 nchi yetu itakuwa zaidi ya watu milioni 200 na moja kati ya nchi kubwa kwa idadi ya watu Duniani.

Najiuliza hao watu watakula nini? Wataishi wapi na kulala wapi? Duh, sipati, nitakuwa nimeshaenda hata hivyo, nyie fyatueni tuu, kazi kwenu ukichukulia IQ haiongezeki sijui mtatua vipi matatizo, Tanzania watu zaidi ya milioni 200? Duh!

View attachment 1301392

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu watu huwa wanaongelea mafanikio ya Botswana au Namibia kiuchumi ila wanasahau wenzetu wako wachache Namibia na Botswana wote wana watu chini ya milioni 2 wakati nchi zao zina ukubwa karibia sawa na nchi yetu.
Binafsi naamini kama sasa hivi tungekuwa chini ya milioni 10 tungekuwa mbali sana kiubora wa maisha.
Tungekuwa milioni 10 halafu kati ya hiyo kuna wazungu, wahindi na waarabu angalau laki 5 tu, aisee tungekuwa mbali sana
Namibia na Botswana ni minority ya wazungu ndio inawabeba. Watu weusi pekee yao ni magonjwa, njaa, umasikini na vita.
 
Halafu watu huwa wanaongelea mafanikio ya Botswana au Namibia kiuchumi ila wanasahau wenzetu wako wachache Namibia na Botswana wote wana watu chini ya milioni 2 wakati nchi zao zina ukubwa karibia sawa na nchi yetu.
Binafsi naamini kama sasa hivi tungekuwa chini ya milioni 10 tungekuwa mbali sana kiubora wa maisha.

..wana-ccm wakiambiwa "fyatua" wanawaza KUMWAGA tu, bila kufikiria kuwa baadae kuna kulea, kuuguza, kusomesha, kuoza, etc etc.
 
Watanzania wote wako hivyo wenye vyama na wasio na vyama, karibia kila house girl ana mtoto/watoto baba hajulikani au hana uwezo na wote hao ni Mabinti waliotakiwa kuwa Shuleni, angalia tu mtaani utaona kila siku wasichana wanajifungua ambao hawana hata uwezo wa kuwatunza watoto vijijini ndo usiseme.
 
Hata machangudoa zaidi ya 95% wana watoto. Huwa inaniumiza sana, nawaza ni kwanini Mungu ameruhusu machangudoa wazae lakini kuna akina mama wametulia katika ndoa zao hawajazaa?
 
Swala siyo nafasi ya kuishi, swala ni kwamba wataishije? Watakula nini? Kazi watafanya wapi, wataishi wapi? Kumbuka watahitaji maji ya kunywa, umeme, nyumba za kuishi, Dar ya leo tuko kwenye milioni 5 lkn inatushinda, hao milioni 250 wataishije?

Ni suala na siyo swala....
 
Back
Top Bottom