Tanzania YETU: Je, ni jamii ya vilaza na viongozi wa Kiimla na Ukurupukaji?

inaweza kua kweli Mkuu, inabidi viongozi wa chama wawe makini kukusanya data toka kwa wakala wao na kujumlisha wenyewe na hata kama asiposhinda basi matokeo yawe ya haki JK asijejidai kua kapata asilimia kubwa kumbe hamna.
Ikiwa hivyo Upinzani utaonekana hauna nguvu na ni njama za kuua Upinzani.

Hata nikishindwa sawa lakini kwa asilimia sahihi.
 
Kwa kufuatilia mijadala mbalimbali inaoyoendelea humu JF utagundua kuwa kuna wachangiaji wazuri wenye kuelewa maana ya Demokrasia. Hawa wanakubali ukweli pale palipo na ukweli. Kuna wachangiaji wengine hawakubali ukweli pale palipo na ukweli, za zaidi ya yote wanakuja na mambo ya kizushi ama wanapinga na kuchangia hoja kwa kuibua uzushi. Kuna wengine lugha za matusi ndiyo wanaona kitu cha kawaida.

Kwa kifupi tu, napenda kuwakumbusha wenzangu kuwa Tanzania ni Nchi yetu na sisi ni watu wake. Hatuna budi kuheshimu hilo na kila mtu yupo huru kujivunia nchi yake kwa kadri aonanvyo inafaa kwake na jinsi inavyomfurahisha. Niliwahi kupewa stori moja, ambayo kama sikosei Mjengwa wa Iringa naye alishawahi kuitoa katika gazeti (nafikiri Rai miaka ya nyuma) kuwa kuna mzee mmoja aliwahi kutoka nyumbani kwake na kijana wake wakaenda njiani ili wajaribu kuwaridhisha watu kwa matendo yao ya barabarani. Mzee huyo na kijana wake wakatoka na punda wao, hao wakitembea wakimswaga punda. Walipoenda kitambo wakakutana na watu na hao watu wakawadharau kwamba kwamba baba na mwana ni wajinga kwa kumwacha punda akitembea badala ya kumdandia awafikishe waendapo. Baba na mwana kusikia hivyo wakaamua kumpanda huyo punda. Wakaenda mbele kidogo watu waliokutana nao wakasikitika sana kwamba baba na mwana hawana huruma kwa kumpanda punda huyo wote kwani walionekana kumtesa. Basi mwana ikabidi ashuke na akamwacha baba juu ya punda na mwana akwa anamswaga huyo punda. Mbele kidogo watu wakaona hicho kitendo na kumwona yule mzee kuwa mkoloni kwani amemfanya mtoto mtumwa na yeye amemdandia punda na mwana akimswaga. Yule baba akashuka kwenye punda na akamwamuru mtoto ampande. Vivyo hivyo walipofika mbele, yule mtoto akaonekana mbele za watu kuwa hana adabu kwani amemwacha mzee akimswaga punda na yeye amempanda. Baada ya kitendo hicho yule baba akamwamuru mwanae ashuke kwa yule punda na akamwambia mwana kwa kuwa kila kitendo walichokifanya hakijamfurahisha mtu basi ni bora wamwacha punda atembee kama wao na wasisikilize mtu tena.

Mfano huo ni kuwaonesha wenzangu kuwa kila kitu mtu akifanyacho si lazima kimfurahishe mwingine. CCM kuendelea kushinda hakujawafurahisha wengi kati yetu. Chadema pia kupata ushindi mzuri kiasi hakujatufurahisha wengi pia kati yetu. Ukilijua hilo basi unakuwa ni mwanademokrasia uliyekamilika. Kwani kaa ukielewa kuwa kila ufanyacho au kikuijiacho sio lazima kimfurahishe unayepingana au unayetofautiana naye. Kwa maana hiyo hiyo ni vema kutotumia nguvu, ubabe, na chuki katika kutafuta ama kupata kila tunachokipenda au tunachokitaka sisi. Tunapokipata sisi wapo pia walioumia kwa kutokukipata. Kikukwa ni uzima na uhai. Tukuze demokrasia, tuheshimu uwepo wa nchi yetu, kwani sisi ni watu wako na tupuuze matamshi na matendo yanayoleta chuki na kusababisha upotevu wa amani na kuhatarisha nchi yetu. Uchaguzi umepita, wote tujipange kwa ajili ya mwaka 2015.
 
Iwapo kura za wananchi hazina umuhimu wowote, basi hata hakuna haja ya kuwa na uchaguzi tena nchini. Viongozi wa CCM watatuchagulia wanaowataka wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom