Tanzania YETU: Je, ni jamii ya vilaza na viongozi wa Kiimla na Ukurupukaji?

Kalamu na Mzalendohalisi nawashukuruni. tuendeleze mjadala huu kwani yawezekana tukapata majibu sahihi ya kwa nini sisi ni vilaza kama Mtoa mada alivyoita.

Ukichukua mfano wa kenya ni kwamba Kibaki hakuondoka peke yake, kulikuwa na wengi na wote walikuwa ni vigogo wanaokubalika kwenye siasa za Kenya. kilichotokea sote tunajua. Sasa sisi hapa ni tofauti. haitoshi rais kushinda bila wabunge kwa hiyo tunahitaji kikundi cha viongozi kuondoka huko. Naamini tukiweza kupata viongozi kumi kutoka ccm, Siasa za nchi yetu zitabadilika sana na as a result tutashuhudia mabadiliko makubwa ktk uchumi wa nchi yetu.
 
MzalendoHalisi:
Ninasita sana kuutumia mfano wa Kenya katika hali yetu ilivyo Tanzania. Ukabila, pamoja na hulka yao ya vuruguvurugu kila mara inatutofautisha sana kitabia na jamaa hao.
Hata hivyo, kidogo kuna mambo yanayowaendea vizuri kidogo katika uwezo wao wa kutong'ang'ania chama au serikali hicho hicho hata kama inaonekana wazi kuwa maslahi ya wananchi hayatekelezwi.
Hata kama malengo ya ubinafsi (e.g. Kalonzo Musyoka na Raila Odinga), ya kuwa rais, hata kama hawatofautiani kivyovyote kisera kunatuelekeza huko huko kwenye ulafi zaidi kuliko kuwatumikia wananchi, lakini angalao wao wamekuwa majasili kidogo, na kwa kutumia muungano wa ukabila wao (Raila, Mdavadi, Ruto, Balala, Nyaga na pengine kidogo Ngilu), wanaweza wakaleta mabadiliko ya serikali.

Kwetu hapa, viongozi waliomo ccm, wameganda huko pamoja na kuona uozo chungu nzima kwa sababu tu ya kujua tu kuwa ulaji bado upo hapo kuliko sehemu nyingine yoyote.

Tuseme wanasiasa wetu bado ni wafanyabiashara zaidi - they are risk averse!

Malawi na Zambia, hali zao sizijui vizuri kuweza kuzizungumzia. Pengine inafaa pia tujifunze kutoka huko.

CCM is still too much overbearing, until such time that it loosens its grip alittle, we'll continue with the 'self-preservation' concept.
 
Go east west mfumo wa Elimu wa Tanzania UANGALIWE UPYA.

Mtazunguka wee lakini suala linabaki palepale usomi wa watanzania unashaka sana inabidi uangaliwe upya.
watu wengi tunafikiri tatizo ni watu wa ccm si kweli , tatizo ni elimu ndogo yani(hatujaelimika) tukawa na upeo mpana wa kuweza tazama mili kadhaa.

Nikupeni mfano mdogo ambao wala si ccm bali ni upeo mdogo wa wasomi wetu japo wengine watasema nawakashifu.

Ukiomba kazi kwenye INTERNATIONAL NGO'S na ukamukuta mtanzania mwezako ndiye yupo kwenye jopo yani INTERVIEW PANNEL kwa 98% jua umeumia huna chako tena.

Kwanini kila mmoja anafahamu UPEO KIDUCHU yani elimu duni atachonga huyo kwenye pannel mpaka utashangaa mwenyewe kisa eti msilingane.

Huyo anayeogopa kutetea maslahi ya Taifa akilinda masilahi yake binafsi ndio wale wale hajaelimika ELIMU KIDUCHU hata kama ni prof ,mfano ikitokea akafa leo watoto ,wajukuu ndugu na jamaa ndio wanapotelea ktk umasikini hamjawaona hao jamani??

Kumbe angetetea maslahi ya Taifa watanzania wote wakapata standard life hata akifa bado ndugu na jamaa wataishi ktk maisha ya middle life kwani is common life to everybody.

Umasikini wa Tanzania sio ccm bali ni la watanzania wote na hii inatokana na ELIMU YA KUKALILI .
 
"Ukiomba kazi kwenye INTERNATIONAL NGO'S na ukamukuta mtanzania mwezako ndiye yupo kwenye jopo yani INTERVIEW PANNEL kwa 98% jua umeumia huna chako tena."

"Umasikini wa Tanzania sio ccm bali ni la watanzania wote na hii inatokana na ELIMU YA KUKALILI ".

Toa ushahidi wa haya usemayo. Hizi ni propaganda kuliko ukweli. Watu wanaingia kwenye International NGOs kwa competence zao na si kubebwa. Yaleyale ya Ajira BoT na Sera ya NEPOTISM.

Mbona unaitetea sisiem, Nani anatunga sera(mbofumbofu) za nchi kama si sisiem. Sera mbovu huzaa strategy mbovu na hatimaye umaskini wa Watanzania."
 
mkamap:
Sasa umetutoa katika hoja yako ya mwanzo kabisa, na umezua mambo mengine tofauti kabisa. Hapo itakuwa vigumu kuchangia maoni binafsi.

Kama ni ubovu wa elimu itolewayo Bongo, sema na watu watalijadili hilo; lakini kutokuwepo wasomi Tanzania kama ulivyochangia mwanzo, hilo nalo ni jambo tanzu linaloweza kuchangiwa kivyake; na ni hivyo hivyo kuhusika kwa ccm katika elimu hiyo; au wasomi hao.

Jitahidi uwe unapambanua mambo vizuri ili yajadiliwe sawaia.
 
SteveD,



Ndugu zangu wamekuwa wakidai kuwa hawaoni mtu mweingine wa kumpa uongozi kwa hiyo wanampa fisadi yule yule; sijawahi kuelewa maana yao kufanya uamuzi wa aina hii. Namna nyingine ya kumfunza fisadi ni kumnyima kula hata kwa kumpa nafasi fisadi mwingine lakini siyo yule yule.

Duuh!! Kichuguu, kweli tunakuhitaji hapa na mawazo yako... ulipopotea ilibidi nianzishe thread kwenye 'udhuru' kukuulizia uko wapi... lol.

Hilo uliloliongelea ukiliangalia kwa juu juu tu ni jambo tata, and if i could get away with, i would liberally call it 'practical-abstract-thinking'.

Katika ulilo ongea basi, undani wake miye nauona kuwa ni kweli ukimnyima fisadi huyu kura na kumwondoa madarakani, kisha kumweka mwingine ambaye baada ya muda naye anakuwa au anavumbulikia kuwa fisadi, mtu wa tatu atakuwa bora zaidi kuliko wa kwanza na wa pili, iwapo tu sababu za kumweka fisadi wa pili na huyu atakayekuwa wa watatu zitakuwa kupunguza ufisadi.

Nadhani hii kama mbinu moja wapo ya kuchuuja na hivyo kutakatatisha viongozi wetu inatumika, nami naikubali. Ili mladi tu 'chujio' la 'kuwafunza' mafisadi hawa linakuwa ni matundu madogo zaidi ya chujio la mwanzo.

Hivyo kuna wakati tunaweza kufikia hatua ya 'super fine' katika 'purity' ya kile tunachokitafuta (uongozi- a dream?), hata kama anayechaguliwa anakuwa fisadi- aliyepunguza ufisadi wa mara ya kwanza lasivyo asingepita kwenye nyavu ya chujio. Kwa kuwa tunapomchagua na chujio hilo 'atapita' tu iwapo anaweza kujipenyeza katika matundu yake, lakini tunaweza kumkamata ngwe ya pili maana chujio lake litakuwa na matundu madogo zaidi ya lile la mwanzo, na kuendelea ili mradi tu nyavu ya chujio letu inabakia imara...

SteveD.
 
SteveD,Kalamu,SaharaVoice,Kichuguu,...
niliwahi ku-post habari ya Non-Violence protest miaka ya 1940 ambapo wakazi wa Kilimanjaro waliandamana kupinga matumizi ya kodi yao.

Wananchi hao walimkaba koo DC wa Mkoloni na walipeleka kilio chao mpaka kwa King George!! Hiyo ilitokea Tanganyika/Tanzania Bara miaka ya 1940.

Wengi walioisoma topic yangu hapa JamboForums waliishia kuniponda kwamba nataka kuchochea maasi. Watanzania wa mwaka 2007 wanaona maandamano na mgomo wa Watanzania wa 1940 kuwa ni maasi au vurugu!!

Nafikiri Watanzania hatujui haki zetu ndani ya mfumo huu wa demokrasia tulionao. Hatujui kuishinikiza serikali kutekeleza ajenda yetu kwa kutumia mamlaka yetu ndani ya mfumo wetu wa Uongozi na Utawala.

Haitoshi kulaumu ati wananchi wanachagua mafisadi. Kama fisadi ataona mlo wake unatishiwa, kwa wananchi kumhoji kila kukicha, nakuhakikishia atatekeleza ahadi zake za uchaguzi.

Naomba wananchi tuwe macho haswa wakati wa Uchaguzi/Kampeni. Ule ndiyo wakati mzuri wa kuhojiana na kuwekana sawa. Mfano mdogo ni hii hoja ya Kadhi. Mbona hakuna aliyewahoji CCM na Kikwete wakati wa kampeni?
 
--Ni viongozi wapi wameamuru siku za hivi karibuni?!

-- Je, amri hizo zitatekelezeka?

--Kama hazitatekelezeka, kwanini waliamuru... kuonekana tu ni viongozi wakali na wanaopenda maslahi ya nchi yao (ahadi hewa) au ni kukurupuka kutokana na kutojua undani wa mambo (ulimbukeni)?

--Kama zitatekelezeka, ni kwa kiasi/kiwango kipi? Je, wangefanya nini kuboresha kiasi/kiwango hicho kabla ya kutoa hizo amri?

SteveD.
 
'Mchezo' wenu ni mauti yetu sote

Chesi Mpilipili Septemba 3, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

MTUMWA wa Kiyunani, Esopo, ametuhadithia juu ya vyura waliolazimika kuinua vichwa vyao juu ya bwawa la maji na kuwakemea watoto waliokuwa wanacheza mchezo wa kutupa mawe ndani ya bwawa hilo kuwa mchezo wao ulikuwa ni chanzo cha mauti kwa vyura hao.

'Vyura' waliomo ndani ya 'bwawa' liitwalo Tanzania wana kila sababu sasa kuinua vichwa vyao na kukemea kwa sauti kuu 'watawala' wanaotupa 'mawe' ndani ya bwawa hilo kuwa mchezo wao huo si tu chanzo cha maafa kwa 'vyura' hao bali pia hata kwa watupa mawe wenyewe ambao wengi wao wanaishi kwenye nyumba za vioo.

Kuna pia hivi vitabu mashuhuri ulimwenguni vya taasisi ya kumbukumbu ya Guinness. Lengo kuu la waanzilishi wa vitabu hivi lilikuwa kuweka kumbukumbu mbali mbali za mambo yasiyokuwa ya kawaida kwenye jamii ya wanadamu.

Kwa kawaida, kwenye vitabu hivi kuna orodha za watu wanaodhaniwa kuwa warefu zaidi kuliko wote duniani, wafupi zaidi, wanene zaidi, gari kubwa zaidi na dogo zaidi kupita yote ulimwenguni, nchi yenye watu wengi zaidi na yenye wachache zaidi kupita zote duniani na mambo mengine yenye mwelekeo wa namna hiyo.

Sina hakika kama Guinness wameishaliandika hili, lakini kwa jinsi mambo yanavyoendelea nchini mwetu, upo uwezekano mkubwa wa Tanzania kuingizwa kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Guinness na kuanzishiwa 'sifa' mpya ya kuwa nchi ambayo watawala wake wanaongoza kwa kuwafanyia mizaha mibaya kabisa raia wao.

Kwa muktadha huo huo, taasisi ya kumbukumbu ya Guiness inaweza pia kwenda mbele zaidi na kuiorodhesha Tanzania kama nchi pekee ambayo wananchi wake licha ya kunung'unikia chini chini badala ya kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya mizaha ya watawala wao, bado wanaweza kushawishiwa na watawala hao, na wakakubali, kuandamana mchana wa jua kali kuunga mkono mizaha hii.

Katika haya yote, tunapaswa tu kumshukuru Mungu kwamba tofauti na nchi nyingine ambazo raia wake wana vichwa vinavyowaka moto na mizaha mibaya ya watawala dhidi ya wananchi wao kama tunayofanyiwa ingeshughulikiwa mara moja, bado wananchi wetu walio wengi wameendelea kukubali kunyweshwa 'mvinyo' wa 'amani, utulivu na mshikamano wetu' na hivyo kushindwa kuchukua hatua zinazostahili.

Yetu ni nchi pekee ambayo mtu anaweza kuwa mjumbe wa tume inayochunguza ubadhirifu wa fedha uliotokea kwenye benki wakati huo huo yeye mwenye akawa ni miongoni mwa watu wanaochunguzwa utendaji kazi wao na tume nyingine inayochunguza mkataba wa umeme hewa ulioliingizia taifa hasara kubwa.

Mtu kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika, kwa mfano. Yeye alikuwa, na bado, ni mjumbe kwenye Tume ya kuchunguza na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya waliohusika na uchotaji wa pesa kwenye akaunti ya EPA ndani ya Benki Kuu (BoT).

Lakini pia yeye ni miongoni mwa watumishi wa umma ambao kamati ya Dk. Harrison Mwakyembe iliyokuwa inachunguza mkataba wa umeme hewa wa kampuni hewa ya Richmond, ilishauri wachukuliwe hatua kutokana na ushiriki wao kwenye mchakato mzima wa kuishauri na hatimaye kuiingiza Serikali kwenye mkataba mbovu wa kununua umeme hewa wa kampuni hewa ya Richmond.

Ama kwa kutokujua, kupitiwa ama kwa dhana ile ya 'watoto kutupa mawe bwawani bila kujali vyura watakaoumizwa', Rais Jakaya Kikwete alimjumuisha Mwanyika kuwa miongoni mwa wajumbe wa tume aliyoteua kuchunguza sakata la EPA.

Pamoja na vyombo vya habari kueleza kuhusu utata huu, hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa, Mwanyika akaendelea na shughuli kazi yake ya kuchunguza huku akichunguzwa. Huu ni mzaha mbaya kabisa dhidi ya nchi na raia wake.

Ni mzaha mbaya kama si kichekesho cha mwaka, mtuhumiwa wa uovu mmoja dhidi ya nchi na wananchi wake anayechunguzwa na tume moja kuteuliwa na mamlaka za juu kabisa za nchi kuwa mjumbe kwenye tume nyingine ya kuchunguza uovu mwingine dhidi ya nchi hiyo hiyo na wananchi hao hao! Hili linawezekana Tanzania tu.

Akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Serikali wa maazimio 23 ya Bunge, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ananogesha mambo zaidi pale alipofafanua bungeni kuhusu Mwanyika. Alisema: " … kutokana na nafasi yake kikatiba, mamlaka yake ya nidhamu ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano….

Kwa hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa miongoni mwa watendaji wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Serikali…"


Hivi ni hatua gani za kinidhamu ambazo Rais anaweza kumchukulia mteule wake huyu ambaye wiki moja kabla ya taarifa ya Richmond kusomwa bungeni na Waziri Mkuu, alimsifia yeye na wenzake kwa utendaji wao mzuri wa kazi na kuandaa ripoti nzuri kuhusu sakata la EPA wakati anakabidhiwa ripoti hiyo?

Kwa akili za kawaida kabisa, haiyumkiniki kwamba Rais anaweza kutoa adhabu kwa mteule wake kutokana na ushiriki wake kwenye kadhia moja wakati amekwisha kusifu utendaji wake mzuri wa kazi kwenye kadhia nyingine.

Jina la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwanyika linaibuka tena kwa namna nyingine wakati Waziri Mkuu anahitimisha hotuba yake. Nanukuu; "Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeanza kulifanyia kazi suala la kuimarisha Mfumo na Uwezo wetu wa ndani wa Majadiliano ya Mikataba hasa ile mikubwa ya Kibiashara na Kiuchumi na ya muda mrefu yenye maslahi makubwa kwa Taifa letu kwa kuchukua hatua mbalimbali.

"Ofisi yangu tayari imepata maoni ya wanasheria mbalimbali wakiwemo Mheshimiwa Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu; Mheshimiwa Johnson Mwanyika - Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na Mheshimiwa Nimrod Mkono, Mbunge wa Musoma Vijijini. Maoni yao yatatusaidia sana katika kuimarisha Mfumo wetu wa Majadiliano ya Mikataba. Naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge hawa kwa maoni na ushauri wao mzuri sana".

Kwangu mimi huu ni aina nyingine ya mzaha mbaya kwa wananchi. Andrew Chenge ndiye aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati nchi inaingizwa kwenye mikataba mibovu kabisa na iliyoitia hasara kubwa kuanzia ule wa TTCL, Rada, IPTL, uuzwaji wa benki ya makabwela NBC na mingineyo.

Hivi kuna ulazima wa watu kama Chenge kutajwa tena katika mazingira ya leo inapofahamika kwamba mikataba aliyosimamia yeye na ofisi yake wakati huo ndiyo majuzi ilikuja kupitiwa tena na Tume ya Jaji Mark Bomani? Kama si kinyume chake, kweli ushiriki wa watu kama hawa unaweza kusaidia kuleta mchango chanya katika "kulifanyia kazi suala la kuimarisha mfumo na uwezo wetu wa ndani wa majadiliano ya Mikataba hasa ile mikubwa ya kibiashara na Kiuchumi na ya muda mrefu yenye maslahi makubwa kwa taifa letu"?

Hivi tutaaminije kwamba watu hawa watatoa ushauri mwingine mzuri zaidi wa jinsi ya kuingia mikataba ya kimataifa tofauti na walioutumia wakati wanaishauri Serikali kuingia mikataba kama hiyo iliyoorodheshwa hapo juu ambayo mpaka leo inatuliza?

Hivi kulikuwa na ulazima gani kwa Serikali kwenda kuomba ushauri wa namna ya kuingia mikataba mikubwa ya kibiashara kwa Johnson Mwanyika ambaye tayari Kamati ya Bunge iliyoteuliwa kuchunguza sakata la Richmond ilikwisha kumtaja kuwa miongoni mwa watumishi wa Serikali wanaostahili kuadhibiwa kutokana na ushiriki wao kwenye kashfa hiyo?

La Nimrod Mkono hatuwezi kulizungumza sana hapa zaidi ya kukumbusha tu kuwa yeye ni wakili aliyekuwa akilipwa kiwango cha juu kabisa cha ada kwa ajili ya kusimamia kesi zilizokuwa zinaikabili BoT.

Ni kweli kwamba kulikuwa na ulazima sana wa kuwataja waheshimiwa hawa bungeni na kuwashukuru sana kwa maoni waliyotoa kwa ajili ya kuimarisha mfumo na uwezo wetu wa ndani wa majadiliano ya mikataba mikubwa ya kibiashara na kiuchumi?

Kwa nini hatukusikia majina mengine mashuhuri katika masuala ya sheria kama Profesa Issa Shivji? Bob Makani? Tundu Lisu? Wanasheria wetu wasomi wa kitivo cha Sheria pale Mlimani? Kwa nini hawa hawa tu?

Kwa nini tusiamini kwamba huu ni mwendelezo wa juhudi za makusudi za kusafisha na kuyaweka katika mwanga mzuri mbali na kutuzoesha sisi wananchi kuyaona hivyo majina ya watu ambao kwa namna moja ama nyingine majina yao hayakoseni kila masuala ya ufisadi yanapozungumzwa? Kwa nini tusiamini kwamba hizi ni miongoni mwa mbinu kadha wa kadha zinazotumika kuwasafisha?

Upo pia mzaha mwingine unaoudhi zaidi. Miongoni mwa kaulimbiu ambazo Serikali ya Awamu ya Nne iliingia nazo kwenye utawala ni ile ya Utawala Bora. Kinachoendelea sasa nchini mwetu ni kila kitu kasoro Utawala Bora.

Moja ya maazimio ya Bunge iliyotoa kwa Serikali Februari mwaka huu lilikuwa lile la kuitaka Serikali kuwachukulia hatua kali watendaji wake wa ngazi za juu ambao kwa namna moja ama nyingine, ushiriki wao katika kashfa ya Richmond ulichangia katika kuitia hasara nchi.

Miezi sita baadaye hatua pekee ambazo waheshimiwa hawa wamechukuliwa ni kuandikiwa barua za kutakiwa kujieleza uhusika wao katika sakata zima na kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu. Miezi sita baadaye!

Kwa serikali iliyoingia madarakani kwa 'mgongo' wa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya katika utendaji kazi wake, hili la kuchukua miezi sita kwa hatua moja tu ya kumuandikia mtu barua ya kutaka maelezo yake kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu, linatia shaka juu ya umakini wa kutaka kuwa na utawala bora. Kwa hakika, haishangazi kwa nini mambo yetu mengi yanakwama!


chesimpilipili.blogspot.com
 
EPA yageuka kaa la moto

2008-09-04
Na Muhibu Said


Hatima ya mafisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bado ni kitendawili kutokana na kila kiongozi wa serikali anayezungumzia suala hilo kukwepa kwa mbinu zote kutoa kauli mahususi kama watafikishwa mahakamani wote bila kujali kama wamerejesha fedha walizoiba au la.

Umma ukiendelea kutafakari kauli ya Rais Jakaya Kikwete bungeni hivi karibuni kwamba mafisadi wa makampuni 22 yaliyojichotea Sh. bilioni 133 za EPA wana mpaka Oktoba 31, mwaka huu wawe wamerejesha fedha hizo, vinginevyo watashitakiwa ifikapo Novemba mosi, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi, ametoa kauli inayoonyesha wazi kwamba yu gizani kwa asilimia 100 kuhusu EPA.

Akizungumza na Nipashe jana, Feleshi alisema hajui lolote kuhusu EPA na hata kama alishiriki kutoa ushauri kwa Timu ya watu watatu ya Rais inayochunguza jinai katika sakata hilo, haina maana kwamba anafahamu kuwa kuna suala EPA.

``Mimi kila mahali napoitwa kwenda kushauri nakwenda tu,`` alisema bila kuwa tayari kuingia kwa undani juu ya ushauri aliokuwa anautoa kwenye Timu hiyo na kama kuna makubaliano yoyote yalifikiwa ya kushitakiwa kwa wahusika wote wa EPA.


Feleshi alikuwa mmoja wa wataalam wa serikali waliokuwa wanatoa ushauri kwa Timu hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Wajumbe wengine ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea.

DPP huyo alisema hana la kusema kama watuhumiwa wa EPA watashitakiwa au la, kwani suala hilo liko mikononi mwa Timu ya Rais ya Kuchunguza wizi huo.

Feleshi alitoa kauli hiyo alipotakiwa kueleza sheria inasemaje iwapo mtu akiiba fedha na kisha akazirejesha.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai namba 258, kuiba ni kosa la jinai.

Hata hivyo, alisema timu hiyo inayoongozwa na Mwanyika ndiyo yenye wajibu wa kutoa maelekezo iwapo watuhumiwa hao wakabidhiwe kwa Polisi, Takukuru au katika Ofisi ya DPP kwa ajili ya mchakato wa kufikishwa mahakamani.

``Rais akishaunda timu, ni wajibu wa timu, ndiyo inayotoa maelekezo kama watu hao wakabidhiwe polisi, au Takukuru au kwangu,`` alisema Feleshi.


Kauli hiyo imetolewa na Feleshi siku chache baada ya Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndullu, kukaririwa na Nipashe akisema kwamba benki hiyo ina wajibu wa kuwashughulikia watumishi wake kwa kuwawajibisha kinidhamu tu, lakini kama kuna kushitakiwa mahakamani ni jukumu la timu ya Mwanyika.

Hata hivyo, Feleshi alisema hawezi kuzungumzia suala la watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA kwa madai kwamba, suala hilo halijafika rasmi ofisini kwake na pia, hawafahamu watuhumiwa hao na pia, hafahamu kiasi cha fedha walichoiba.

``Hilo lina wasemaji wake, kwani sifahamu ni makubaliano yapi waliyofikia, hotuba ya Rais sina, ripoti ya timu sina, ni kina nani hao na waliiba shilingi ngapi,`` alisema Feleshi.


Timu hiyo ilikabidhi ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia aliitumia kueleza Bunge kwa kirefu hatua alizochukua kutaka makampuni yote 22 yaliyoiba fedha hizo, yawe yamekwisha kuzirejesha ifikapo Oktoba 31, vinginevyo, Novemba Mosi, mwaka huu, watafikishwa mahakamani.

Suala la EPA limekuwa gumu kupata wasemaji, hata wajumbe wa Timu ya Rais inayoongozwa na Mwanyika wamekuwa wepesi kukwepa kuzungumzia sakata hilo linalodaiwa kuigharimu serikali Sh. bilioni 133 zilizochotwa kwa njia za kifisadi BoT.

Mara kadhaa, Mwanyika amekuwa bubu kuzungumzia suala hilo, ama amekataa kutoa maoni yoyote mbali tu ya kusema uchunguzi unaendelea.

Serikali kwa ujumla wake imefanya bidii zote suala hilo lisijadiliwe kwenye vyombo vya habari na kuthibitisha nia hiyo, hata makabidhiano ya ripoti ya akina Mwanyika kwa Rais Kikwete yalifanyika kimyakimya.

Awali waandishi wa habari walikuwa wamealikwa Ikulu kushuhudia makabidhiano hayo, lakini ghafla walipofika Ikulu walielezwa kwamba hafla hiyo imeahirishwa, na baadaye jioni picha na habari ya makabidhiano hayo vikasambazwa kwenye vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.


SOURCE: Nipashe
 
...it was then.
...jinamizi ulijualo...

Halikuli likakwisha...Ila sijawahi kuona watu vilaza kama wafanyakazi wa serikali ya Tanzania..

Hivi Steve Don...hivi uajiriwe serikali lazima uwe kilaza..??
 
Mara nyingi huwa najiuliza, hivi sisi tumelaaniwa? Na kama tumelaaniwa, ni laana gani hasa tuliyonayo? Ni nini hasa kinachosababisha tuwe hivi tulivyo?

Sababu kubwa za kujiuliza hivi ni kutokana na hali yetu kimaisha, ikilinganisha na wengine karibu wote duniani. Na ukizingatia uwezo wa kirasilimali tulizo nazo.

Nchi hii ina kila kitu kinachohitajika katika kuleta hali bora zaidi kwa watu wake.

1. Ina madini ya aina zote zinazoweza kupatikana duniani na zaidi (Tanzanite). Tunashindwa kuyavuna na kuamini kuwa watu kutoka nje ndio wanaoweza kutusaidia na sisi tukapata tija kwa kuwatoza 3% tu ya mapato yao. Ni nini hasa kinachotafuna akili zetu?

2. ina maji kila upande wa nchi yetu. Lakini bado mabomba yetu ni makavu na kipindupindu kinamaliza watu.

3. ina ardhi nzuri na ya kutosha kuliko nchi nyingi duniani (hakuna eneo lenye jangwa). Inatumikaje kuinua pato la mTanzania?

4. ina maliasili (hata dawa za kienyeji, misitu, mbuga za wanyama n.k.). Tunashindwa hata kuitangaza, kuitumia kupata tija. Kwanini hasa?

5. ina bahari yenye zaidi ya kilometer 1440. Maziwa yanayopakana na nchi jirani kila upande (Maziwa Tanganyika, Victoria, Nyasa). Tunayatumiaje?

6. Bahari na maziwa/mito ina samaki wa maji baridi na maji chumvi. Ila tunashindwa kuwavua, na wanaoweza kuwavua tunawakamata na hatujui tuwafanye nini.

7. Ina watu wakarimu, wenye akili na uwezo wa kufanya kazi. Kwa ujumla ina kila kitu isipokuwa hali bora kwa watu wake. Ila wote ni watazamaji, walalamikaji na wasio na fursa yoyote ya kujiendeleza kwa uhakika na usawa.

Kwa mtazamo wangu, nchi hii inakosa dira na uongozi wenye nia madhubuti ya kutumia rasilimali zilizopo katika kuleta tija. Swali ni je, kwanini pamoja na yote hayo tunashindwa kufikia malengo yetu na kudhani kuwa wahisani, matajiri duniani ndio wenye jukumu la kutusaidia kwa kile wanachopata kutoka kwao ambako wengi wao wala hawana tulichonacho hata kwa asilimia 10?

Je ni laana gani inayotusumbua sisi waTanzania? Nini hasa kinachotakiwa kufanyika kujitoa kwenye laana hiyo? Nani hasa alietutupia laana kali namna hiyo?
 
Hamna laana mimi nina jibu, jipya pengine haujawahi kulisikia, shusha pumzi kula kwanza, kama umekula relax kwa mambo mengine jibu linakuja, fanya kama unasubiri majibu ya ukimwi! baadae
 
Waberoya,

Una nondo ka za Jared Diamond au unazuga watu tu?

Duh simfahamu huyo mtu mkuu!

U mimi mwingi sana Bongo, that's it.

Mh, mkuu acha kulazimisha mambo, nimepita na haraka zangu nikaona sitaweza kuandika chochote.Hata hivyo haya ni mawazo yangu tu! hata hivyo nashukuru kwa ku-niinua hata nijisikie nina umimi. japo nakataa hiyo sifa!
 
hakuna cha laana wala nini .........aonavyo nafsini ndivyo alivyo!Watanzania tunajiona maskini sana ndani ya nafsi zetu kutwa kuomba misaada.Laana yetu iko nafsini mwetu,tubadilike ndani kwanza!
 
Back
Top Bottom