SoC04 Tanzania yenye uchumi jumuishi/uchumi wa wote

Tanzania Tuitakayo competition threads

Dingilee

Member
Jun 2, 2023
6
4
Tanzania tuitakayo ni ipi?, kwa maoni yangu Tanzania tuitakayo ni Tanzania yenye uchumi jumuishi. Yaani aina ya Tanzania yenye uchumi utakaomjumuisha kila mtu bila kujali umri, jinsia, rangi/ukabila, elimu, jiografia, historia, ulemavu, au sifa zingine. Ni aina ya Tanzania ambayo uchumi wake utaheshimu makundi yote ya kijamii; wafanyakazi, makundi tegemezi, wanafunzi, wanafamilia, wajasiriamali, wakulima na wamiliki wa biashara. Pia ni Tanzania yenye uchumi ambao kila mtu atakuwa na fursa na uhuru wa kushiriki katika mipango yake, kufaidika na fursa zake na ni endelevu, yaani ustawi wake unadumu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Andiko hili limebeba dhana hiyo ya uchumi jumuishi kwasababu mwaka huu Tanzania iko kwenye hatua za awali za kuandaa mpango wake wa maendeleo wa miaka 50 ijayo. Hivyo tuna fursa maridhawa ya kujenga aina hii ya uchumi ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini wa Jamii na Taifa letu.

Ieleweke kwamba, kama ilivyo katika nchi nyingi za kiafrika, tokea Tanzania ipate uhuru hatujawahi kupata fursa ya kukaa pamoja na kupanga mipango yetu ya kimaendeleo, haswa maendeleo ya kiuchumi. Hivyo kupitia mpango huu Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na mpango wa maendeleo wenye maono ya kila Mwananchi. Tofauti na awali ambapo mipango ya maendeleo ilikuwa ni utashi wa wanasiasa wachache na mashirika ya nje ya nchi.

Hivyo basi, ili kuifikia Tanzania hiyo, serikali, kupitia Wizara ya Mipango na Uwekezaji, ambayo ndio yenye jukumu la kupanga maendeleo yetu ya miaka 50 ijayo mwaka huu inatakiwa kuwezeshwa kuwa na timu ya watu wenye uzoefu na uwelewa mkubwa juu ya maswala ya uchumi jumuishi, ambao wataunda kamati zao za kukusanya maoni na maono ya namna ya kutengeneza Tanzania yenye Mipango ya uchumi unaojumuisha kila mtu.

Katika hatua hii, timu hiyo na kamati zao zitakuwa na wajibu wa kuzunguka kila kijiji na mtaa wa Tanzania kukusanya maoni na maono hayo. Maoni na maono hayo yanatakiwa yahusishe makundi yote yanayopatikana Tanzania ili kufikia lengo la kuwa na uchumi wa wote. Ni muhimu timu hii na kamati zake kuzunguka kila mtaa na kijiji cha Tanzania kwasababu kila sehemu ina rasilimali zake tofauti na kila sehemu ina vipaombele vyake tofauti na wengine.

Baada ya hapo timu hiyo na kamati zake, chini ya usimamizi wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, zitaunganisha maoni hayo kuwa mpango rasmi wa maendeleo ya Tanzania 2025-2075. Hapa kitu cha muhimu cha kuzingatia ni kugawa vipaombele hivyo vya maendeleo kutokana na rasilimali na vipaombele vya maeneo husika ili kuwawezesha wananchi kuwa na uhuru wa kunufaika na mipango hiyo moja kwa moja.

Baada ya hatua hiyo ni muhimu sana kuunda mifumo, sera, sheria na kanuni mbalimbali ili kuhakikisha kwamba mipango hiyo ina nguvu ya usimamizi wa kisheria, na pia inatekelezwa kulingana na makubaliano hayo rasmi kati ya wananchi na serikali. Msingi mkuu wa uundaji wa mifumo hiyo ya kikatiba, kisera, kisheria na kikanuni ni wananchi wa kila mtaa, kijiji, kata, wilaya, halmsashauri na mikoa ya Tanzania wawe huru kuzifikia na kizitumia rasilimali zinazowazunguka kujiletea maendeleo binafsi na ya nchi. Na pia kila Mwananchi awe na uelewa juu ya mifumo na fursa hizo ili kuondoa urasimu katika utekelezaji wake wa kila siku.

Tukishafanikisha hatua hizo za awali, kinachofuata ni kuwapata aina ya viongozi watakaotekeleza maono hayo. Hapa sizungumzii wanasiasa, nazungumzia maafisa watendaji na maafisa maendeleo wa vijiji, mitaa na kata zetu, nazungumzia wakuu wa idara na wakurugenzi wa halmashauri zetu, nazungumzia makatibu makhususi na watendaji kazi wao kitika kila wizara, nazungumzia Waziri Mkuu na mawaziri wake. Wote wanatakiwa kuwa na uwezo wa kutekeleza mpango huo kwa vitendo na matokea yaonekane dhahiri kwa wananchi.

Hatua hiyo haiwezi kufanikiwa bila kuwa na aina ya vyama na viongozi wa kisiasa wenye uwezo mkubwa wa kuisimamia na kuishauri serikali kutimiza wajibu wake ipasavyo. Hivyo ni muhimu kutengeneza mfumo bora wa kisheria wa kuwapata viongozi wenye uelewa, uzoefu na uzalendo mkubwa kwa nchi. Na mfumo huo ni lazima uzingatie uwepo wa demokrasia nzuri ya ndani na nje ya vyama vya siasa ili tuwapate viongozi watakaokuwa sehemu ya utatuzi wa Changamoto zitakazoikumba serikali katika kutekeleza mpango huo na si vinginevyo. Hapa nazungumzia mabalozi wa nyumba kumi, wenyeviti wa vijiji na Mitaa, madiwani, wabunge, na raisi.

Pia, utayari na uwezo wa wananchi katika utekelezaji wa mpango huo ni nguzo muhimu sana ya mafanikio. Hivyo ni lazima wananchi watengenezewe utayari wa kutekeleza mpango huo. Yaani ni lazima kila Mwananchi kulingana na ushiriki wake katika Mipango awe tayari na uwezo wa kutumia fursa zinazomzunguka kuongeza uzalishaji ili kukuza kipato binafsi na cha nchi. Kupitia hatua hii serikali itaongeza idadi ya walipa kodi watakaosaidia mipango yetu ya maendeleo kuendeshwa na vyanzo vya mapato vya ndani.

Katika kuwajengea wananchi uwezo na utayari wa kufaidika na mpango huo ni lazima wananchi kupitia vikundi, makampuni, mashirika, au wananchi kwa ubia na wawekezaji wa ndani na nje wawezeshwe kuanzisha shughuli zao kisheria kwa kuzingatia maono ya mpango huo. Na ni lazima Wizara ya Mipango na Uwekezaji iwe na mfumo mzuri wa usimamizi wa shughuli hizo. Pia ni lazima wawe wanatathmini matokeo na mchango wa shughuli hizo katika kufanikisha malengo ya mpango wetu. Lakini pia itakuwa na wajibu wa kutatua changamoto na migogoro itakayojitokeza ili kuhakikisha uimara wa taasisi hizo.

Baada ya hapo, ni muhimu shirika la kijasusi na balozi zetu watengenezewe mfumo utawapa jukumu la kutafuta masoko ya bidhaa na huduma zetu. Pia wanatakiwa kuwa na uwezo wa kubainisha na kusaidia upatikanaji wa wawekezaji wenye tija na uwezo wa kuanzisha viwanda vya ndani vitakavyokuza thamani ya malighafi zetu kwa kuzigeuza kuwa bidhaa. Hii itasaidia nchi kuongeza fedha za kigeni zitakazosaidia kurahisisha utekelezaji wa Miradi ya kimkakati, na pia itasaidia utekelezaji wa Miradi ya kijamii kama ya afya, maji, umeme, elimu, barabara n.k.

Mwisho kabisa na kwa umuhimu, ni lazima tufanyie mageuza sekta yetu ya elimu ili kuwawezesha vijana kuingia moja kwa moja katika utekelezaji na ufanikishaji wa mpango wetu. Ni lazima elimu yetu iwafanye wahitimu waweze kugeuza na kutumia mazingira na changamoto za Jamii kuwa fursa za kiuchumi. Hili liende sambamba na uimarishwaji wa sekta ya habari, teknolojia na sanaa, ambayo ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa kisasa.​

JEDWALI LA UTEKELEZAJI
PICHA MPANGO.jpeg
 
Tanzania tuitakayo ni ipi?, kwa maoni yangu Tanzania tuitakayo ni Tanzania yenye uchumi jumuishi. Yaani aina ya Tanzania yenye uchumi utakaomjumuisha kila mtu bila kujali umri, jinsia, rangi/ukabila, ufikiaji wa elimu, jiografia, historia, ulemavu, au sifa zingine. Ni aina ya Tanzania ambayo uchumi wake utaheshimu makundi yote ya kijamii; wafanyakazi, makundi tegemezi, wanafunzi, wanafamilia, wajasiriamali, wakulima na wamiliki wa biashara. Pia ni Tanzania yenye uchumi ambao kila mtu atakuwa na fursa na uhuru wa kushiriki katika mipango yake, kufaidika na fursa zake na ni endelevu, yaani ustawi wake unadumu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Andiko hili limebeba dhana hiyo ya uchumi jumuishi kwasababu mwaka huu Tanzania iko kwenye hatua za awali za kuandaa mpango wake wa maendeleo wa miaka 50 ijayo. Hivyo tuna fursa maridhawa ya kujenga aina hii ya uchumi ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini wa Jamii na Taifa letu.

Ieleweke kwamba, kama ilivyo katika nchi nyingi za kiafrika, tokea Tanzania ipate uhuru hatujawahi kupata fursa ya kukaa pamoja na kupanga mipango yetu ya kimaendeleo, haswa maendeleo ya kiuchumi. Hivyo kupitia mpango huu Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na mpango wa maendeleo wenye maono ya kila Mwananchi. Tofauti na awali ambapo mipango ya maendeleo ilikuwa ni utashi wa wanasiasa wachache na mashirika ya nje ya nchi.

Hivyo basi, ili kuifikia Tanzania hiyo, serikali, kupitia Wizara ya Mipango na Uwekezaji, ambayo ndio yenye jukumu la kupanga maendeleo yetu ya miaka 50 ijayo mwaka huu inatakiwa kuwezeshwa kuwa na timu ya watu wenye uzoefu na uwelewa mkubwa juu ya maswala ya uchumi jumuishi, ambao wataunda kamati zao za kukusanya maoni na maono ya namna ya kutengeneza Tanzania yenye Mipango ya uchumi unaojumuisha kila mtu.

Katika hatua hii, timu hiyo na kamati zao zitakuwa na wajibu wa kuzunguka kila kijiji na mtaa wa Tanzania kukusanya maoni na maono hayo. Maoni na maono hayo yanatakiwa yahusishe makundi yote yanayopatikana Tanzania ili kufikia lengo la kuwa na uchumi wa wote. Ni muhimu timu hii na kamati zake kuzunguka kila mtaa na kijiji cha Tanzania kwasababu kila sehemu ina rasilimali zake tofauti na kila sehemu ina vipaombele vyake tofauti na wengine.

Baada ya hapo timu hiyo na kamati zake, chini ya usimamizi wa Wizara ya Mipango ya Mipango na Uwekezaji, zitaunganisha maoni hayo kuwa mpango rasmi wa maendeleo ya Tanzania 2025-2075. Hapa kitu cha muhimu cha kuzingatia ni kugawa vipaombele hivyo vya maendeleo kutokana na rasilimali na vipaombele vya maeneo husika ili kuwawezesha wananchi kuwa na uhuru wa kunufaika na mipango hiyo moja kwa moja.

View attachment 3028443
✅✅✅✅
 
WORD/NENO🙌🏿
 
🙏🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom