Tanzania yenye Uchumi Imara Ripoti ya Benki ya Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yenye Uchumi Imara Ripoti ya Benki ya Dunia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Invisible, Feb 22, 2012.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  [FONT=&amp] DAR ES SALAAM, Februari 22, 2012[/FONT][FONT=&amp] – "Tanzania inaweza kuitimiza ndoto yake ya kutamani kukua haraka kupitia kutumia hazina iliyonayo Serikali, kufanya marekebisho yanayotarajiwa kwenye sekta ya elimu, pamoja na kutunga na kutekeleza sera mwafaka zinazolenga kukuza mageuzi ya mashirika mbalimbali," unasema uchambuzi wa kina ambao umefanywa karibuni na Benki ya Dunia.[/FONT]

  Mapitio ya kwanza ya uchumi wa Tanzania ambayo yamepewa kichwa: Uchumi Imara: Hazina Iliyonayo Serikali, Thamani ya Fedha Kwenye Elimu, na Mageuzi ya Kiuchumi ya Mashirika Mbalimbali ambayo imezinduliwa leo inaonyesha kwamba nchi imekuwa ikifanya vema kwa miaka kadhaa iliyopita kutokana na kutunga na kutekeleza sera zinazofaa lakini mapitio hayo yanatoa onyo dhidi ya kuridhika kupita kiasi.

  "Kutengwa kwa Tanzania kutoka masoko ya dunia kumeisaidia kuhimili misukosuko ya kiuchumi ya nje pamoja na ya kikanda ya hivi karibuni. Hata hivyo, misukosuko hiyo iliyopita haitoi hakikisho lolote kwa Tanzania la kuwa na kinga ya kiuchumi siku zijazo
  ," alionya Mercy Tembon, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania, Uganda na Burundi. "Ila Tanzania ikiendelea kuitumia hazina kubwa ya busara iliyonayo serikali na kuendelea kudumisha utengemano uliopo nchini na kuwekeza zaidi katika raslimali watu na kuwezesha maendeleo ya biashara, inaweza kulifikia lengo lake la kutamani kukua haraka katika muongo huu."

  Ripoti hiyo inatabiri kwamba Tanzania inaweza kukua kwa takriban asilimia 6 (6%) katika mwaka wa 2011/12 lakini inaongeza mara moja kwamba utendaji huu mzuri hata hivyo unaweza kuwa unawakilisha utendaji wa kiwango cha chini sana kwa sababu kiwango hicho cha utendaji kilidhihirishwa kabla kwenye miaka ya awali ya 2000 na kinaonyesha kushuka kwa utendaji ukikilinganisha na utendaji wa asilimia 7.3 na 6.5 (7.3% na 6.5%) ulioshuhudiwa baina ya mwaka 2009/10 na 2010/11. Ripoti inakumbusha kwamba kushuka huku kwa utendaji kwa sehemu kunatokana na masharti mapya yanyoonekana kuwa magumu pamoja na msimamo mkali wa kifedha, ambao umechukuliwa ipasavyo na Serikali ya Tanzania baada ya viashiria vingi kupungua sana kwenye nusu mwaka ya pili ya mwaka 2011.

  "Tanzania inatakiwa kutafuta njia mpya za kukua baada ya miaka mitatu ya upanuzi mkubwa" anasema Jacques Morisset, Mchumi Kiongozi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania. "Changamoto kubwa ni kuwezesha kuwepo msukumo mpya wa ukuzi kupitia matokeo na ujuzi vitakavyopatikana kutokana na elimu bora,vitu ambavyo hatimaye vitadumisha upatikanaji wa ajira na mageuzi ya mashirika mbalimbali."

  Mapitio ya kwanza ya uchumi wa Tanzania yanasisitiza kwamba elimu limekuwa jambo ambalo limekuwa likipewa kipaumbele kitaifa eneo ambalo Serikali imewekeza takriban asilimia 20 (20%) ya bajeti yake kila mwaka lakini changamoto nyingine itakuwa kuzalisha wahitimu wengi wakati shule nyingi zikiwa na rasilimali chache huku kukiwa na ongezeko kubwa la idadi kubwa ya wanafunzi.

  "Ili thamani ya fedha izidi kuthaminiwa zaidi, itabidi kuwepo na mabadiliko katika mgawanyo wa fedha na rasilimali miongoni mwa wilaya, itabidi pia uwezo wa walimu na usimamizi wa fedha viboreshwe, na kuwepo na ubia baina ya sekta binafsi na wazazi",
  anasema Stevan Lee, Mwandishi mwenza wa ripoti hii.

  Benki pia inahisi kwamba ishara za mageuzi ya kiuchumi zimejitokeza kutoka sekta binafsi pamoja na kutokana na maendeleo ya kiteknolojia na kielimu kama nyenzo muhimu. Mashirika madogo na ya kati kwa sasa ni vyanzo vikuu vya ajira na uzalishaji wa bidhaa za nje umeendelea kustawi tangu mwaka 2005. Ishara njema zaidi zinaweza kudumishwa kwa kuwepo sera nzuri.

  Mapitio ya uchumi wa Tanzania yatakuwa yanachapishwa mara mbili kwa mwaka na ni sehemu muhimu ya Mpango wa Uchambuzi wa Benki ya Dunia ambao una lengo la kusaidia kutoa fursa ya kuwepo mjadala unaoboresha sera baina ya wadau mbalimbali na waandaaji wa sera na kuhimiza kuwepo kwa majadiliano kuhusu masuala muhimu ya kiuchumi.


  ====================
  For English Users:

  Tanzania on Stairways to Economic Heaven – World Bank Report

  DAR ES SALAAM, February 22, 2012 – Tanzania can achieve her vision of accelerated and shared growth through the combination of fiscal prudence, cost-effective reforms in the education sector, and smart policies aimed at promoting the transformation of firms, says the latest World Bank analysis.

  The first Tanzania Economic Update titled Stairways to Heaven: Fiscal Prudence, Value for Money in Education, and Economic Transformation of Firms, launched today, shows that the country has been performing well over the past few years due to effective demand policies but warns against complacency.

  "Tanzania relative isolation from global markets has helped it to survive recent external and regional shocks. However, this resilience of the economy in the past does not necessarily guarantee immunity in the future," cautioned Mercy Tembon, World Bank Acting Country Director for Tanzania, Uganda and Burundi. "But if Tanzania continues to commit to fiscal prudence and stability and make further investments in human capital and in facilitating business development, it could reach its ambitious target of rapid and shared growth in the current decade."

  The report forecasts that Tanzania could grow at around 6 percent in 2011/12 but quickly adds that this good performance would nevertheless represent the lowest rate achieved since the early 2000s and a slowdown compared to 7.3 and 6.5 percent observed in 2009/10 and 2010/11. The report notes that this deceleration is partly the result of the new restrictive fiscal and monetary stance, rightly adopted by the Government of Tanzania after the deterioration of several indicators during the second half of 2011.

  "Tanzania needs to find new drivers of growth after three years of rapid fiscal expansion" says Jacques Morisset, the Bank's Lead Economist for Tanzania. "The challenge is to create new impulse for growth through better education outcomes and skills, which will in turn sustain job creation and transformation of firms."

  The first economic update on Tanzania underlines that education has been a national priority where the Government has invested as much as 20 percent of its budget every year, but the next challenge will be to produce more graduates with limited fiscal resources and fast growing school populations.

  "Getting better value for money will require some reallocation of fiscal and human resources across districts, improvements in teachers' capabilities and in financial management, and synergies with the private sector and parents", says Stevan Lee, co-author of the report.

  The Bank also considers that signs of economic transformation have emerged from the private sector with technological and educational improvements as main drivers. Small and medium firms are now the fastest source of employment growth and manufacturing exports have been booming since 2005. The good signs can be further encouraged by smart supportive policies.

  The Tanzania Economic Update will be published biannually and constitutes an important aspect of the World Bank's analytical program that aims at fostering a constructive policy dialogue between stakeholders and policymakers and to stimulate debate on critical economic issues.
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Nyimbo zile zile!
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  "Kuanzia 2005".


  Kwi kwi kwi kwi kwi. Wenye chuki wajinyonge. Hii imefunga midomo ya wengi.
   
 4. Ukoo Flani

  Ukoo Flani Senior Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  labda imefunga midomo watu wasiofahamu, wanaoelewa won't buy this trash.
  Marekani ni nchi ya kwanza kwa utajiri, lakini kama unafuatilia Occupy Mov't s zao utajua kuwa uchumi wa marekani unashikiliwa na 1% tu ya wamarekani wote. Tanzania nayo ni hivyo hivyo, takwimu nzuri lakini walioshikilia Uchumi wa Nchi ni kakikundi na wanajulikana kwa majina.
   
 5. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Who is Bank ya dunia? Nafikiri hapa kuna changa la macho. Nafikiri hizi ni njama mahsusi za magharibi kutuliza hasira za WaTZ juu ya utawala mbovu ukikumbatia mikataba mibovu ya madini na gesi ili waendelee kutunyonya zaidi kupitia makampuni ya nchi zao. Ukisoma gazeti la Mwananchi la jana kuna habari waliyoitoa kwenye jarida la London post la tarehe 20 mwezi huu iyayozungumzia jinsi wahisani wanavyoisifia nchi ili hali halisi ni mbaya. Sehemu ya habari hiyo inasemeka hivi:-

  "MISAADA inayoendelea kutolewa na wahisani kwa Serikali ya Tanzania imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vitendo vya ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu huku ikiwaacha wananchi wakiishi katika maisha duni na umasikini wa kutupwa.

  Madai hayo yamewekwa bayana na Jarida la The London Evening Post, la Februari 20 mwaka huu ambapo limeeleza kuwa wakati rushwa na ufisadi vikiwa vimeenea katika ngazi zote za Serikali nchini Tanzania, nchi wahisani zimeendelea kuimwagia sifa serikali ya Tanzania.

  Makala katika Jarida hilo inaeleza kuwa kuitaja Tanzania kama mfano wa kung'ara katika utawala bora na hadithi za mafanikio kwa Afrika ni jambo linaloacha maswali mengi"

  Kwa habari nzima bofya HAPA
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huko nyuma uchumi ulikuwa wa Umma, ulikuwepo? kama ulikuwa haupo tuulize tuliokuwepo. Tulikuwa maskini wa kutupwa hata kandambili za kuendea chooni tulikuwa hatuna. Tunavaa makatambuga.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uchumi haupimwi kwa makala, hupimwa kwa takwimu.

  Umaskini wa US si umaskini wa Tanzania. Maskini wa US ana jiko la supu ya bure kila siku, usifananishe makamasi na uharo, kamasi ulivyokuwa mdogo ulizilamba, uharo jee?
   
 8. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Bora humu tunaingia kwa id na majina bandia. Kama tungekuwa tunatumia picha na majina halisia basi tungedharauliana waziwazi. Sikuelewi hata chembe
   
 9. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,370
  Trophy Points: 280
  Hii ni taarifa toka kwa mshirika mnafiki.
  BD wanajua hakika namna serikali hii na iliyopita ilivyochezea na inavyoendelea kuchezea rasilimali za taifa na kufukarisha umma kwa manufaa ya kikundi kidogo cha watu 'wanaohesabika'.

  Ukiamua kuzifuatilia takwimu hizi bila kujihoji, maendeleo kwako utayasikia na kuyapigia makofi toka kwa jirani yako
   
 10. 911

  911 Platinum Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, at Sokoine Stadium Mbeya on May 01, 1995 said,'Duniani kuna watu maskini na watuwasio maskini, lakini umaskini mbaya kuliko wote ni umaskini wa mawazo - mbaya sana.Duniani kuna kutegemea, unaweza kutegemea, na kutegemea wakati wote ni kutegemea kubaya sana lakini kutegemea kuliko kote kabisakabisa ni kutegemea mtu mwinginekwa mawazo, ni kutegemea kwa ovyo sana. kunakunyima utu wako.Watu tunashirikiana mawazo lakini mawazo ambayo waziwazi ni ya kijinga lazima tuyakatae, kwa sababu mtu mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu usipoyakataa anakudharau.... udogo wa mawazo ... umaskini wa mawazo ni umaskini kupita wotekabisa kabisa ....'
   
 11. C

  Chintu JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  ..............Unaweza kupewa kichupa hivi na mtu mwenye akili akakuambia hiyo ni almasi, na anajua kuwa nawe pia una akili na unajua hicho ni kichupa na sio almasi. Lakini ukapokea na kukikubali kuwa ulichopewa ni almasi tena huku ukichekacheka kwi kwi kwi kwi kwi!!!! kama zuzu vile.
  ----Aliyekupa hicho kichupa kwa kuwa ana uhakika kuwa una akili anaishia kukudharau.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh teh, "kuanzia 2005".
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ndiyo, wameweza kuingia na kuchota mali ya taifa jinsi watakavyo, wananchi wakifukuzwa kwenye maeneo yao kama nguruwe pori, huku watetezi wao wakikenua meno bila msaada wowote. Ndiyo maana taarifa zao ni za kuwafurahisha watawala wetu waendelee kukenua menu, nchi na wananchi wake wakiteketea kwa njaa.

  Nyama ya mifupa inauzwa 5,000/=
  Mchele 2,500/=
  Sukari 2,500/=
  Unga 800/=
  Mafuta ya taa vijijini 2,500/= - 3000/=
  Dagaa 5000/=
  Mchicha fungu 1000/=

  Labda ni kwa sababu serikali imeachana na matumizi ya fedha yetu ya shilingi kwa matumizi yote ya ndani na kutumia pesa yao ya dola?

  Serikali imeshidwa kabisa kulipia huduma zake kama mishahara, elimu, madawa nk. huku miradi yote ya maendeleo inayofadhiliwa na serikali ikiwa imesimama. Moto wake utakapolipuka hiyo midomo iliyofungwa hakuna mamlaka itakayoweza kuinyamazisha.

  Mercy acha ulaghai wako kwa Watanzania na ripoti yako mbovu mbovu.

   
 14. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wasomeane wenyewe hizo ripoti huko Bungeni na wajipongeze kwa posho, hapa JF hasifiwi mtu na mawe tu hadi kieleweke!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Great, kwanini tusiondoe kikomo cha uongozi ili aendelee kufanya vizuri?
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,774
  Trophy Points: 280
  hii stori imepikwa
   
 17. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,864
  Likes Received: 2,791
  Trophy Points: 280
  Acha uongo mazeei! Makatambuga yalianza kuvaliwa miaka ya 80's baada ya kuambiwa tufunge mikanda kwa miezi 18. Kabla ya hapo mambo yalikuwa poa sana!
   
 18. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hata yule mzungu jana alivyo kuwa anasifia uchumi unakua ameona hali za watu huko Temeke, vijijini n.k au kanunuliwa?
   
 19. assa von micky

  assa von micky Senior Member

  #19
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huo uchumi unapimwa kwa kuangalia safari za raisi nje ya nchi hivyo wanafikia HITIMISHO kuwa watanzania wote tunasafiri kama mkuu wa nchi? uchumi unapimwa kwa kuangalia maisha halisi ya watu na si hizi blabla za WB......
   
 20. K

  KVM JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Wewe unasikia tu hukuona. Mwaka 1976 nilikuwa National Service Makutupora na kumalizia Mgulani - Operayion Mapambano. Mwaka mzima hakuna aliyepata kiatu ch jeshi (boot) isipokuwa "green vest ya kijani", bukta na kombati. Kiatu nilichotumia mwaka mzima ilikuwa ni " kata mbuga " baada ya safari buti nilizotoka nazo uraiani kwisha ndani ya mwezi mmoja. Fikiria kupiga kwata na safari Buti!
   
Loading...