Tanzania yenye Neema: Madini ya Almasi yagunduliwa mkoa wa Singida

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Madini ya Almasi yamegunduliwa katika mkoa wa Singida.Hayo yamesema na kamishna wa madini. Hata hivyo uchimbaji wa madini hayo mkoani hapo hayajaanza kuchimbwa.

Chanzo: Magazeti asubuhi

Rai yangu ni kwamba iwekwe mikakati thabiti kuhakikisha madini hayo yanakuwa msaada kwa watanzania sana sana mkoa wa Singida ambao ni mkoa masikini Tanzania.

Sitegemei kuona wanasiasa wanaanza kujimilikisha vitalu ili kunufaisha mitumbo yao na familia zao.
 
Singida sehemu gani?

Mwandishi Wetu
Toleo la 449
16 Mar 2016
Gazeti la Raiamwema.

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wamegundua uwepo wa madini mengi aina ya Almasi pamoja na dhahabu mkoani Singida yanayopatikana katika milima ya Kimbalaiti wilayani Iramba.
Kwa mujibu wa wakala hao ambao ni watafiti wa upatikanaji wa madini nchini na waratibu wa majanga ya asili ya jiolojia, uwepo huo wa madini kunaifanya Kanda ya Kati kushika nafasi ya pili kwa kuwa na madini mengi ukitanguliwa na Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Profesa Abdul Mruma, ameliambia Raia Mwema kuwa madini hayo yamegundulika baada ya upimaji kufanyika kwa kutumia ndege maalumu za kupimia madini chini ya ardhi.
“Tumezoea kuona almasi inapatikana Mwadui mkoani Shinyanga na maeneo ya Kahama, lakini sasa tumeweza kugundua madini ya almasi mengi mkoani Singida yanayopatikana katika milima ya Kimbalaiti wilayani Iramba,” alisema.
Professa Mruma anasema wawekezaji bado hawajahamasishwa vya kutosha ili waweze kujitokeza na kuwekeza kwenye madini yaliyopo kwenye mkoa huo ili uweze kuondokana na umaskini.
Anashauri ili kuhakikisha wananchi wananufaika na uwepo wa madini katika maeneo yao ni vyema Serikali ikatoa leseni kwa wachimbaji wadogo ambao wataweza kuingia ubia na wawekezaji wakubwa ili waweze kupata hisa ambazo zitawalipa vizuri.
‘‘Serikali ikianza kugawa vitalu hivi, mimi ninapendekeza na kuishauri igawe vitalu kwa Watanzania, pia itoe leseni kwa Watanzania ili wao waingie ubia na wawekezaji waweze kupata manufaa zaidi kuliko wawekezaji kuzitajirisha nchi zao,” alisema Professa Mruma.
Alisema wapo wawekezaji ambao hawana utalaamu wa kutosha ambao wamekuwa wakiingia mkataba na wakala wa Jiolojia hao kama washauri, nafasi hiyo pia inaweza kutumiwa na watanzania kuutumia wakala huo katika upimaji.
Wataalam na wananchi wameonya kuwa kuwepo kwa madini ya aina tofauti katika mkoa wa Singida huku mengine kama ya almasi yakiendelea kugundulika yanaweza yasilete tija kwa wananchi husika iwapo Serikali haitaweka utaratibu mzuri.
Wameonya kuwa ugunduzi huo lazima kujiepusha na makosa yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakabale mkoani Geita ambao wanazungukwa na mgodi wa dhahabu wa Geita lakini umaskini umetamalaki kwa wananchi hao. - See more at: Raia Mwema - Singida: Mkoa tajiri wa madini usiovuma
 
Ni habari njema ila suala la watanzania kupewa vitalu vya kuchimba ni muhimu sana.

Kwaujumla mimi sipendi wawekezaji katika hii sekta ya madini kwa sababu wasomi tunao. Serikali iwawezeshe kwa kuwapa mitambo ya kisasa kuchimba hayo madini ili pato kubwa liingie serikalini.

Kuliko kutegemea kodi kutoka kwa hawa wawekezaji inakuwa haina maslahi sana.

Huu ni ushauri wangu wa kama mzalendo halisi wa nchi hii yenye neema kwa Raisi Magufuli.

Lasivyo siku nyingine tutarudi hapa tukipiga kelele kama wendawazimu.
 
....mapesa mengi zaidi kuhamishiwa katika mabenki ya ulaya hasa 20%s.
NAFIKIRI KWA SASA MUDA UMEFIKA TUKAYACHIMBA WENYEWE KWA 100% BILA WABIA.
Ili tuupunguze umasikini kwa dhati.
I'll tuanze ku subsidise bidhaa za chakula na mfumuko wa bei.
 
Mwandishi Wetu
Toleo la 449
16 Mar 2016
Gazeti la Raiamwema.

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wamegundua uwepo wa madini mengi aina ya Almasi pamoja na dhahabu mkoani Singida yanayopatikana katika milima ya Kimbalaiti wilayani Iramba.
Kwa mujibu wa wakala hao ambao ni watafiti wa upatikanaji wa madini nchini na waratibu wa majanga ya asili ya jiolojia, uwepo huo wa madini kunaifanya Kanda ya Kati kushika nafasi ya pili kwa kuwa na madini mengi ukitanguliwa na Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Profesa Abdul Mruma, ameliambia Raia Mwema kuwa madini hayo yamegundulika baada ya upimaji kufanyika kwa kutumia ndege maalumu za kupimia madini chini ya ardhi.
“Tumezoea kuona almasi inapatikana Mwadui mkoani Shinyanga na maeneo ya Kahama, lakini sasa tumeweza kugundua madini ya almasi mengi mkoani Singida yanayopatikana katika milima ya Kimbalaiti wilayani Iramba,” alisema.
Professa Mruma anasema wawekezaji bado hawajahamasishwa vya kutosha ili waweze kujitokeza na kuwekeza kwenye madini yaliyopo kwenye mkoa huo ili uweze kuondokana na umaskini.
Anashauri ili kuhakikisha wananchi wananufaika na uwepo wa madini katika maeneo yao ni vyema Serikali ikatoa leseni kwa wachimbaji wadogo ambao wataweza kuingia ubia na wawekezaji wakubwa ili waweze kupata hisa ambazo zitawalipa vizuri.
‘‘Serikali ikianza kugawa vitalu hivi, mimi ninapendekeza na kuishauri igawe vitalu kwa Watanzania, pia itoe leseni kwa Watanzania ili wao waingie ubia na wawekezaji waweze kupata manufaa zaidi kuliko wawekezaji kuzitajirisha nchi zao,” alisema Professa Mruma.
Alisema wapo wawekezaji ambao hawana utalaamu wa kutosha ambao wamekuwa wakiingia mkataba na wakala wa Jiolojia hao kama washauri, nafasi hiyo pia inaweza kutumiwa na watanzania kuutumia wakala huo katika upimaji.
Wataalam na wananchi wameonya kuwa kuwepo kwa madini ya aina tofauti katika mkoa wa Singida huku mengine kama ya almasi yakiendelea kugundulika yanaweza yasilete tija kwa wananchi husika iwapo Serikali haitaweka utaratibu mzuri.
Wameonya kuwa ugunduzi huo lazima kujiepusha na makosa yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakabale mkoani Geita ambao wanazungukwa na mgodi wa dhahabu wa Geita lakini umaskini umetamalaki kwa wananchi hao. - See more at: Raia Mwema - Singida: Mkoa tajiri wa madini usiovuma

serikali inatakiwa sasa ifanye mambo kisayansi, kama kweli madini ya almasi yapo hapo singida, yapimwe ni kiasi gani, yawe mali ya serikali, ifunguliwe account maalumu kwa ajili ya hayo madini, yachimbwe na pesa itakayopatikana ifanye vitu vya maana kwa maendeleo ya nchi yetu. Kugawa vitalu kwa wazawa bado hakutasaidia sana maana wazawa hawana technology wala mitaji wataishia kuwa madalali na haohao wawekezaji kutoka nje ndio watawazidi akili wazawa na kuchukua madini yoote na kuacha mashimo tu hapo singida.
 
Hii habri imekaa kienyeji. Kwanza hakuna milima ya Kimberlite. Inaelekea mwandishi hakuelewa hata kilichokuwa kikizungumzwa na Prof. Mruma.

Pili hakuna almasi au madini ya aina yoyote unayoweza kuyapata kwa kutumia ndege (airbone survey). Ndege au chopper hutumika katika kutambua 'geological structures' au aina za miamba.

Airbone survey husaidia kutambua deep burried kimberlite pipes ambazo ndiyo huweza ku-host diamond lakini hata ukigundua kimberlite ilipo siyo lazima kimberlite hiyo iwe na diamond. Mpaka sasa Tanzania ina kimberlite pipes zilizotambulika zaidi ya 160, diamondiferous kimberlite hazifiki hata 5, na kimberlite yenye economic quantity ya diamond bado ni ile moja tu ya Mwadui.

Taarifa hii itakuwa ni ya uwongo, uwezekano mkubwa mwandishi hakuelewa kilichoongewa na prof. Mruma.

Prof. Mruma ni Mkurugenzi wa GST (Geological Survey of Tanzania). Uwezo wa GST katika utafiti wa madini ni mdogo sana. Hakuna mgodi au deposit hata moja ambayo imewahi kugunduliwa na GST. Wao hupokea tu taarifa za utafiti za makampuni binafsi ambayo huamua ni taarifa gani zipelekwe GST na taarifa gani ziendelee kuwa siri ya kampuni mpaka pale zinapoweza kuwa public bila ya kuleta madhara kwa kampuni kibiashara.
 
....mapesa mengi zaidi kuhamishiwa katika mabenki ya ulaya hasa 20%s.
NAFIKIRI KWA SASA MUDA UMEFIKA TUKAYACHIMBA WENYEWE KWA 100% BILA WABIA.
Ili tuupunguze umasikini kwa dhati.
I'll tuanze ku subsidise bidhaa za chakula na mfumuko wa bei.

Sawa kabisa Crocodiletooth baadala ya kikimbilia wawekezaji tungeshirikisha kwanza jopo la waatalamu watanzania wakakaa chini wakafanya mchaka ni jinsi gani watafanya aidha kama wanaweza patiwa mitambo wakachimba wenyewe au hata kama ni ubia ufanywe kati watanzania hasa wa eneo husika ufanywe kwa umakini sana.
 
sioni faida ya ugunduzi huo zaidi ya kuimarisha sarafu ya kaburu na maisha ya kaburu tuu..asilimia tunayopata katika hayo madini hata Tanzania yoote ichimbwe almasi maisha ya watanzania yataendelea kuwa duni tuu..mfumo mbovu hatujui thamani ya madini tunayatoa Bure tunang'ang'ania kodi ndogo ndogo..
 
Madini ya Almasi yamegunduliwa katika mkoa wa Singida.Hayo yamesema na kamishna wa madini. Hata hivyo uchimbaji wa madini hayo mkoani hapo hayajaanza kuchimbwa.

Chanzo: Magazeti asubuhi

Rai yangu ni kwamba iwekwe mikakati thabiti kuhakikisha madini hayo yanakuwa msaada kwa watanzania sana sana mkoa wa Singida ambao ni mkoa masikini Tanzania.

Sitegemei kuona wanasiasa wanaanza kujimilikisha vitalu ili kunufaisha mitumbo yao na familia zao.
Mkuu,Singida kuna kila aina ya madini isipokuwa Tanzanite tu hadi uranium ipo lkn ukiujiuliza kwa mkoa huu na ht nchi yemyewe ni maskini kiasi hiki utaishia kuumwa kichwa tu.
 
Nyie ndiyo mnagundua sahv wakati miaka mitano ikiyopita kuna jamaa yangu moja anaitwa muta alipata almasi kwenye sehemu inayotoka zircon
Sehemu moja inatwa kipuma....
 
Back
Top Bottom