Tanzania yaweka msimamo mradi wa bomba la mafuta

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,364
8,096
Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na athari zozote za kimazingira wakati wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga kwani tahadhari zote zilizingatiwa kitalaamu.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 16, 2022 ikiwa ni sehemu ya ufafanuzi ya maazimo yaliyotolewa siku tatu na Bunge la Ulaya (EU) kuhusu utekelekezaji wa mradi huo.

Kwa mujibu wa DW, bunge hilo linatoa maazimio ikionyesha athari baada ya kampuni ya bima Allianz Group, benki 15 na kampuni saba za bima (HSBC, BNP Paribas na Swiss Re) kukataa kutoa ufadhili wa kifedha kwa mradi huo kufuatia kampeni inayoendeshwa na kundi la kimataifa la 350.org.

Siku tatu zilizopita Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limetoa maazimio saba ikiwamo madai ya mradi huo kutozingatia viwango vya kimataifa katika kulinda haki za binadamu na mabadiliko ya Tabianchi, kutolipa fidia huku likishinikiza kulinda haki za wanaharakati wa mazingira,

“Wito kwa EU na jumuiya ya kimataifa kutoa shinikizo kubwa kwa mamlaka za Uganda na Tanzania, pamoja na waendelezaji wa mradi na wadau, kulinda mazingira na kukomesha shughuli za uchimbaji katika mazingira yaliyohifadhiwa na nyeti, ikiwa ni pamoja na pwani ya Ziwa Albert,”ilinukuu taarifa.

“Kujitolea kutumia njia bora zaidi kuhifadhi utamaduni, afya, na mustakabali wa jamii zilizoathiriwa na kutafuta njia mbadala kulingana na ahadi za kimataifa za hali ya hewa na bayoanuwai; wito kwa waendelezaji wa mradi kutatua migogoro yote iliyopaswa kutatuliwa kabla ya uzinduzi wa mradi huo.”

Pia Bunge hilo limeagiza kuzingatia hatari zote zinazotishia mradi huo, ikiagiza Total Energies kuchukua mwaka mmoja kabla ya kuzindua mradi wa kusoma uwezekano wa njia mbadala ya kulinda vyema mifumo ikolojia inayolindwa, nyeti na rasilimali za maji za Uganda na Tanzania.

Aidha, pia bunge hilo limeagiza kupunguza hatari ya kuathirika kwa mabonde ya maji katika ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika, ambayo ni rasilimali muhimu kwa kanda, na kuchunguza miradi mbadala kulingana na nishati mbadala kwa maendeleo bora ya kiuchumi.

Msimamo wa Serikali

Hata hivyo akitoa ufafanuzi juu ya wasiwasi huo, Makamba katika taarifa yake ya maandishi alinukuliwa akisema Mfumo wa kisheria na kibiashara wa bomba hili umeanzishwa katika Makubaliano ya mkataba kati ya mwekezaji na Nchi husika (HGA) yaliyotiwa saini Mei 20, 2021 kati ya Serikali na EACOP.

“HGA inaweka wazi uhusiano kati ya EACOP na Serikali ya Tanzania katika masuala kama vile Ardhi, viwango vya HSE (Afya, usalama, ulinzi, mazingira), utawala wa fedha, Uidhinishaji na taratibu za migogoro. Mamlaka ya Serikali ya kufuatilia mradi huu ni Ewura na NEMC,”amesema Makamba.

“Kilomita 1,147 za bomba zitakazojengwa Tanzania pamoja na temino na 4 vituo vya kusukuma maji. Bomba linahitaji upana wa mita 30 wa kulia wa njia, Bomba la kuzuia mivujo na joto la nje litajengwa kina cha mita moja, baada ya ujenzi udongo wa juu na mimea itarejeshwa na ardhi itafikiwa na watu na wanyama.”

Katika ufafanuzi wake, Makamba bomba litafuatiliwa na kebo ya hali ya juu inayoweza kugundua mabadiliko ya halijoto na mitetemo katika urefu wote wa bomba.

Amesema hakuna ardhi itakayochukuliwa na mradi bila kufanyiwa fidia zinazokadiriwa kuwa Sh23bilioni kwa wakazi 9,122.

“Utwaaji ardhi unazingatia Sheria zote mbili za Tanzania na Viwango vya Utendaji vya Shirika la Fedha la Kimataifa. Tanzania wapo Watu 9,513 walioathiriwa na mradi na 331 za kuhamishwa kwa chaguo la makazi au fidia ya pesa taslimu. Takriban asilimia 85 yao wamechagua kwa makazi na ujenzi unaendelea.

MWANANCHI
 
Ilikuwa kampeni ya Wakenya wakigoma kutoa hela tunahamia nchi zingine kwa ufadhili
 
Wazungu wanatuchezea kwasababu wanajua sisi ni omba omba, na kama mentality zetu hazijabadilika, hawawezi kuheshimu haya matamko yetu, wataendelea kutuchezea tu mpaka siku tutakapojitegemea.
 
Wataalamu “mradi umezingatia haki za binadamu na mabadiliko ya Tabianchi Ukiwa pamoja na mazingira”

(EU) bunge la umoja wa ulaya wametumia vigezo gani katika ufuatiliaji wa hayo yaliyosemwa/kutekelezwa ili kupinga huu mradi kutofanyika?wanapinga huku wakiagiza kufuata athari zinazoweza kujitokeza kutokana na huu mradi hii ni dhahiri maazimio Yao wametoa kiukandamizi .
Serikali kamatia hapo hapo kwenye msimamo kwa faida yetu Ukiwa hakuna madhara/mada hayo yakupinga mradi huo
 
Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na athari zozote za kimazingira wakati wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga kwani tahadhari zote zilizingatiwa kitalaamu.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 16, 2022 ikiwa ni sehemu ya ufafanuzi ya maazimo yaliyotolewa siku tatu na Bunge la Ulaya (EU) kuhusu utekelekezaji wa mradi huo.

Kwa mujibu wa DW, bunge hilo linatoa maazimio ikionyesha athari baada ya kampuni ya bima Allianz Group, benki 15 na kampuni saba za bima (HSBC, BNP Paribas na Swiss Re) kukataa kutoa ufadhili wa kifedha kwa mradi huo kufuatia kampeni inayoendeshwa na kundi la kimataifa la 350.org.

Siku tatu zilizopita Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limetoa maazimio saba ikiwamo madai ya mradi huo kutozingatia viwango vya kimataifa katika kulinda haki za binadamu na mabadiliko ya Tabianchi, kutolipa fidia huku likishinikiza kulinda haki za wanaharakati wa mazingira,

“Wito kwa EU na jumuiya ya kimataifa kutoa shinikizo kubwa kwa mamlaka za Uganda na Tanzania, pamoja na waendelezaji wa mradi na wadau, kulinda mazingira na kukomesha shughuli za uchimbaji katika mazingira yaliyohifadhiwa na nyeti, ikiwa ni pamoja na pwani ya Ziwa Albert,”ilinukuu taarifa.

“Kujitolea kutumia njia bora zaidi kuhifadhi utamaduni, afya, na mustakabali wa jamii zilizoathiriwa na kutafuta njia mbadala kulingana na ahadi za kimataifa za hali ya hewa na bayoanuwai; wito kwa waendelezaji wa mradi kutatua migogoro yote iliyopaswa kutatuliwa kabla ya uzinduzi wa mradi huo.”

Pia Bunge hilo limeagiza kuzingatia hatari zote zinazotishia mradi huo, ikiagiza Total Energies kuchukua mwaka mmoja kabla ya kuzindua mradi wa kusoma uwezekano wa njia mbadala ya kulinda vyema mifumo ikolojia inayolindwa, nyeti na rasilimali za maji za Uganda na Tanzania.

Aidha, pia bunge hilo limeagiza kupunguza hatari ya kuathirika kwa mabonde ya maji katika ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika, ambayo ni rasilimali muhimu kwa kanda, na kuchunguza miradi mbadala kulingana na nishati mbadala kwa maendeleo bora ya kiuchumi.

Msimamo wa Serikali

Hata hivyo akitoa ufafanuzi juu ya wasiwasi huo, Makamba katika taarifa yake ya maandishi alinukuliwa akisema Mfumo wa kisheria na kibiashara wa bomba hili umeanzishwa katika Makubaliano ya mkataba kati ya mwekezaji na Nchi husika (HGA) yaliyotiwa saini Mei 20, 2021 kati ya Serikali na EACOP.

“HGA inaweka wazi uhusiano kati ya EACOP na Serikali ya Tanzania katika masuala kama vile Ardhi, viwango vya HSE (Afya, usalama, ulinzi, mazingira), utawala wa fedha, Uidhinishaji na taratibu za migogoro. Mamlaka ya Serikali ya kufuatilia mradi huu ni Ewura na NEMC,”amesema Makamba.

“Kilomita 1,147 za bomba zitakazojengwa Tanzania pamoja na temino na 4 vituo vya kusukuma maji. Bomba linahitaji upana wa mita 30 wa kulia wa njia, Bomba la kuzuia mivujo na joto la nje litajengwa kina cha mita moja, baada ya ujenzi udongo wa juu na mimea itarejeshwa na ardhi itafikiwa na watu na wanyama.”

Katika ufafanuzi wake, Makamba bomba litafuatiliwa na kebo ya hali ya juu inayoweza kugundua mabadiliko ya halijoto na mitetemo katika urefu wote wa bomba.

Amesema hakuna ardhi itakayochukuliwa na mradi bila kufanyiwa fidia zinazokadiriwa kuwa Sh23bilioni kwa wakazi 9,122.

“Utwaaji ardhi unazingatia Sheria zote mbili za Tanzania na Viwango vya Utendaji vya Shirika la Fedha la Kimataifa. Tanzania wapo Watu 9,513 walioathiriwa na mradi na 331 za kuhamishwa kwa chaguo la makazi au fidia ya pesa taslimu. Takriban asilimia 85 yao wamechagua kwa makazi na ujenzi unaendelea.

MWANANCHI
Mbona kipindi cha JPM iwakati mradi wa Mwalimu Nyerere Hydro Power unataka kuanza yeye akiwa waziri wa mazingira alipinga na kutoa utafiti iwa athari za mazingira (environmental impact iassessment)? Moja ya vigezo vilivyotumika kumwengua kwenye uongozi; leo kwa sababu bomba linapita na kuishia mkoa wake wa asili ndio anajitokeza kukanusha kwamba bomba la mafuta halitaleta athari zozote za kiuchumi wakati akijua ya kwamba ni enzi za JPM ndio waliofanya utafiti huo na kujiridhisha kwamba athari ni ndogo ukilinganisha na faida za kiuchumi endelevu wa nchi.
 
"Asante Mwanangu January kwa kuwapasha,waende wakajitizame na vijicho vyao"
 
Hawa Wazungu hovyo kabisa. Wasituletee mambo yao ya ukoloni mamboleo! Washindwe kabisa na watokomee!
 
Mbona kipindi cha JPM iwakati mradi wa Mwalimu Nyerere Hydro Power unataka kuanza yeye akiwa waziri wa mazingira alipinga na kutoa utafiti iwa athari za mazingira (environmental impact iassessment)? Moja ya vigezo vilivyotumika kumwengua kwenye uongozi; leo kwa sababu bomba linapita na kuishia mkoa wake wa asili ndio anajitokeza kukanusha kwamba bomba la mafuta halitaleta athari zozote za kiuchumi wakati akijua ya kwamba ni enzi za JPM ndio waliofanya utafiti huo na kujiridhisha kwamba athari ni ndogo ukilinganisha na faida za kiuchumi endelevu wa nchi.
Mbongo halisi jamvini!!!! Hatari sana...
 
Back
Top Bottom