Tanzania yawa mshindi wa tuzo ya malengo ya milenia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yawa mshindi wa tuzo ya malengo ya milenia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALU-MASOLI, Sep 22, 2010.

 1. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hallow!!! wanajamii wenzangu naomba tulijadili hili suala
  .............do u think we deserve with the real situation we are having.....??


  [FONT=&quot]
  [/FONT]

  Tanzania yaibuka mshindi malengo ya milenia
  na Mwandishi wetu, New York

  TANZANIA imeshinda tuzo kwa kutekeleza vizuri malengo ya Elimu katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa yanayotakiwa yakamilishwe mwaka 2015.

  Tuzo hiyo, ilipokelewa rasmi jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye sherehe ya Tuzo za Malengo ya Milenia kwa mwaka 2010, katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria mjini New York, Marekani.

  Akipokea tuzo hiyo, Waziri Mkuu alisema itaipa moyo Tanzania kufanikiwa katika malengo yote ya milenia ifikapo mwaka 2015.
  “Ni kama mafuta ya kulainisha katika injini,” alisema huku akishangiliwa na mamia waliohudhuria tafrija hiyo.

  Tanzania imefanya vizuri katika lengo la elimu la kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shuleni, na kufikia Asilimia 95 mpaka sasa.
  Malawi nayo, imepata tuzo kwa kufanikiwa kuondoa njaa na kuwafanya wananchi wawe na chakula cha kutosha. Rais Bingu wa Mutharika alipokea tuzo ya Malawi.

  Tuzo ya Utekelezaji wa Malengo ya Milenia hutolewa na Kamati ya Tuzo, ambayo ni taasisi isiyo ya kibiashara yenye madhumini ya kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa Malengo hayo.

  Mapema, Waziri Mkuu Pinda alikutana kwa mazungumzo ya kawaida na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na baadaye mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa, Amina Salum Ali.

  Pinda yuko New York, kwa niaba ya Rais Kikwete, kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Mkutano Mkuu wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  We deserve bse tumeshinda kwa kipengele cha enrollment bila kujari kuwa kuna ambao wataambulia mimba,watakaoacha.
  Na jana tuu kwa TV kuna reaserch firm wanasema 20% ya std 7 wanaomaliza shule hawajui kusoma na kuandika vyema.
  Ubora wa elimu bado ni kitendawili
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  pia nayo ni success... at least we have won something
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  NI TUZO YA QUANTITY BUT NOT QUALITY....!

  ni kweli 95% ya watoto wanaandishwa, lakini umeona how poor the classes are..? POOR QUALITY , POOR TEACHERS, POOR TEACHING ENVIRONMENTS...!

  kwa kifupi ni UKUBWA WA PUA...but no KAMASI.
   
 5. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ebu tuwasikilize hawa wenzetu.....  [FONT=&quot]Wadau waikosoa ripoti ya malengo ya Milenia [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Monday, 12 July 2010 08:46 [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Editha Majura

  WANAHARAKATI wa maendeleo nchini, wameponda ripoti ya utekelezaji ya malengo ya milenia inayoonyesha kuwa Tanzania inaongoza Afrika katika ukanda wa Sahara kwa kutekeleza lengo la pili linalotaka kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule aende.

  Wakijadili ripoti hiyo, iliyozinduliwa nchini Marekani Juni 17 mwaka huu, wadau hao walipinga taarifa hiyo wakisema sio kweli kwani watoto wengi wanaosailiwa hawaendelei kusoma kutokana na sababu mbalimbali.

  Ripoti hiyo, ilizinduliwa na kiongozi wa Mpango wa Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), Helen Clark jijini New York, Marekani.

  Anastazia Rugaba, alisema ripoti hiyo imepotoshwa kwa kuwa taarifa ilipatikana kutoka serikalini bila kufanyiwa utafiti wa kina na kwamba zinakinzana na hali halisi.

  "Inaelekea ripoti hii imezingatia taarifa kutoka serikalini badala ya hali halisi tunayoishuhudia. Wanafunzi wengi wanaosailiwa kuingia shule za msingi au sekondari, wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na mapungufu mengi, ikiwemo uhaba wa madarasa, walimu na vifaa vya kufundishia," alisema mwanaharakati huyo.

  Mwanaharakati Mohamed Mkonongo, alisema Watanzania wenye uwezo wa kuwapeleka watoto katika shule za awali ambao wana umri kati ya miaka mitatu na mitano ni wachache, ni dhahiri kwamba mfumo wa elimu nchini unaotaka mtoto kuanza darasa la kwanza akiwa na miaka saba unaongeza tabaka la maskini na matajiri.

  Alipendekeza umri wa mtoto kuanza darasa la kwanza upunguzwe hadi kufikia angalau miaka mitano kwa sababu mtoto anaanza kujenga misingi ya ufahamu wa mambo kati ya umri wa miaka mitatu na mitano.

  Ripoti hiyo, iliyosomwa na Mwakilishi wa UNDP, Amon Manyama, inaitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za Afrika zilizoondoa ada katika shule za msingi, jambo lililoelezwa na Mkonongo kwamba ni uamuzi mzuri kutokana na mlolongo wa michango katika shule hizo.

  Naye Mkurugenzi wa Mipango ya Maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini, Bariki Kaale alisema Tanzania itapata wakati mgumu kufikia lengo la milenia la kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja.

  Alisema hali hiyo, imesababishwa na wananchi kutoshirikishwa tangu awali.

  Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Amon Mbele alisema pamoja na serikali kusaili wanafunzi wengi, imeshindwa kuwaendeleza kama vile kuwapatia na kwamba utafiti umeonyesha wanafunzi hawajatayarishwa vya kutosha kutoka daraja moja hadi lingine.

  Alisema kati ya malengo manane ya milenia, likiwemo la kupunguza vifo vya wanawake kutokana na matatizo ya uzazi na kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu moja moja, yatakuwa magumu kutekelezwa kutokana na tatizo la uwajibikaji.
  [/FONT]
   
 6. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  :becky::becky:beta samuthini zani nasini
   
 7. V

  Vaticano Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unless iwe negative news, positive development hazijadiliwi kwenye ukumbi huu.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yeah, na usishangae kuona jamaa anakuja na boasting wataki quality is not there
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  [/COLOR][/SIZE][/FONT] Tanzania imefanya vizuri katika lengo la elimu la kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shuleni, na kufikia Asilimia 95 mpaka sasa.
  Malawi nayo, imepata tuzo kwa kufanikiwa kuondoa njaa na kuwafanya wananchi wawe na chakula cha kutosha. Rais Bingu wa Mutharika alipokea tuzo ya Malawi.

  Kama hiki ndiyo kigezo kikubwa cha tuzo hii nadhani Tanzania inastahili hasa baada ya MMEM na MMES ambazo kwa kiwango kikubwa zimeongeza idadi ya vyumba vya madarasa na uandikishaji wa wanafunzi. Ila kama kungekuwa na tuzo inayoangalia kiwango cha elimu inayotolewa kwenye hayo madarasa katika maeneo ya uwezo wa wanafunzi kusoma, kuandika, kuelewa na kufanya mahesabu nadhani tusingeweza kupata hiyo tuzo.
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  WELL SAID. ndo maana hata mimi hua nashindwa kuelewa hivi hawa watu wa jf mbona hata ikiwa positive kama kuna uwezekano wakuigeuza kuwa negative hawachelewi. ndo maana siku zote huwa naishia kuwadhihaki. hatutaki kueleza ukweli. wangefanya hivi kila moja angekuwa mkweli, yaani beleshi iitwe beleshi na si kijiko. SO BORED.
   
 11. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Ukisoma documents za MMEM na MMES utaona kulikuwa na mpango mzuri tuu wa kushughulikia maswala ya elimu. Cha kusikitisha vyote hivyo vilipotelea mbali baada ya kauli kama "Tutajenga shule za sekondari katika kila kata" wakati walimu bado wanapikwa UDSM, DUCE na MUCE! Vile vile, cabinet reshuffle zinamuondoa mtu aliyesimamia dede mradi huu na kumpeleka wizara nyingine kabisa - matokeo yake momentum inapungua, lawama kibao, etc lakini kwa watu wanaoelewa hili tuzo lingekuwa dedicated kwa huyo former waziri, period!

  Yeah, I said it!!!!
   
Loading...