‪Tanzania yaunga mkono Bunge la China kupitisha uamuzi wa kutunga Sheria ya Usalama wa Taifa mkoa wa Hongkong‬

CRI Swahili

Member
Dec 21, 2013
19
42
677FD9B3-8BF9-4D6B-A622-1910D96A0F4E.jpeg


Serikali ya Tanzania imeunga mkono Bunge la Umma la China kupitisha uamuzi wa kutunga sheria ya usalama wa taifa kwenye mkoa wa Hongkong.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Bw. Hassan Abbas amesema Tanzania imekuwa ikifuatilia maendeleo ya hali ya Hongkong, na kwamba serikali ya Tanzania siku zote inashikilia msimamo wa kuunga mkono sera ya China ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", akiona kuwa ni jukumu muhimu kwa nchi yoyote kulinda usalama wa nchi na utulivu wa jamii.

Amesema Tanzania inaamini kuwa utungaji wa sheria ya usalama wa taifa kwa mkoa wa Hongkong si kama tu utakamilisha mfumo wa sheria katika kulinda usalama wa taifa, pia utakuwa msukumo wa kurejesha utaratibu wa kawaida wa kijamii mkoani Hongkong.

Bw. Abbas pia amesisitiza kuwa mambo ya Hongkong ni mambo ya ndani ya China, ambayo yanatakiwa kuamuliwa na China yenyewe. Nchi nyingine hazina haki ya kuingilia, kuchochea au kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kufanya hali ya wasiwasi izidi kuwa mbaya.
 
Haya masuala mazito ya kidiplomasia yanatakiwa kutamkwa na Palamagamba Kabudi waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom