Tanzania yaugomea Umoja wa Mataifa haki za binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yaugomea Umoja wa Mataifa haki za binadamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Dec 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  • YAKATAA SHERIA YA KUZUIA NDOA YA WAKE WENGI NA USHOGA

  SERIKALI ya Tanzania imeyakataa rasmi mapendekezo manne yaliyotolewa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu likiwamo lile lililotaka kuzuiwa kwa haki ya kuoa wanawake wengi. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema hayo mjini hapa jana alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano uliojadili vipengele 53 vya haki za binadamu kama vilivyopendekezwa mbele ya Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.


  Aliyataja mapendekezo mengine yaliyokataliwa kati ya 153 yaliyopendekezwa kuwa ni pamoja na lile lililotaka Tanzania kuwa na sheria inayoruhusu ndoa za jinsia moja (ushoga) kupiga marufuku ulipaji wa mahari na kuruhusu tohara kwa wasichana ambalo lilikwisha kukataliwa tangu mwaka 1998.


  Masaju alisema katika mkutano uliofanyika Geneva, Uswisi mwezi Oktoba, mwaka huu Tanzania ilitakiwa kukubaliana na mapendekezo hayo, lakini iliyakataa kwa kuwa hayaendani na mila na deturi za Kiafrika na zaidi ingekuwa ni kuingilia uhuru wa mtu. Alisema katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania uliridhia mapendekezo 96 kati ya 153, ambayo nayo yatapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya majadiliano ili kupata majibu ya kisera yatakayopelekwa mbele ya baraza hilo baadae.


  Pamoja na kukataa mapendekezo hayo, lakini serikali imesema kuwa haitaweza kufuta adhabu ya kifo kwa sasa kama ilivyoombwa na Watanzania wengi. Masaju alisema kuwa suala hilo ni zito na litaamuliwa tu hadi pale litakapojadiliwa kwa kina na wananchi wote hususan katika mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Tanzania daima
   
 2. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,076
  Likes Received: 7,566
  Trophy Points: 280
  It should be understood that there are human rights and Citizen's rights/customs.
  We cant adopt their resolutions as blindly as un eyed person.
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  tulichomkatalia cameron hakina tofauti na hiki.
  naunga mkono hoja mia kwa mia
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanachotufanyia hawa jamaa ni sawa na kwenda kuingilia mambo ya ndani ya famili ya mtu wakati hayamhusu. Tukitoka nje hapo swa ya ndani watuachie.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wenyewe bado wanafikiria tungali wale wale walipotuacha wakti tunapata uhuru, sasa tumepanuka kwa kiwango cha kuwatesa, wasijeshangaa wanavyogonga ukuta.
   
 6. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Jamani umasikini ni laana. Mimi nawaambieni kuwa iko siku tutakubaliana na mapendekezo yao yote!!! Kwa sasa tunajibaraguza tu lakini wakianza kuvuta majisenti yao tutalegeza tu na tutashuhudia ndoa za jinsia moja. Hiyo ni tupende tusipende, wao ndio wameishikilia dunia hii, hatuwezi kuwakwepa labda tungekuwa matajiri kama China na Japan. MTAKUJA KUNIKUMBUKA.
   
 7. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Agha gha ghaaaaa!

  Wathungu wajinga kweli kweli. Lugha yao imetawalia na hadaa kwenye nafasi ya kushindwa au kusema hapana. Hawapendi kuonyesha udhaifu. Daima watataka uonekana wewe ndo umeshindwa na ikishindikana kabisa basi uonekane wewe ndo umesababaisha wao kushindwa na si wao.

  US na UK wametikisika sana kiuchumi. Jambo hili kwa vyovyote vile lazima liathiri akiba zao za ndani na ajira. Wakati haya yakitokea tayari wamefanya ahadi za muda mrefu kusadia kifedha mifuko (WB, IMF, UN agencies, etc) na nchi maskini mbalimbali ulimwenguni.

  US ilianza kushindwa kutekeleza ahadi zake toka mwaka juzi. Nakumbuka hata awards za Grants zilipunguzwa sana mwaka jana. Na mwaka huu, kuna baadhi ya maombi yaliyoitishwa, yakashinda na kukubaliwa lakini mwisho wakapunguza idadi ya waliowazawadia na kiwango. (Chunguza kuongezwa kwa kipengele kinachosema ".....pamoja na hayo, maamuzi ya mwisho juu ya nani apewe na kiasi gani yatategemea USAID. Na USAID inayo mamlaka mwisho kufuta msaaada wakati wowote"-Tafsiri isiyo rasmi!

  UK mfumo wa "Ring-fenced budget" uliwabana sana na bado unawabana wanapotaka kupunguza fedha zilizotengwa au zinazopaswa kutengwa kwenye bajeti kwa ajili ya misaada ya maendeleo kwa nchi maskini. Mtindo huu uliwekwa kwa sheria na kuuondoa lazima wauondoe kwa kubadili sheria mbali mbali. Hili si jambo jepesi ukizingatia ukinzani katika Mabalaza na Mabunge ya UK. Njia pekee ya kubatilisha matumizi au kuzichukua pesa toka kwenye "Ring-fenced budget" ni kuonyesha kuwa walengwa wameshindwa kufikia vigezo vya kupatia fedha hizo.

  Na ili linafikiwaje?
  Kwa kuweka masharti magumu kabisa ya kinyume na maadili ya walengwa wa misaada, namaanisha kulazimisha msaada kutolewa kwa nchi zinazokubaliana na Ushoga. Hili ni sharti wanalojua fika kuwa si Afrika wala nchi maskini za bara ya Asia wataafiki. Na wasipoafiki, pesa zitabaki kapuni na itakuwa raisi kwao kujenga hoja ya kuzitumia kupunguza nakisi (deficit) ya ndani.

  Na hadhithi yangu imeishia hapo!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kiwa nini baadhi ya mapokeo, mila na desturi za kiafrika hazidonelewi kuingizwa kwenye haki za binadamu, ila za kizungu kama ushoga na ndoa?
   
Loading...