Tanzania yatandikwa bao 12 na Senegal kwenye mechi ya soka la ufukweni

Hongera una furaha isiyo na kifani as if JPM na familia yake ndo waliokuwa wachezaji


Badala ya ku analyse performance kwa siku zijazo mnaiponda. Major trick ni kujua ku recruit aina ya wachezaji wazuri kwa hii beach soccer. Siri ya msingi naiona ya mchezo huu ni kuwa na watu wenye nguvu ya kuweza kuucheza mpira na layer ya juu ya mchanga yaani tifu tifu ili kuutawala mpira kama ground ya kawaida. Kwa hiyo lazima wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira ni sifa ya kwanza, sifa ya pili ni nguvu ya miguuni ya kubeba tabaka dogo la tifutifu na mpira halafu kipaji cha soka kama kwenye soka la kawaida.

Misri waliucheza kama wako kwenye ground ya kawaida kwa ajili ya hilo. Mambo ya kila mchezaji kuanzia beki mpaka fowadi, kunyanyua kwanza afu kupiga, shabaha mbaya et.c. haiwezekani.

Bottom line ni kwamba kwenye level ya Afrika au kimataifa, sifa zote za soka la kawaida mchezaji awe nazo, alafu kwa kuongeza kupambana na layer ya mchanga tifutifu.

Namna nyingine mchezaji mwepesi sana na anayeweza kuepuka unyayo kuzama anaweza kuwa na faida, lakini awe na skills za Ninja wa martial arts, otherwise, hakuna short-cut, ni mpira mgumu tu kama mingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom