Tanzania yatakiwa kuridhia Sheria ya Wafanyakazi wa Majumbani no 189

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
d696fb9feff68286160e58ba8a180143.jpg

Serikali imetakiwa kuridhia na kupitisha mkataba wa kimataifa wa wafanayakazi wa majumbani namba 189 wa kazi zenye staha wa mwaka 2011 ili kuwezesha haki za wafanyakazi wa majumbani zifatwe kisheria.

Mkataba wa wafanyakazi wa majumbani ulipitishwa tarehe 16/6/2011 na shirika la kazi duniani ILO huko Geneva Switzerland ambapo hadi sasa aslimia kubwa ya nchi hazijaridhia mkataba huo ikiwemo Tanzania.
Hata hivyo katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi wa majumbani Watanzania wameungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo ambapo endapo mkataba huo utaraidhiwa utakuwa ni suluhisho kwa matatizo ya wafanyakazi.

Akizungumza na wafanyakazi wa majumbani Mwenyekiti wa wanawake kutoka chama hicho ATUPAKISYE MTAFYA amesema kuwa endapo mkataba huo utaridhiwa na kupitishwa itakuwa chachu ya mabadiliko kwa wafanyakazi wa majumbani ikiwemo kupata haki zao za msingi .

Nao baadhi ya wafanyakazi wa majumbani wameiomba serikali kuitambua rasmi kada hiyo katika kuchochea uchumi wan chi huku wakieleza changamoto wanazokumbana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao
 
Mkuu hili suala limepuuzwa miaka mingi sana.Wengi wameumia sana na jambo hili.Halafu wakimaliza na hili WAMULIKE PIA VIWANDANI.kuna watu wanalipwa hadi 3500 kwa siku huku viwandani.
 
Back
Top Bottom