Tanzania yataka amani Afrika ili kupunguza mzigo wa wakimbizi nchini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1581315007042.png

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta amani katika maeneo yenye migogoro Barani afrika hususani katika Nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuipunguzia Tanzania mzigo wa wakimbizi ulioubeba kwa muda mrefu hivi sasa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani ameyasema hayo katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 33 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Nchini Ethiopia ambapo ameongeza kuwa kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ya kunyamazisha silaha (silencing the gun) umekuja wakati muafaka kwa kuwa mapigano na kutokuwepo utulivu katika baadhi ya nchi za Afrika zinachelewesha maendeleo katika Bara hilo.

Ameongeza kuwa endapo Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa zitaongeza nguvu katika kunyamazisha silaha na kukawepo amani na utengamano,ni dhahiri viongozi wataelekeza nguvu kubwa katika maendeleo endelevu ya wananchi na hivyo kupunguza umasikini katika Bara la Afrika ambalo linaonekana kama Bara lililoghubikwa na migogoro na mapigano.

Mhe. Samia Suluhu Hassani pia ameuahidi Umoja wa Afrika kuwa Tanzania itatekeleza kwa kasi mpango wa Umoja huo katika Mapambano dhidi ya Malaria na kwamba Tanzania imedhamiria kuutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

Katika Mkutano huo wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wameshuhudia mabadilishano ya uenyekiti ambapo Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mhe.Abdel Fattah el-Sisiambae pia ni Rais wa Misri amekabidhi Uenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini Mhe. Cyrill Ramaphosa ambae anakuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika.
 
wanatangaza amani huku wameficha mapanga-Prof. J(Kipi sijakisikia song).

dodge
 
Kwani wao si ndio wanahatarisha amani huku kwetu? Si ndio wanapiga watu marisasi? Si ndio wanatangaza kuwa watu wauwawe? Au sio hawa? Maaajabu ya dunia kwakweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
beth umenikumbusha wimbo wa professor Jay.
"Wanatangaza amani huku wamebeba mapanga" Tuzidi kuiombea Dunia iwe sehemu salama ya kuishi kwa Amani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom