Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye ongezeko kubwa la watu wenye matatizo ya afya ya akili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye ongezeko kubwa la watu wenye ugonjwa wa akili ambao wataalamu wa afya ya akili wanasema unarudisha kwa kasi ari na ufanisi wa utendaji kazi na uzalishaji katika maeneo mengi ya kazi.

Akitoa tathmini ya matatizo ya akili nchini wakati wa Maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha,Katibu wa Chama cha wataalamu wa afya ya akili nchini Tanzania MEHATA bi.Tasiana Njau anasema iwapo hali hiyo haitadhibitiwa mapema itaathiri kufanikisha azma ya serikali ya kufikia kwenye uchumi wa kati.

Joyce Felix ni Mratibu wa afya ya akili mkoa wa Arusha anasema katika mkoa huo katika kipindi cha miaka mitatu kuna wagonjwa zaidi ya elfu sitini waliopatiwa matibabu changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa wataalamu wa tiba hiyo.

Akizungumza katika Maadhinisho hayo Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Edna Munisi anasema serikali utaendelea kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje kutoa tiba ya magonjwa hayo na hapa anatoa angalizo kwa waajiri kuepuka kuwanyanyapaa watumishi wenye matatizo ya afya ya akili.

ITV
 
Tasiana Njau anafuata nyayo za yule Dokta wa NIMRI aliyetoa tamko kwa niaba ya Waziri wa Afya. Aangalia wasimgeuze kuwa jipu.
 
Mfano mzuri wa kipimo cha ufanisi wa akili za watanzania ni hapa JF

Angalia michango ya wapenzi wasiasa hususan watetezi wa ccm.....utapata majibu mubashara kabisa.
 
Aaah lazima iongoze tu kwa sababu kwenye familia baba ndie anayetazamwa zaidi ya watoto.
 
Back
Top Bottom