Tanzania yasuasua katika maendeleo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Tanzania yasuasua katika maendeleo

na Ratifa Baranyikwa na Mkolo Kimenya
Tanzania Daima

TANZANIA bado inasuasua katika kufanya vizuri kwenye masuala ya mazingira ambapo kwa mwaka huu imeshika nafasi ya 159 kati ya nchi 177.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa, iliyozinduliwa jana na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Profesa Mark Mwandosya, kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Mratibu Mkazi wa UN, Oscar Fernandez-Taranco, ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), alisema kuwa kwa mwaka huu Tanzania imefanya vizuri ukilinganisha na ripoti ya mwaka jana, iliyokuwa ikizungumzia masuala ya maji, ambapo Tanzania ilishika nafasi ya 162.

Fernandez alisema kuwa ripoti hiyo inatoa changamoto tano ambazo ni ishara zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo Tanzania na dunia kwa ujumla zimeanza kuonekana.

Changamoto zilizoainishwa katika ripoti hiyo ni pamoja na kutokuwa na kilimo kinachozalisha na kutokuwepo kwa chakula cha kutosha, uhaba wa maji na kutolinda vyanzo vya maji, kuongezeka kwa kina cha bahari, hali inayosababishwa na kuyeyuka kwa barafu, kuongezeka kwa magonjwa yanayoongoza kwa vifo kama malaria, pia ongezeko la joto duniani.

Akizindua ripoti hiyo, Profesa Mwandosya alisema kuwa uchumi wa Tanzania unategemea sana hali ya hewa.

Profesa Mwandosya alisema kuwa mabadiliko yanayoonekana hivi sasa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyeyuka kwa barafu ya Mlima Kilimanjaro, licha ya kutishia watalii na watu wanaozunguka mlima huo, husababisha hali ya uchumi kushuka.

Aidha, alisema kuwa kuongezeka kwa kina cha bahari hususani katika Wilaya ya Bagamoyo, husababisha ukosefu wa maji salama. Pia mgawo wa umeme ulioikumba nchi mwaka 2005 nao ulikuwa pigo na kuacha ukweli kuwa Tanzania inahitaji kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

Alisema kuwa rasilimali zinazotokana na mazingira ikiwamo kilimo, utalii, uvuvi, misitu na maji, ndiyo tegemeo la maisha ya watu walio wengi hasa katika nchi zinazoendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom