Tanzania yashtushwa na hali ya uvunjifu wa amani kwenye Uchaguzi wa Marekani

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,613
Serikali ya Tanzania imeonyesha wasiwasi wake kufuatia taarifa za wizi wa kura na ukosefu mkubwa wa amani kufuatia fujo na uharibifu wa mali uliotokea katika baadhi ya maeneo na miji nchini humo.

Tanzania pia imesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi huo kujitangazia ushindi kinyume cha taratibu jambo linalochangia kuzuka kwa fujo na uvunjifu wa Amani, na kuitaka serikali ya Marekani kuhakikisha kwamba haki na demokrasia inatawala katika kipindi chote cha uchaguzi.

Tanzania inaendelea kufuatilia kwa makini uchaguzi huo na kuzitaka pande zote husika kujizuia na vitendo vyovyote vyenye kusababisha uvunjifu wa Amani.
 
bila kusahau "serikali ya Tanzania haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaovuruga uchaguzi USA na kama vitendo hivyo ovu vitakidhiri basi serikal ya Tanzania itaiwekea vikwazo vya kiuchumi USA".

Niko usingizini, nafikiri naota.
 
Baada ya nyinyi kuiba kura bila aibu mumeshaanza kushutumu nchi zingine eti wameiba kura? Nyani haoni kundule
Wacha kupanic wakati baba wa East Africa anaanza kukaripia mabwana zenu, Tanzania haiwezi kuzungumzia shutuma za kijinga kama hizo zisizokua na ushahidi wowote, inachokaripia ni kitendo cha Trump kujitangazia ushindi kabla ya tume ya uchaguzi kutoa matokeo rasmi.

Tabia ya kulalamika kuibiwa kura bila kuwa na ushahidi ni tabia ya watu wajinga wanaposhindwa uchaguzi popote pale duniani
 
Hivi Marekaki ambao ni mabwana wa wapinzani Tanzania hawawezi Fanya uchaguzi kwa amani na uadilifu? mnataka Tanzania iwafunze democrasia? Takataka nyie
Wewe nawe tukuite bibi wa mafisiem takataka wewe mwenyewe.Rafu zipo kila sehemu ktk mechi tatizo lenu mnajifananisha na marekani wkt huku tume ni yenu haichukui hatua mkifanya makosa nyinyi ila inaona makosa ya wapinzani wenu tu.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaovuraga uchaguzi wa raisi nchini Marekani. Pia Serikali ya JMT inasisitiza uwazi wa zoezi zima la uchaguzi.
 
Serikali ya Tanzania imeonyesha wasiwasi wake kufuatia taarifa za wizi wa kura na ukosefu mkubwa wa amani kufuatia fujo na uharibifu wa mali uliotokea katika baadhi ya maeneo na miji nchini humo.

Tanzania pia imesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi huo kujitangazia ushindi kinyume cha taratibu jambo linalochangia kuzuka kwa fujo na uvunjifu wa Amani, na kuitaka serikali ya Marekani kuhakikisha kwamba haki na demokrasia inatawala katika kipindi chote cha uchaguzi.

Tanzania inaendelea kufuatilia kwa makini uchaguzi huo na kuzitaka pande zote husika kujizuia na vitendo vyovyote vyenye kusababisha uvunjifu wa Amani.
Mfyuuuuu %$374%2$-9744*!(&5 period.
 
kbs
bila kusahau "serikali ya Tanzania haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaovuruga uchaguzi USA na kama vitendo hivyo ovu vitakidhiri basi serikal ya Tanzania itaiwekea vikwazo vya kiuchumi USA".

niko usingizini, nafikiri naota.
 
Back
Top Bottom