Tanzania yashiriki kikao cha pili cha mkutano mkuu wa 27 wa umoja wa Posta Duniani

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
594
500
Abidjan. Ivory Coast
Katibu Mkuu ,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bwana Amour Hamil Bakar wamehudhuria kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani unaoendelea jijini Abidjan,Ivory Coast.

Mkutano huu , pamoja na mambo mengine Utafanya Uchaguzi wa viongozi wakuu wa Umoja huo ambao ni Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 25 Agosti,2021 .
Wanaowania nafasi za Mkurugenzi Mkuu ni Bw. Pascal Clivaz kutoka nchi ya Uswiss, Bwana Jack Hamande kutoka Ubelgiji na Bwana Masahiko Metoki kutoka Japan.

Wanaowania nafasi ya Unaibu Mkurugenzi Mkuu ni BiMarcela Maron wa Ajentina , Bwana Younouss Djibrine,Kameruni ,Bwana Marjan Osvald, wa Slovania na Vladyslav Dubenko wa Ukraine.

Mkutano Mkuu huo pia utachagua wajumbe wa mabaraza ya Umoja huo, yaani Baraza la Utawala na Baraza la Uendeshaji katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 26 Agosti,2021.

Imeandaliwa na:

Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom