Tanzania yashinda tuzo ya mdg kwa kufanya vizuri katika elimu

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

*

Tanzania imeshinda tuzo kwa kutekeleza vizuri malengo ya Elimu katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa yanayotakiwa yakamilishwe mwaka 2015.*

Tuzo hiyo ilipokokelewa rasmi jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye sherehe ya Tuzo za Malengo ya Milenia kwa mwaka 2010, katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria jana (Jumapili Sept. 19, 2010) mjini New York, Marekani.

*

Akipokea tuzo hiyo, Waziri Mkuu alisema tuzo hiyo itaipa moyo Tanzania kufanikiwa katika malengo yote ya Milenia ifikapo mwaka 2015.

*

“Ni kama mafuta ya kulainisha katika injini,” alisema huku akishangiliwa na mamia waliohudhuria tafrija hiyo.

*

Tanzania imefanya vizuri katika Lengo la Elimu la kuhakikisha Watoto wote wanaandikishwa shuleni, na kufikia Asilimia 95 mpaka sasa.*

Malawi nayo imepata tuzo kwa kufanikiwa kuondoa njaa na kuwafanya wananchi wawe na chakula cha kutosha. Rais Bingu wa Mutharika alipokea tuzo ya Malawi.*

Tuzo ya Utekelezaji wa Malengo ya Milenia hutolewa na Kamati ya Tuzo, ambayo ni Taasisi isiyo ya kibiashara yenye madhumini ya

*kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa Malengo hayo.

*

Mapema, Waziri Mkuu Pinda alikutana kwa mazungumzo ya kawaida na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Dk. Asha-Rose Migiro na baadaye Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Amina Salum Ali.

*

Mhe. Pinda yuko New York, kwa niaba ya Rais Kikwete, kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Mkutano Mkuu wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia.

(mwisho)

Imetolewa na:

********* Ofisi ya Waziri Mkuu,

********* S.L.P. 3021,

********* DAR ES SALAAM

Jumatatu Sept. 20, 2010

*
 
Tanzania imefanya vizuri katika Lengo la Elimu la kuhakikisha Watoto wote wanaandikishwa shuleni, na kufikia Asilimia 95 mpaka sasa.*

Kuandikishwa ni sawa, je quality ya elimu inayopatikana imekuwa asessed?...Je kuna madawati mashuleni, je kuna walimu..je walimu kama wapo wana nyumba?

That remains a myth!
 
Kiujumla, Tanzania na Burundi ndio ambao MDG hazijatekelezwa kama ilivyokusudiwa ukilinganisha na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda.
 
Hata nyie mnatakiwa kuchangia madawati shuleni si lazima wizara ya elimu tuu!
Mimi nimepeleka madawati 200 katika shule 5 tofauti jijini Dar es salaam kwa mwaka huu wa 2010(si vyema kuzitaja hapa),nanyi fuateni moyo huo!
 
Kuna mwenye chanzo kingine cha habari zaidi ya hii na michuzi, We have to see the details maana hii serikali yetu hawaaminiki kabisa!
 
He makubwa!! Tumefanya vizuri.........!!!!!:lalala:

Wanaoshindanisha hawako serious hata kidogo, Tanzania na Malawi . Tanzania mafanikio Elimu , Malawi mafanikio kuondoa Njaa na chakula cha kutosha.

Watoke kwenye ofisi zao waje field waone tofauti na ripoti zao na realities.

Nashangaa na sisi tumepokea zawadi hiyo naomba yale madarasa ya kuchekesha chini ya mbuyu yatumwe kwenye web ya MDG wajione hawajui kazi.
 
wazungu wanapenda sana tuendelea na mandondocha tulio nao, kwani marais mandondocha ndo kula ya wazungu
 
Nchi yetu kufikia ufanisi bado kabisa. Hatuna budi kuvuta socks kwa malengo. wenzetu wa Rwanda dalili njema
BBC asubuhi ilitoa habari kuwa wameshaanza kusambaza laptops kwa kila mwanfunzi nchini mwao. Tanzania hiyo itawezekana???????????.
Kweli tuache blaa blaa, Tuamue kufanya changes na changes huanzia kwenye fikra zetu!! TUONDOE UONGOZI DHALIMU

BILA NCHA YA UPANGA AMANI YA KWELI HAIPO! LETS FIGHT FOR CHANGE, LETS VOTE FOR SLAA AND STAND FIRM WITH HIM
 
Hongera Tz kwa tuzo hii, ni suala la kujivunia. Ripoti nyingi za umoja wa mataifa zinasema kuwa Tz tunajitahidi that it is encouraging, though wa ndani tunachonga sana but hata Yesu alisema nabii huheshimika isipokuwa nyumbani kwao. Suala la enrollment ni lingine na quality ni jingine.
 
Subiri kesho (jumanne), itakapotoka ripoti ya utafiti juu ya ubora wa elimu Tanzania ndio mtajua tatizo lilivyo kubwa na kuwa hata hiyo tuzo hatustahili kabisa!!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

*
Mapema, Waziri Mkuu Pinda alikutana kwa mazungumzo ya kawaida na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Dk. Asha-Rose Migiro na baadaye Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Amina Salum Ali.

*

(mwisho)

Imetolewa na:

********* Ofisi ya Waziri Mkuu,

********* S.L.P. 3021,

********* DAR ES SALAAM

Jumatatu Sept. 20, 2010

*


Huyu Asha-Rose Migiro ni mwanachama wa CCM - maana CCM wana tentacles hadi UN ati! Isije ikawa kuna mkono wake hapa.
 
Hongera Tz kwa tuzo hii, ni suala la kujivunia. Ripoti nyingi za umoja wa mataifa zinasema kuwa Tz tunajitahidi that it is encouraging, though wa ndani tunachonga sana but hata Yesu alisema nabii huheshimika isipokuwa nyumbani kwao. Suala la enrollment ni lingine na quality ni jingine.

WANAFUNZI12.jpg
 
Statistics, Tanzania, United Republic of
* Total population (millions): 38.3
* Population growth (annual %): 2.0
* Surface area (sq. km): 945,087
* GDP per capita (PPP US$): 730
* GDP growth (annual %): 5.9
* Inflation, GDP deflator (annual %): 6.3
* Unemployment (% of total labor force): N/A
* Life expectancy at birth (years): 49.7
* Median age of total population (years): 17.5
* Human Development Index (Rank 1 - 177): 162
* Human Development Index Value: 0.4
* Sex ratio at birth (males per 100 females): 103.0

MDG GOALS
Goal 2: Achieve universal primary education
* Net enrollment ratio in primary education (% both sexes): 98.0
* Percentage of pupils starting Grade 1 and reach Grade 5 (% both sexes): 82.8

Goal 3: Promote gender equality and empower women
* Gender parity Index in primary level enrollment (ratio of girls to boys): 1.0
* Literacy rates of 15-24 years old (% both sexes): 77.5
* Seats held by women in national parliament (%): 30.4

Goal 4: Reduce child mortality
* Mortality rate of children under 5 years old (per 1,000 live births): 118
* 1-year-old children immunized against measles (%): 93

Goal 5: Improve maternal health
* Maternal mortality ratio (per 100,000 births): 950

Goal 6: Combat HIV/AIDS, malaria and other diseases
* People living with HIV,15-49 yrs old (%): 6.2
* Prevalence of tuberculosis (per 100,000 people): 459

Goal 7: Ensure environmental sustainability
* Land area covered by forest (%): 39.9
* Carbon dioxide emissions per capita (metric tons): 0.1160
* Access to improved drinking water sources (% of total population): 55

Goal 8: Develop a global partnership for development
* Internet users (per 100 people): 1.0
 
Katika malengo 8 ya MDG's (maendeleo ya melinia), ni lengo 1 kati ya 8 (1/8) Tanzania tunaweza kufanikiwa ifikapo 2015.

Majirani zetu ni kama ifuatavyo, Rwanda 6/8, Ethiopia 6/8, Uganda 3/8, Zambia 3/8, na Kenya 1/8.

Maana yake nini? :confused2: Katika mkakati wa nchi kufikia malengo ya MDG ifikapo 2015, Tanzania na Kenya ni nchi za mwisho East Africa.

Source: MDG Monitor: Quick Facts

My take, PM should have just stayed at home, the money saved from the cost of his (plus wapambe) trip to NYC could have been used to provide "madawati" and "delivery tables" to some schools and dispensaries in Rukwa. Such decisive actions to cut down on unproductive trips by our leader and put the money into better use will contribute substantially towards achieving some of MDG in 2015.
 
* Literacy rates of 15-24 years old (% both sexes): 77.5

Hii data sidhani kama ni kweli, na hata kama ni kweli si ya kujivunia hata kidogo!!!!!!
 

Makubwa haya! Wanafunzi hawana madawati, walimu hakuna, vyumba vya madarasa ndiyo kama hivi na wengine hukaa chini ya miti na bado tumeshinda! Sijui ni vigezo gani vilivyotumika katika huo ushindi wetu wa kushangaza.
 
Swala la selection tu limewashinda bado wanapewa tunzo eeejaman siasa kwel ni mchezo mchafu
 
Back
Top Bottom