Tanzania yashikilia nafasi ya 7 kwa kuvutia kwa uwekezaji Afrika

Nina uhakika hakuna mwekezaji hata mmoja wa maana tangu awamu hii iingie. Anayebisha, ataje makampuni makubwa yaliyowekeza katika awamu hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio uweke ushahidi kuwa hakuna uwekezaji wa maana. Usitumie hisia alafu unataka watu wakuwekee ushahidi kwa kitu cha hisia zako.
 
Wewe ndio uweke ushahidi kuwa hakuna uwekezaji wa maana. Usitumie hisia alafu unataka watu wakuwekee ushahidi kwa kitu cha hisia zako.
Kwenye orodha ya vitegauchumi katika awamu hii, hakuna mwekezaji hata mmoja aliwekeza mtaji wa kufikia U$500m. Hayupo hata mmoja. Sizungumzii hisia, mimi nazungumza kwa takwimu. Mwekezaji mkubwa wa mwisho alikuwa Dangote ambaye alipoanza aliwekeza U$700m.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye orodha ya vitegauchumi katika awamu hii, hakuna mwekezaji hata mmoja aliwekeza mtaji wa kufikia U$500m. Hayupo hata mmoja. Sizungumzii hisia, mimi nazungumza kwa takwimu. Mwekezaji mkubwa wa mwisho alikuwa Dangote ambaye alipoanza aliwekeza U$700m.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ziko wapi hizo takwimu?
Acha kutumia hisia.
 
Benki ya Rand Merchant (RMD), Benki ya huduma za kifedha ya Afrika Kusini imewasilisha orodha ya nchi 10 zinazovutia zaidi kwa wawekezaji mwaka 2019. Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo ikiwa imeshika namba 7 kati ya nchi 10 zilizoainishwa.
View attachment 1017237

Hatuna budi kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji nchini. Tuendelee kuiunga mkono serikali yetu kwa kudumisha Amani na Umoja ili kuvutia uwekezaji zaidi na zaidi.
Mazingira ya uwekezaji yalianza kutengenezwa toka enzi ya Mwinyi, akaja Mkapa akayaimarisha, Kikwete akayaimarisha zaidi so awamu ya Tano imekuta misingi ya mazingira ya uwekezaji yapo imara sana. Wao wanatakiwa kuendeleza tu na kurekebisha kasoro ndogo ndogo tu.
 
Ni swali zuri na la msingi, lakini hutaweza kujibiwa.

Kama kuna mtu anayejua, tangu Rais Magufuli aingie madarakani ni wawekezaji wangapi wamewekeza na ni kiasi cha thamani gani uwekezaji huo.

Nadhani kuna umhimu wa kulifanyia utafiti wa kina jambo hili ili tupate takwimu sahihi.
Wakati wa Mkapa hadi Kikwete tulipata wawekezaji wengi kweli kweli LAKINI wengi wao ni matapeli,Richmond,IPTL,ATC ubia na SAA,Buzwagi,Barick na Accacia,Makanikia,Uuzaji wa Vitaro vya gesi asilia,Bomba la Gesi asilia toka Mtwara hadi Dar, Mlimani City,Uvuvi wa samaki bahari kuu,Mabenki fake.
 
Tunapashwa tuangalie sera yetu ya nje ,mahara penye kurekebisha twaweza kurekebisha hili sera zetu za uwekezaji ziweze kustawi.There is a need to revisit our foreign policies.Kwa mfano Tanzania ilipojitoa mikataba ya MIGA je kuna muwekezaji wa nje anaweza kuvutiwa kuwekeza nchini kama kunahitajika kusuruhishwa /Arbitration na mahakama za ndani badala ya mahakama za nje?.Pia kuna swala la confidentiality ya wawekezaji wa nje hawapendi maswala yao muliyowekeana mikataba yawe abrogated kwa sababu za aina yeyote kwa mfano kuwagombanisha na communities ambao hawana ufahamu na vifungu vya sheria vilivyomo kwenye mikataba hiyo.Wanaitaji mazingira ya uwekezaji ambayo yako predictable and not unpredictable.
 
Nina uhakika hakuna mwekezaji hata mmoja wa maana tangu awamu hii iingie. Anayebisha, ataje makampuni makubwa yaliyowekeza katika awamu hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mtu anaeupenda mtaji wake atakuja kuumwaga hapa.

Hata waliopo wanavumilia tu kwa kuwa waliletwa na viongozi wa nyuma na walishaweka uwekezaji wao.
 
Wakati wa Mkapa hadi Kikwete tulipata wawekezaji wengi kweli kweli LAKINI wengi wao ni matapeli,Richmond,IPTL,ATC ubia na SAA,Buzwagi,Barick na Accacia,Makanikia,Uuzaji wa Vitaro vya gesi asilia,Bomba la Gesi asilia toka Mtwara hadi Dar, Mlimani City,Uvuvi wa samaki bahari kuu,Mabenki fake.

Hii ni kweli, na panatakiwa pawe na mjadala wa uchambuzi wa uwekezaji huo kama ulivyogusia juujuu tu. Mjadala huu hapa unataka kujua "ni wawekezaji wangapi," bila kuzungumzia ni uwekezaji wa aina gani.
Natumaini utakuwa umenielewa.

Sasa jitahidi utueleze "ni wawekezaji wangapi wamekuja kuwekeza tangu Magufuli aingie madarakani"

Huo mjadala mwingine wa aina ya wawekezaji, tuuweke kiporo kwanza.
 
Back
Top Bottom