Tanzania yashika nafasi ya 4 kwa nchi ambazo watu wake hawana furaha duniani (2019)

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,315
1,366
Ripoti ya dunia ya nchi ambazo watu wake wana furaha ya mwaka 2019 imetolewa.

Hapa chini ni nchi 10 bora ambazo raia wake wana furaha na zile amabazo raia wake hawana furaha.

Kwa mwaka 2019 nchi amabazo wananchi wake wana furaha zaidi ni:
1. Finland
2. Denmark
3. Norway
4. Iceland
5. Netherlands
6. Switzerland
7. Sweden
8. New Zealand
9. Canada
10. Austria

Katika Ripoti hiyo, nchi 10 ambazo wananchi wake hawana furaha ni :
1. South Sudan
2. Central African Republic
3. Afghanistan
4. Tanzania
5. Rwanda
6. Yemen
7. Malawi
8. Syria
9. Botswana
10. Haiti

Mambo yalizingatiwa katika utafiti huu ni pamoja na: uchumi wa Taifa- country GDP, msaada wa jamii toka kwa ndugu na marafiki, umri wa kuishi (healthy life expectancy), uhuru wa kufanya uhamuzi (freedom to make life choices), ukarimu, kiwango cha ufisadi, na hali ya hisia alikutwa nayo mshiriki wa utafiti huo.

Mambo mengine yaliyotazamwa ni kwa kiwango gani teknolojia inavyoathiri furaha za watu. Katika tafiti huo imeonyesha kuwa vijana wanaoshinda kwenye mitandao wengi wao hawana furaha.

My take:
Kwa nchi za Afrika ambazo ziko kwenye list ya nchi ambazo raia wake hawana furaha ni zile ambazo ziko au zimekuwa kwenye vita kwa muda mrefu au zilikua kwenye msukosuko wa kiuchumi, je Tanzania tunakwama wapi?
 
Furaha ni kitu cha kubadili muda mfupi sana. Tangu huo utafiti ufanyike umepita muda gani?
 
Kuna siku Nyerere alijibu swali akaelezea kuwa serikali haiwezi kuhakikisha furaha ya wananchi, bali inaweza kuhakikisha huduma za jamii.

Jibu lake lilikuwa la kifalsafa kweli.

Kwa sababu, unaweza kumpelekea maji safi mwanamke wa kijijini, halafu kumpelekea maji huko kukamuondolea furaha.

Kwa sababu, nyumbani kwake kabanwa sana, hana uhuru, uhuru pekee anaoupata ni wakati wa kwenda ku hota maji mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukosekana kwa
Zimbabwe
Libya
Mynar
Na kuwepo kwa
Botswana na Tanzania ktk hiyo orodha kunaleta ukakasi
 
Wewe unayesema huu utafiti sio sahihi, unaweza kutuambia ni kwa nini jina la Tanzania liwe ndilo peke yake liko kwenye orodha wakati nchi nyingine za SADC na EAC hazipo? Inasikitisha sana. Nchi nyingine tatu za kwanza zilizotajwa, zote zina vita vinaendelea au zimekuwa na vita miaka ya karibuni. Kama Tanzania hatujawa na vita kwa nini watu wasiwe na furaha? Tena katika nchi zote Africa hakuna nchi yenye rasilimali na fursa nyingi za kutajirika kama Tanzania. Tunakosea wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom