Tanzania yasema haijapuuza sayansi katika mapambano dhidi ya Corona

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tanzania imesema haijapuuza hatua za kisayansi katika kupambana na #COVID19 na haijajitenga na dunia katika jitihada za kutafuta suluhisho la Ugonjwa huo.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, Tanzania haitopuuza matumizi ya dawa zitokanazo na mitishamba kwakuwa bado dunia inatafuta Tiba na Chanjo ya Virusi vya Corona.

Akiwa Paris Nchini Ufaransa ambapo amekutana na Watanzania waishio huko, Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wapuuze habari zisizo na ukweli kuhusu Tanzania kupuuza hatua za kisayansi.

Amesisitiza, "Tunatumia mbinu zote kupambana na maradhi ya mlipuko"

Chanzo: TBC Aridhio
 
Atahangaika kumtetea jiwe mpaka basi. Jiwe anatoa kauli zenye utata wao wanabaki kubadili kauli. Kumtetea na kusema alinukuliwa vibaya.
 
Ameokotwa jalalani atamsikiliza nani? Wa jalalani, alijisema mwenyewe na wala si mimi! Mheshimiwa Mungu.
 
Kuna Sayansi bila takwimu na tafiti? Hawa maprofesa wa Tanzania nadhani Ni maprofesa wabobezi kwenye ujinga na unafiki.
 
Atahangaika kumtetea jiwe mpaka basi. Jiwe anatoa kauli zenye utata wao wanabaki kubadili kauli. Kumtetea na kusema alinukuliwa vibaya.
Wangemuuliza swali moja tu, mmeagiza chanjo kutoka kwa mabeberu? Hatuwezi kutegemea mitishamba pekee wakati kuna chanjo ambazo ziko proven kisayansi
 
Back
Top Bottom