Tanzania yasaini Mkataba na serikali ya Oman | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yasaini Mkataba na serikali ya Oman

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kongosho, Oct 16, 2012.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  nimesikia kwenye taarifa ya habari ITV, Tanzania imesaini mkataba na serikali ya Oman.

  Mkataba huo umewafurahisha sana Oman sababu kuna kipengele cha kulinda mali za wafanyabiashara wa nchi zote mbili.

  Zanzibar itafadhiliwa/saidiwa kwenye elimu ya madaktari, engineering, na walimu.

  Mkataba huo umegusia madini, kilimo na elimu.

  Najiuliza, mkataba huo terms and condition zikoje??

  Madini tunabadilisha na kusomeshewa walimu? Madaktari?
   
 2. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndiyo Tanzania ya sasa. Huwa nachukia sana ninaposikia mkataba umesainiwa na unakuwa ni siri. Sasa kama ni siri kwanini watutaarifu wananchi kwamba wameusaini? Serikali wanapojifanya viongozi wa dini ni tatizo kubwa. Kwa uelewa wangu hapa Tanzania watu wenye haki ya kuongea bila kuulizwa why ni viongozi wa dini wakiwa makanisani au misikitini. Wanasiasa wanatakiwa wahojiwe why popote waongeapo hata kama wanaongea wakiwa kwenye nite dress. Sasa mtu ukiuliza mkataba huo unahusu nini? Uliandaliwa kwa mchakato gani? Nini faida na gharama za mkataba huo kwa walipa kodi wa Tanzania? Ni nini masharti na viggezo vya mkataba huo. Utaambiwa mkataba ni siri. Sheer stupidity why confidentiality whil my tax money will be involved?
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Mikataba yote ya kihuni haitakuwa Valid kuanzia 2015. tukeshe tukiomba tuliondowe hili zimwi CCM madarakani, then ndio tutadeal na huyo Sultan.
   
 4. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kazi kweli kweli. Hii mikataba ya dakika za mwisho. Katiba inasemaje kuhusu mtu/watu kuingia mkataba kwa niaba ya nchi yake TZ?
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huo ni mkataba wa kuueneza Uislam nchini. Shame on you JK ( brain dead idiot president ).
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  sio rahisi hivi kuvunja mikataba valid

  kuna implications zake na inategemea gharama ya kuvunja mkataba ni zipi pia.

   
 7. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni kawaida ya mzee wa farasi Jk
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Hiyo mikataba ya kusilimisha watu ni kwa nini isivunjwe? hata mikataba ya kihuni aliyokwenda kusaini Canada yote inavunjika, hatuko tayari kwa any Implication wakati urithi wa watoto zetu unafanywa gulio.
   
 9. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Biashara ya kupeleka dada zetu utumwani Oman??? Dhaifu mbayaaaaaaaa!
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hata kama haina tija kwa nchi? labda iwe serikali legelege na raisi dhaifu.
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  wamahojiwa Kigoda na yule waziri wa Zanzibar wa elimu, sikuwaelewa na wala hawakunishawishi walichosaini ni nini.

   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mbona JK ameongeza spidi ya kusaini mikataba huko ughaibuni na anafahamu kwamba anaelekea ukingoni katika uongozi wake? kuna agenda gani hapa bandugu?
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Huo mkataba umesainiwa na ulisomwa na kuchunguzwa saa ngapi kama unafaa?si jana tu mkulu kaenda huko na mara anaibuka kusaini mikataba? Nina mashaka...Tusijekuambiwa badae kuwa yalikuwa makosa na nchi imeuzwa..
   
 14. m

  mwl JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 180
  kaazi kwelikweli, hawa ndio baadhi ya GT wa JF hata mikataba hatuwezi kutofautisha?
   
 15. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,725
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nilimwona jana vasodagama na team yake wakiwa wanashangashangaa kweli jumba la mfalme wa oman hadi aibu
   
 16. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,725
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  duh nahisi kama umepotea huku,mida hii ulitakiwa uwe kule chitchat au mmu
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Huyu Sultan ana chumba cha dhahabu hapo ndipo uwazuzuwaga wageni wake malimbukeni wasiojuwa walifuata nini Muscat.

  [​IMG]
   
 18. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Nilistushwa JK na Mawaziri wake walivyokuwa wanashangaa jumba lililo nakshiwa na Dhahabu...yaani wametoa Mimacho hadi aibu... watoto wa Sultan wakawa wanawacheka tu Washamba wapya... Kweli tembea sana ujionee Mengi Jk kinachomtembeza duniani ni Ushamba raha zake ni kwenda kushangaa tu... Sasa hiyo mikataba unasinishwa na Mtu aitwae Sultan? tobaa ah... Alikimbizwa na Sasa keshampa njia ya kurejea Zanzibar sasa kwisha tena...
   
Loading...